Sasa Cpt Hadock, nini hitimisho lako?
Blistering Barnacles,
Hoja yangu ni kuhoji aliyesema kuwa TANESCo isinunue mitambo mikuukuu au michakavu. Mimi nikauliza, ilikuwaje tukaingia mkataba wa kuzalishiwa umeme kwa kutumia mitambo mikuukuu?
Je kama mfanp Richmond wangeweza kufanya kazi yao na hawakuwa kampuni ya mazabe, lakini wakatumia mitambo mibovu na chakavu, je pale ambapo wangeshindwa kuzalisha umeme inavyotakikana kutokana na ubovu huo tungemlaumu nani?
Or in other owrds, kwa nini Serikali huruhusu kukodisha mitumba mfano kama ule wa ATCL kukodisha Airbus lililochoka lakini tukaingia gharama karibu sawa na kununua ndege mpya?
That is my point Jellyfish!
Mwinyi ni wa pwani zitto ni wa bara, hahisi wala haogopi mtu kuwa nyuma yake hahaha!
Ninayo machache dhidi ya Mhe. wangu Zitto. Kwanza nikubaliane na wewe Rev.Kishoka, Zitto ni charismatic leader to be. Zitto ana malengo, malengo lazima yapaliliwe kabla ya kufikiwa. Kupalilia kwa Mhe.Zitto, ni kujidhihirisha mbele ya wtz kwa yale anayoyatetea kwa maslahi ya umma. Unapopalilia malengo yako, kuna vikwazo njiani, kwanza, wasiopenda mtizamo wako watakuzulia mabaya ili kukuchafulia juhudi zako. Au kama hauko kwenye system yao kwa lugha rahisi kama si mwenzao basi watajiunga pamoja kwa lengo la kukumaliza. Haya yamefanyika dhidi ya zitto, kasimamishwa Bungeni, akina Matlida Burian mashangingi ya Chama yakishangilia tukio hilo. Lakini umma wa wtz, ulikuwa nyuma yake, wapiga kura wake wako pamoja naye. Tumpe support, tunamkosoe pale anapofanya ndivyo sivyo, tumsaidie kumnyooshea njia apite bila matatizo na kufika kwenye enzi (Urais) anazochugulia bila kukwama. Ni kiongozi, ni mzalendo, ana sifa, ana uchungu na nchi yake, tujiandae kumkabidhi rungu, rungu hilo liwapige Mafisadi wa RICHMOND, KAGODA, RADA, NDEGE YA RAISI, TICTS, IPTL na wenzi wengine wa mali ya umma. Lazima atufikishe pale tunapotaka kwenda, Maisha bora kwa wote
Jokakuu,
Zitto na Omarilyas ni watu wawili tofauti. Wote wanatumia majina yao halisi. Omarilyas alikuwa anatumia nick ya Tanzanianjema zamani ila akaamua kubadili na kutumia jina lake la kweli ambalo ni Omar Ilyasi.
Omar na Zitto wote wamesoma mlimani na ni marafiki wakubwa sana. Kama wanajua pw za kila mmoja na kuzitumia hapa, hilo siwezi kujua na sina hata chembe ya uthibitisho. Wakati mwingine inakuwa too convenient kwa Omar kuingia hapa kila mara zitto anapobwana. Je ni zitto anaingia kwa jina la Omar? Sina jibu katika hili ingawa ukweli ni kuwa Zitto na Omar ni watu walioko karibu sana na unaweza kudhani kuwa wanafikiri sawa.
Tofauti ya Zitto na Omar ni kwamba, Zitto ni mbunge lakini pia ni mpinzani wa ccm kisiasa (ni mwanachadema) ila Omar hajui kama awe mpinzani au awe mwanaccm.
Omar hana cha kupoteza baada ya kujitoa kwenye staff ya Zitto kiaina kwa hiyo hana ukaribu wowote na chadema na hajali kitakachotokea huko chadema. Mara nyingi nimekuwa namuuliza kama anachoandika ni mawazo yake binafsi au ni ya Zitto lakini amekuwa hasemi.
Wanaomfahamu Omar kama mimi, wanajua anachotaka - anataka kula pande zote mbili (za ccm na chadema). Usishangae sana kusoma anachoandika humu.
Habari ndiyo hiyo.
I am bussy, but will come back to you SOOOON. Pamoja na haya pia nitazungumzia "MAPANA YAKE" suala la the so called Zittos Rants on wachaga ambalo kwa makusudi mazima mmendelea kulikuza mkidhani mnamharibia yeye kumbe mnajimaliza wenyewe. Administrator naomba ukae pembeni kama ulivyoacha haya.....
omarilyas
Omar
Achana na mambo ya CHADEMA waachie wenyewe kama sio mwanachama. Labda wameamua hivyo kukaa hivyo, au anzisha chama chako na Zitto bila shaka atakushauri au kukufuata. Unatachanyia habari pasipo sababu.
Tenganisha urafiki wako na Zitto na shughuli za CHADEMA.
Kaka ulitaka nimjibu vipi.
Zitto amehangaika huko alikohangaika akapata mkataba. akarisk maisha yake akaulipua. Akapewa adhabu ambayo ikawarudi wale waliompa na kuwapa nafasi nzuri CHADEMA kufaidika kisiasa. Zitto kama angekuwa oppurtunist basi angeamua kung'ang'ania hiyo ni ajenda yake na asingeamaua kuwapa jukwaa alilolitengeneza kwa gharama kubwa wakubwa zake kina Mbowe, Silaa, Mrema, Hamad Rashid na wengine wengi hapa.
Wengine wakaamua kujilundikia ajenda zingine bila hata kushughulikia hiyo na kujua mwisho wake. Sasa hizo ajenda walizorukia tayari wameporwa. Cha ajabu badala ya kuwa creative kuja na ajenda zingine zenye maana zaidi kwa watanzania, wameng'ang'ania na ajenda hiyohiyo wakati wakijua wazi hawana umma wala uzito wa kimadaraka wa kuweza kufikisha hiyo ajenda to the conclusion.
Kama wao pamoja na hao washikaji zao kina Mwakyembe wameshindwa kushughulikia hayo wanayoyapigia kelele, iweje wategemee Zitto asimamishe ya Buzwagi. Tena wanadhani atawezaje kufanya hivyo wakati wao wenyewe wako bize kumpiga vita wakijidanganya kuwa eti watammaliza kisiasa kumbe wanasaidia wengine kuwamaliza wao kama chama. Yaani hawa wote wamebebwa mgongoni na Zitto huyohuyo kuingizwa CHADEMA sasa wanajidanganya kuwa eti wao ndio wenye chama. Huyo Mzee Mtei mwenyewe hathubutu kujiona hivyo itakuwa hawa.
Sasa yamewashinda wanaanza kutafuta mchawi kwa Zitto na wengine. wakiambiwa ukweli kuwa wanasumbuliwa na majungu na fitina za kina Kiranja aka Mpakakieleweke pamoja na ugoigoi wa kimikakati wanaishia kusema wanatukanwa.
Wanaona wao ndio wana haki ya kumtukana na kumzushia kila uozo na kugeuza maneno ya Zitto kila wakati wakitegemea Zitto hatakuwa tayari kuwajibu kwa maslahi ya chama chake.
Sasa mimi sina loyalty ama kwa chama chao au mwenyekiti wao. And they know it. Hapo zamani nilikuwa ninaamini kuwa wanaweza kuwa chachu ya mbadala makini kwa watanzania kuchagua. Lakini sasa ni wazi kuwa tusipokuwa makini sisi basi tutaletewa bora mbadala ambao utaishia mambo ya NARC Kenya ya IT'S OUR TURN TO EAT...
Kama nina haki ya kukosoa uvundo wa CCM vilevile nina haki ya kukosoa uozo wa CHADEMA kabla nao haujageuka uvundo.
Kaka najua na wewe pia ungetamani kuona mbadala makini out of CHADEMA. Samahani kwa kukukwaza lakini kamwe siwezi kuacha kuwakosoa hawa kwa manufaa ya watanzania.
Ili tuweze kufanikisha matunda ya siasa za demokrsia ya vyama vyingi tunahitaji mbadala makini kutoka katika chama chenye utashi wa kuleta mabadiliko ya kweli na sio bora mbadala usio na tija na pengine yakawa na athari zaidi kwa Tanzania yetu.
Hawa jamaa wanapaswa kukaa chini na kufanya self reflection ya matatizo yao badala ya kukimbilia kutafuta mchawi kwa Zitto ama Omarilyas. Wachawi wao wenyewe wakiongozwa na sumu mbaya za Kiranja aka Mpakakieleweke....
Kuhusu kumuongelea Zitto, as long as wanakuja hapa na kwengineko na uzandiki wao i will not stop deciphering their cheap and loosy spinnings.....Kama wao wanadhani wana haki ya kumpaka uozo wao wa Zitto basi nami nina haki ya kupambana na uozo wao.
Na wewe bana...sasa "undavyaundavya" ndio nini maana'ake?
Hivi what is wrong with these guys.......Kiranja, Omarlyasi,Mwafrika,Mpaka Kieleweke and Zitto on the other hand......?
These guys seem to know one another quite well! Anzisheni chama chenu or kama mpo chama kimoja gawane chama hicho then kila upande ulete upinzani wa kweli kwa manufaa ya nchi nzima!
NL,
Naona unataka kuchanganya madawa.
Kuna makasa kibao yamechanganywa kwenye madesa yanayotumiwa (lugha ya vijana wa mlimani) na miongoni mwa watu uliowataja hapo juu.
Mimi binafsi sijasema kama namjua Kiranja na Mpaka kieleweke hapa JF. Naweza kudhani kuwa nawafahamu, but, until wamejitambulisha wenyewe hapa, hizi zitabaki hisia tu.
Omar kakoroga mambo kwa kusema kuwa Kiranja ndiye Mpaka kieleweke. Jambo ambalo sio tu kuwa hana uhakika nalo, bali pia, ni kinyume cha sheria za JF.
Zitto kalishwa kasa kwa kudhani kuwa mimi ni mbunge mwenzake ndani ya chadema (kitu ambacho Omar anasisitiza kwa kuniita mimi kuwa ni mdogo wake wa kike ndani ya chadema).
Zitto na Omar Ilyas wanatumia majina yao halisi kwa hiyo haikuhitaji sayansi ya maroketi kuwatambua hapa jamvini. Tafadhali usichanganywe na misinformation zinazotolewa hapa na Omar hapa kuhusu wanachama wa JF ambao hawajajitambulisha hapa kwa majina yao halisi.
Huu ni mchezo anao ucheza Omar kwa kudhani kuwa anamsaidia rafiki yake Zitto. Otherwise, mimi nilishajua anachokicheza Omar hapa - anataka sana kuivuruga chadema kutokea ndani. Soma sana anachoandika na utaiona hii nia yake kwa uwazi zaidi.
Too low and personal!
how low and how personal?
Just read the posting you will figure it out!. Mtu akienda personal sio lazima na wewe uende personal. Tutashindwa kuwatofautisha.
Anyway umeme umekatika hapa Mbagala. Kwaheri
Tuangalie mpira wa Taifa stars na Pharaos