Deleted Files/Folders Katika Computer, Hupelekwa Wapi?

Iselamagazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
6,083
Reaction score
6,234
Salaam wana Jamvi!

Deleted files au folders katika hard drive, nadhani upelekwa katika recycle bin (trash can).

Napenda kujua: Baada ya matumizi ya PC kwa muda mrefu, je system ya computer au tuseme trash can haiwezi kujaa deleted files au folders na hivyo kuchukua space kubwa na kusababisha performance ya PC kuwa ndogo?

Ikiwa jibu ni HAPANA, je deleted files/folders upelekwa wapi?

Wataalamu wa IT au yeyote yule anayejua hili anijuze!
 
Acha nijaribu, ni kwamba unapodelete file linaenda kwenye recycle bin ambapo kila partition huwa ina recycle bin ambayo huwa iko hidden na hivyo hata kama ukifuta file kwa mfano la mb 500 bado utaona space kwenye partition iko vile vile haiongezeki na ili iongezeke utaenda na kuyafuta kwenye recycle bin ambayo iko kwenye desctop ambayo hukusaidia kuona yale mafaili ambayo yako kwenye hidden recycle bin ya kila partition.

NB: Pamoja na kuwa utayafuta hayatapotea kabisa ila kuna mahali maalumu ambapo yanaenda tena baada ya kufutwa kwenye recycle bin, sasa hapo napo panakusaidia endapo utayahitaji tena utatumia program maalum kuyarudisha pia endapo unataka yapotee permanent kuna software za kufanya hivyo. Ni kwa uelewa wangu tu sijui wengine wanasemaje.
 
Maelezo yako sahihi mkuu,mimi kinachonichanganya ukishafuta ktk recycle bin kwanini uki2mia recovery program una uwezo ya kuyarudisha wakati ushafuta maana yake kuna link kati ya huko yalipo na comp.
 
Lol! Unapofuta file haliondoki katika sector lilipohifadhiwa, kinachobadilika ni entry tu, OS yako inabadili anuani kutoka say "my documents" kwenda "trash", hivyo sector ya hdd lilipohifadhiwa hilo file inakuwa bado na kitu kilekile kama kilivyohifadhiwa kuondoa anuani tu.

Hivyo basi, uki-empty recycle bin yako unafuta hata hiyo anuani ya pili "recycle bin" hivyo inakuwa ngumu kulitrace file lako kiurahisi, lakini si kwamba file limetoweka kabisa, linabaki palepale kwenye sector ileile, na computer ita-asign jina maalum katika file lako,

computer itakwepa kwa kadri iwezekanavyo kuandika data nyingine katika sector hiyo, hivyo katika muda huo ukitumia software maalum inalocate file lako na inaweza kulirejesha kwa kulipa anuani nyingine!
 
well said mkuu...the only way unaweza ku delete mafaili yako permanently kwenye pc ni kwa kutumia program maalum za kufuta na si hii right click delete..au delete ya kawaida...hata ku epmty recycle bin never deletes the file permanently..its just allocation ya file space addresses..
 
recycle bin ni sawasawa na desktop.. Ni part mojawapo ya hdd.. So unapodelete vikaenda kwa recycle bin unakuwa hujadelete.. Unakuwa ni sawasawa na ku-move folder kutoka huku na kupeleka kule..

Na ndo maana ukidelete file kuuubwa inakwambia"mzee!, huu mzigo ni mkubwa.. Tutaudelete moja kwa moja" hivyo huwezi kurestore..

Ndo maana kama hdd yako ina wino mwekundu.. Ukidelete kitu kikaingia kwa recycle bin.. Nafasi haipungui
 
Unapofuta kutoka recycle bin eneo la disk ambapo file lipo linakuwa marked kuwa linaweza kutumika kwa kuhuifashi data zengine, na ukiwa unasave mafile mengine liaweza kkuhifadhiwa sehemu hiyo. Ndo maana kanununi kuu ukiwa umepoteza files ni kutotumia hiyo HD kwa kitu chochote maana unaongeza chance za kulipoteza kabisa hilo file.

Program za kufuta kabisa kabisa kama Eraser zinafanya kazi kwa kuandika juu ya hilo eneo la file na random data hivyo kupoteza original file na kulifanya lizeweze kuokolewa.

Hii procedure inafanya na makampuni wanapotaka kutupa au kuuza vifaa vyenye harddrive kuzuia data ku leak pamoja na njia nyingine kama Degausing ambayo inatumia nuvu za sumaku kuiharibu HD na Hardrive Shredding ambayo inavunja vunja HD kama shredder ya makaratasi.

Last edited by a moderator:
Lol! Unapofuta file haliondoki katika sector lilipohifadhiwa, kinachobadilika ni entry tu, OS yako inabadili anuani kutoka say "my documents" kwenda "trash", hivyo sector ya hdd lilipohifadhiwa hilo file inakuwa bado na kitu kilekile kama kilivyohifadhiwa kuondoa anuani tu.

Hivyo basi, uki-empty recycle bin yako unafuta hata hiyo anuani ya pili "recycle bin" hivyo inakuwa ngumu kulitrace file lako kiurahisi, lakini si kwamba file limetoweka kabisa, linabaki palepale kwenye sector ileile, na computer ita-asign jina maalum katika file lako,

computer itakwepa kwa kadri iwezekanavyo kuandika data nyingine katika sector hiyo, hivyo katika muda huo ukitumia software maalum inalocate file lako na inaweza kulirejesha kwa kulipa anuani nyingine!

Dah yaani umenijibu vile nilivyokuwa nataka big up mkuu!!
 
Sasa wakuu nashukuru kwa hii elimu, mimi kwenye pc yangu huwa natumia external sasa mwezi January mdogo wangu nikakuta amedelete yote kwenye external na imebadilika na jina kabisa. Sasa sijui aliformat au alidelete sasa hii external ilikuwa na very important document sasa je mwaweza nisaidia namna ya kurudisha hizi document. Natanguliza shukrani
 
Inategemea na format yenyewe na kama data zengine zimesharekodiwa juu yake. Ila download Easeus Data Recovery Free Edition Best data recovery software, recover deleted or lost files - EaseUS Data Recovery Family.

Install kisha run na chagua Complete Recovery, chagua aina ya file unazotaka kurecover au chagua zote, chagua drive yako, itafanya search ya drive nzima,

hii inaweza kuchukua muda mrefu sana masaa 7 au zaidi, mwishoni utaweza kuona file ambazo kuna uwezekano wa kuziokoa. Free version inaokoa hadi 1GB of files hivyo chagua zile za muhimu tu.
 
Asanteni watalaamu wa IT; na mimi hapa naendelea kupata darasa taratiiiiibu.
Mkuu unayefanya PhD kuhusu kufuta mafaili na mafolda ktk Compyuta, leta mchango wako mapema.
 
Mpaka mtu kufanya PhD hajui filing system za computer zinavyofanya kazi? indexing
na MFT and the like for other Os. kweli elimu yetu uchwara.
 
Lol! Unapofuta file haliondoki katika sector lilipohifadhiwa, kinachobadilika ni entry tu, OS yako inabadili anuani kutoka say "my documents" kwenda "trash", hivyo sector ya hdd lilipohifadhiwa hilo file inakuwa bado na kitu kilekile kama kilivyohifadhiwa kuondoa anuani tu.

Hivyo basi, uki-empty recycle bin yako unafuta hata hiyo anuani ya pili "recycle bin" hivyo inakuwa ngumu kulitrace file lako kiurahisi, lakini si kwamba file limetoweka kabisa, linabaki palepale kwenye sector ileile, na computer ita-asign jina maalum katika file lako,

computer itakwepa kwa kadri iwezekanavyo kuandika data nyingine katika sector hiyo, hivyo katika muda huo ukitumia software maalum inalocate file lako na inaweza kulirejesha kwa kulipa anuani nyingine!

maelezo yako unapata 98%
 
well said mkuu...the only way unaweza ku delete mafaili yako permanently kwenye pc ni kwa kutumia program maalum za kufuta na si hii right click delete..au delete ya kawaida...hata ku epmty recycle bin never deletes the file permanently..its just allocation ya file space addresses..

Japo kwa teknolojia za siku hizi njia nzuri kabisa ni kuihsribu kabisa hard disk. Nimewahi ona kompyuta imekuwa fomated kabisa na operating system nyingine ikawekwa, baadae ikaonekana data zilizokuwa mwanzo kwenye hard disk ni za muhimu na zinahitajika, hapakuwa na back up. Mkuu software ilitumika kuzipata.
 
Maelezo yako sahihi mkuu,mimi kinachonichanganya ukishafuta ktk recycle bin kwanini uki2mia recovery program una uwezo ya kuyarudisha wakati ushafuta maana yake kuna link kati ya huko yalipo na comp.

NAdhani naungana na wewe mkuu[MENTION]mndengereko[/MENTION], nadhani hata kama umezidelete huwa bado zinaendelea kubaki humo humo kwenye hard disk.
 
Maelezo mafupi na rahisi ni haya;
utunzaji wa mafaili Kwenye Hdd ni kama uandishi wa kitabu. kuna ukurasa unaitwa yaliyomo (hizi ni references tu)
na kurasa mbali mbali zinafuatia.Ukitaka Habari kihusu jambo fulani unakwenda Kwenye yaliyomo. yaliyomo inakuelekeza ni ukurasa upi.

Ndivyo na Computer ilivyo. computer inakuonyesha yaliyomo kama mafaili ma mafolder.

Kwenye Computer katika kufuta mafaili; maelekezo ( references tu) yaliyo kwenye yaliyomo ndo yanaondolewa na ukurasa unabaki kama ulivyo, japo computer inaweza kuandika tena katika ule ukurasa na kuuingiza kwenye listi ya yaliyomo tena!
 
Back
Top Bottom