Demokrasia huchochea maendeleo

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
Bunge huru hutunga sheria huru na Mahakama huru hutafsiri hizo sheria bila kuingiliwa na mhimili wowote, kuhakikisha sio kandamizi kwa Raia na zinatumika katika maono mapana ya taifa kwa ujumla.

Pia Bunge huiwajibisha Serikali na kuhakikisha matumizi sahihi ya kodi za wananchi, vilevile wanasiasa wanawajibika kutekeleza majukumu yao, na pindi utekelezaji unapokua wa mashaka, huwajibishwa kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Namna hii taifa huendelea kwa kuwa kila mtu anawajibika kadiri ya nafasi yake na kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi husika.
 
Back
Top Bottom