Deleted Files/Folders Katika Computer, Hupelekwa Wapi?

Deleted Files/Folders Katika Computer, Hupelekwa Wapi?

Acha nijaribu, ni kwamba unapodelete file linaenda kwenye recycle bin ambapo kila partition huwa ina recycle bin ambayo huwa iko hidden na hivyo hata kama ukifuta file kwa mfano la mb 500 bado utaona space kwenye partition iko vile vile haiongezeki na ili iongezeke utaenda na kuyafuta kwenye recycle bin ambayo iko kwenye desctop ambayo hukusaidia kuona yale mafaili ambayo yako kwenye hidden recycle bin ya kila partition.

NB: Pamoja na kuwa utayafuta hayatapotea kabisa ila kuna mahali maalumu ambapo yanaenda tena baada ya kufutwa kwenye recycle bin, sasa hapo napo panakusaidia endapo utayahitaji tena utatumia program maalum kuyarudisha pia endapo unataka yapotee permanent kuna software za kufanya hivyo. Ni kwa uelewa wangu tu sijui wengine wanasemaje.

Asante mkuu SuperImpressor!
 
Maelezo mafupi na rahisi ni haya;
utunzaji wa mafaili Kwenye Hdd ni kama uandishi wa kitabu. kuna ukurasa unaitwa yaliyomo (hizi ni references tu)
na kurasa mbali mbali zinafuatia.Ukitaka Habari kihusu jambo fulani unakwenda Kwenye yaliyomo. yaliyomo inakuelekeza ni ukurasa upi.

Ndivyo na Computer ilivyo. computer inakuonyesha yaliyomo kama mafaili ma mafolder.

Kwenye Computer katika kufuta mafaili; maelekezo ( references tu) yaliyo kwenye yaliyomo ndo yanaondolewa na ukurasa unabaki kama ulivyo, japo computer inaweza kuandika tena katika ule ukurasa na kuuingiza kwenye listi ya yaliyomo tena!

Nimeyapenda maelezo na mfno wako mkuu, kwa watu wa kawaida wanakuelewa kiurahisi zaidi! Mia.
 
Asanteni sana wataalam coz hadi sasa naendelea kulicover mafile yangu. Nashukuru sana JF nitawapa matokeo
 
Japo kwa teknolojia za siku hizi njia nzuri kabisa ni kuihsribu kabisa hard disk. Nimewahi ona kompyuta imekuwa fomated kabisa na operating system nyingine ikawekwa, baadae ikaonekana data zilizokuwa mwanzo kwenye hard disk ni za muhimu na zinahitajika, hapakuwa na back up. Mkuu software ilitumika kuzipata.

Ukiformat HDD siyo kwamba ndiyo ume-clear kila kitu, ukitumia hata PANDORA tu inakurejeshea asilimia kubwa ya files zako!!
 
Japo kwa teknolojia za siku hizi njia nzuri kabisa ni kuihsribu kabisa hard disk. Nimewahi ona kompyuta imekuwa fomated kabisa na operating system nyingine ikawekwa, baadae ikaonekana data zilizokuwa mwanzo kwenye hard disk ni za muhimu na zinahitajika, hapakuwa na back up. Mkuu software ilitumika kuzipata.
na ndo maana nikasema the only way ni kutumia program maalum kufuta hizo data ingawa kwa technologia ya siku hizi bado si kitu ila kwa kudelete huku kwa kawaida tu au ku format tu hata kwa kutumia trial version za software nyingi tu unaweza recover..
 
Mkuu sijui nini, nafikiri kuwa neno 'DELETE' kwa maana ya 'futa' ukihusisha majibu mbali mbali yaliyotolewa ktk thread hii si sawa kutumika; neno zuri labda lingekuwa 'MOVE' kwa maana ya kuhamisha file kutoka sehemu lilipo kwenda ktk 'trash can'. Nasema hivi kutokana na sababu kuwa, unaweza kutumia a special program kupata tena file lako lililopelekwa ktk 'pipa la uchafu'.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sijui nini, nafikiri kuwa neno 'DELETE' kwa maana ya 'futa' ukihusisha majibu mbali mbali yaliyotolewa ktk thread hii si sawa kutumika;

neno zuri labda lingekuwa 'MOVE' kwa maana ya kuhamisha file kutoka sehemu lilipo kwenda ktk 'trash can'. Nasema hivi kutokana na sababu kuwa, unaweza kutumia a special program kupata tena file lako lililopelekwa ktk 'pipa la uchafu'.

unachosema ni sahihi ila kumbuka si watumiaji wote wa pc wanahitaji details on how pc works ndo waitumie..kumbuka mtumiaji wa kawaida kabisa yeye anataka simple language inayoeleza kufanyika kile anachokiona kwenye screen yake..

kwamba aki delete basi kiondoke kiende sehem maalum ya uchafu na akisafisha uchafu basi aone kwenye screen yake uchafu umetoka na nafasi ipo wazi..

thats all! hayo mambo mangine ya kutaka kujua what happened huko nyuma ni vurugu za professionals tu na ndo huko sasa mtu anapofuta faili zake kwa bahati mbaya inabidi aende kwa mtu huyu anaejua nini kinafanyika behind the scenes ili aweze kukurudishia data zako,

sanasana na pale tu inapohitajika kupatikana hizo data kama kwenye mambo ya upelelezi huko nk...so ku accomplish this ndo maana watengeneza program wengi wanatengeneza program with just simple commands..delete, move, cut, copy, n.k..ili yule mtumiaji wa kawaida kabisa aelewe nini anafanya...ila ukitaka kujua kwa undni zaidi ndo hapo ujifunze zaidi..

ukitaka kila kitu kiwekwe wazi (kama watu wengi wanavyoamini kwa linux os zilivyo) basi watumiaji wa pc wangekuwa wachache sana..
 
Wataalam:
Unajua sisi wengine huwa delete ili Computer ipunguze mzigo, na mnaposema files zitaendelea kuwepo
ina maana ipo siku Computer itajaa kabisa (kwa maana ya capacity) yake, na hivyo kuhitaji hatua nyingine
kabisa.........................?

cc: sijui nini, Mlamoto
 
Last edited by a moderator:
Inategemea na format yenyewe na kama data zengine zimesharekodiwa juu yake. Ila download Easeus Data Recovery Free Edition Best data recovery software, recover deleted or lost files - EaseUS Data Recovery Family.

Install kisha run na chagua Complete Recovery, chagua aina ya file unazotaka kurecover au chagua zote, chagua drive yako, itafanya search ya drive nzima,

hii inaweza kuchukua muda mrefu sana masaa 7 au zaidi, mwishoni utaweza kuona file ambazo kuna uwezekano wa kuziokoa. Free version inaokoa hadi 1GB of files hivyo chagua zile za muhimu tu.

mkuu nashukuru sana sasa nimepata hizi 1 G lakini bado nahitaji zaidi ya 315 G hasa hizi picha. Nifanye nini ili nipate kununua online sina uzoefu. Hakuna namna ambapo naweza kuzicopy coz zinafunguka full kama kuna mode naweza copy naomba msaada ili nizipate hizi picha naomba sana.
 
Wataalam:

Unajua sisi wengine huwa delete ili Computer ipunguze mzigo, na mnaposema files zitaendelea kuwepo
ina maana ipo siku Computer itajaa kabisa (kwa maana ya capacity) yake, na hivyo kuhitaji hatua nyingine
kabisa.........................?

cc: sijui nini, Mlamoto
mkuu, fuatilia kwa makini comments zilizotolewa hapo juu zimejitosheleza kabisa...ni kwamba :

unapodelete file kwenda kwenye recycle bin ni sawa na ulimove tu kutoka lilipokuwa kwenda kwenye recycle bin..kwa hiyo ile nafasi iliyokuwa inatumiwa na faili lile inabadilika jina tu ila occuped space inabaki vilevile..

sasa unapoliondoa na kwenye recycle bin ni kwamba unafuta njia zote za hilo file kuwa opened again kwa njia ya kawaida na ile nafasi yake inakuwa marked kuwa empty adress (ingawa lile file lipo) na hii empty adress inaweza kutumika kwa kuhifadhi data zingine,

hivyo hili file ulilolifuta sasa linakuwa kwa lugha rahisi ni kama lipo hewani hivi linaelea(mahali maalum)...na linaweza kufunguliwa si kwa njia ile ya kawaida tena bali mpaka kwa program maalum ya kuweza kuliona ..

na upatikanaji wake unategemea na kadri unavyozidi kuingiza na kufuta mafaili mengine kwenye hdd yako maana kadri ya kuingiza na kufuta mafili yako ndvyo unavyozidi kulisukuma lile file la kwanza kuwa deletd kwenda mbalimbali zaidi na kupoteza uwezekano wa kulipata

(labda uzidi kutumia more powerful tools za ku restore) na ndo maana kuna mdau hapo juu alisema ikitokea bahati mbaya umedelete(empty recyecle bin au format) kitu unachokihitaji bado ni vema usiendelee kuitumia zaidi hiyo hdd kwanza maana restore programs nyingi zinaende kwa order ya time file lilipokuwa deteted...so likiwa mbali zaidi si ajabu program zetu hizi za kawaida za ku recover ikashindwa kulifikia ...

kwa technolojia za wenzetu huko unakuta kuna program zinaweza kurudisha data za hata tangu hdd ilipoanza kutumika from factory (tho sina hakika sana kwa hili) na ndo maana unakuta wale watu wanaofanya mambo yasiotakiwa kubakiza ushahidi wowote wana iharibu kabisa hdd kwa kuivunja vunja completely sababu ikipatakina tu watu wanaona kila kitu kilichoingia humo..

so kwa kujibu swali lako ni kuwa uwezo wa kujaa eti kwa sababu unaingiza data na kuzifuta hivyo zile unazozifuta kujaza nafasi si kweli maana inafika hatua nafasi ilele moja uliyoweka data ya kwanza na kufuta itatumika kuweka data ingine na ukifuta itakuwa allocated kwa data ingine nk...

ila tu kaa ukijua hakuna kitu kisicho na lifespan..itafika tu hatua hdd yenyewe itachoka hiyo write-delete action na ku fail...ingawa ni baada ya mda mrefu sna ikichangiwa na factors nyingine nyingi mf kugongwa gongwa nk..hapo ndipo unakuta pc ina detect kabisa hdd inakaribia ku fail

(nilishashuhudia hii kwa macho yangu kwa pc ina kama miaka 7 sahizi inalete error flani hivi kuwa hdd fail ipo karibu back up your data mapema na nilijaribu kufanya kila kitu kuiokoa ila wapi mpaka kuchange kwenye pc zingine tofautitofauti..error still there mpaka leo naitumia kama flash tu)
 
mkuu nashukuru sana sasa nimepata hizi 1 G lakini bado nahitaji zaidi ya 315 G hasa hizi picha. Nifanye nini ili nipate kununua online sina uzoefu. Hakuna namna ambapo naweza kuzicopy coz zinafunguka full kama kuna mode naweza copy naomba msaada ili nizipate hizi picha naomba sana.
ninayo program ya recovery flani hivi ngoja niipekuwe kenye store yangu nita ku attachia hapa uitumia na keys zake..
 
Wataalam:
Unajua sisi wengine huwa delete ili Computer ipunguze mzigo, na mnaposema files zitaendelea kuwepo
ina maana ipo siku Computer itajaa kabisa (kwa maana ya capacity) yake, na hivyo kuhitaji hatua nyingine
kabisa.........................?

cc: sijui nini, Mlamoto

Haiwezekani kujaa!
 
Last edited by a moderator:
Hakika nimepata darasa kupitia thread hii.
Kumbe ktk akili ya kawaida unaweza dhani kuwa file lako la siri umelifuta, kumbe lipo ktk system ya computer!
 
mkuu, fuatilia kwa makini comments zilizotolewa hapo juu zimejitosheleza kabisa...ni kwamba :

unapodelete file kwenda kwenye recycle bin ni sawa na ulimove tu kutoka lilipokuwa kwenda kwenye recycle bin..kwa hiyo ile nafasi iliyokuwa inatumiwa na faili lile inabadilika jina tu ila occuped space inabaki vilevile..

sasa unapoliondoa na kwenye recycle bin ni kwamba unafuta njia zote za hilo file kuwa opened again kwa njia ya kawaida na ile nafasi yake inakuwa marked kuwa empty adress (ingawa lile file lipo) na hii empty adress inaweza kutumika kwa kuhifadhi data zingine, hivyo hili file ulilolifuta sasa linakuwa kwa lugha rahisi ni kama lipo hewani hivi linaelea(mahali maalum)...na linaweza kufunguliwa si kwa njia ile ya kawaida tena bali mpaka kwa program maalum ya kuweza kuliona ..na upatikanaji wake unategemea na kadri unavyozidi kuingiza na kufuta mafaili mengine kwenye hdd yako maana kadri ya kuingiza na kufuta mafili yako ndvyo unavyozidi kulisukuma lile file la kwanza kuwa deletd kwenda mbalimbali zaidi na kupoteza uwezekano wa kulipata (labda uzidi kutumia more powerful tools za ku restore) na ndo maana kuna mdau hapo juu alisema ikitokea bahati mbaya umedelete(empty recyecle bin au format) kitu unachokihitaji bado ni vema usiendelee kuitumia zaidi hiyo hdd kwanza maana restore programs nyingi zinaende kwa order ya time file lilipokuwa deteted...so likiwa mbali zaidi si ajabu program zetu hizi za kawaida za ku recover ikashindwa kulifikia ...

kwa technolojia za wenzetu huko unakuta kuna program zinaweza kurudisha data za hata tangu hdd ilipoanza kutumika from factory (tho sina hakika sana kwa hili) na ndo maana unakuta wale watu wanaofanya mambo yasiotakiwa kubakiza ushahidi wowote wana iharibu kabisa hdd kwa kuivunja vunja completely sababu ikipatakina tu watu wanaona kila kitu kilichoingia humo..

so kwa kujibu swali lako ni kuwa uwezo wa kujaa eti kwa sababu unaingiza data na kuzifuta hivyo zile unazozifuta kujaza nafasi si kweli maana inafika hatua nafasi ilele moja uliyoweka data ya kwanza na kufuta itatumika kuweka data ingine na ukifuta itakuwa allocated kwa data ingine nk...

ila tu kaa ukijua hakuna kitu kisicho na lifespan..itafika tu hatua hdd yenyewe itachoka hiyo write-delete action na ku fail...ingawa ni baada ya mda mrefu sna ikichangiwa na factors nyingine nyingi mf kugongwa gongwa nk..

hapo ndipo unakuta pc ina detect kabisa hdd inakaribia ku fail (nilishashuhudia hii kwa macho yangu kwa pc ina kama miaka 7 sahizi inalete error flani hivi kuwa hdd fail ipo karibu back up your data mapema na nilijaribu kufanya kila kitu kuiokoa ila wapi mpaka kuchange kwenye pc zingine tofautitofauti..error still there mpaka leo naitumia kama flash tu)

Asante sana kwa maelezo, na kuna mdau Mlamoto amemaliza kabisa kwa kusema haiwezi kujaa.
Msinichoke bado mgeni kwenye hayo mambo:

Kama ndiyo hivyo ni kama hakuna limit (ukiacha lifespan), vipi kuhusu hizi capacity unaambiwa Hard disk gb5, Ram and Hdd so on hiyo haimaanishi kwamba kuna limit kuhifadhi data?

ndiyo maana sisi bila kujua tuna-delete tukidhani tunameondoa kila kitu ili kupata space kubwa (hasa tunapoona computer inakuwa slow), kwa maelezo mengine hiyo HDD ukiacha life span haiwezi kujaa kabisa na kutoruhusu trash kutoka recyclebin ziingie?
 
Mkuu platozoom, ebu pitia post zote tangu mwanzo; hata mimi ambaye sina utalaamu wa IT nimeelewa vema.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom