DED Tunduru aamua kufanya unyama

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,091
6,100
Kama ilivyoripotiwa jana mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru amempeleka mwl. wa shule msingi Mrusha polisi ameteswa huko polisi ameshinda njaa na mateso mengine yasiyoelezeka.

Tangia asubuhi alishinda polisi usiku wa saa 4 alipelekwa na gari ya Halamashauri nyumbani kwake kupekuliwa wakarudi naye mjini na kulala rumande hawakumpa taarifa hata mkuu wake pale shuleni. Hawaruhusu mdhamana, yamekuwa km ya Mbowe. Kisa ni taarifa iliyoandikwa hapa JamiiForums juu ya walimu wapya pale Tunduru kunyanyaswa kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Utumishi na Mwanasheria wa Halmashauri aitwaye kwa jina moja Walter.

Huyu bwana kiukweli ndio kawaida yake kuchukua pesa za walimu wapya kiasi cha Shs 82,000/ kila moja kwa vitisho kuwa usipoitoa hutasajiwa ktk mfumo wa ajira. Tulitegemea Mkurugenzi angewachukulia hatua kinyume chake waliochukuliwa pesa wamegeuziwa kipande wakishirikiana na polisi wasio waaminifu pale wilyani Tunduru. Ni walimu wengi waliwatoa pesa kwa njia ya vitisho kuwa wasingesajiliwa, sijui kigezo gani wametumia kumzushia kesi ya uwongo huyu moja.

Mwalimu wetu bado ameshikiliwa polisi hakuna mdhamana hatakiwi mtu kumsogelea wamemchukulia simu yake. Nijui km atatoka akiwa mzima tumwombee. Ana watoto wadogo wawili moja yuko chekechea na anaumwa mwingine yuko darasa la kwanza haijulikani wako ktk hali gani na km wanapata chakula na wamelala wapi ukizingatia moja mdogo ndio mgonjwa. Huu unyama anaoufanya Gasper Zahoro Balyomi(Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru) haujafanywa hata na Adolf Hitler.

Tuna viongozi wanawake lakini inaonekana hawana hata huruma, Rais mama, waziri wa Elimu mama, waziri wa TAMISEMI mama lakini tumeandika hatuoni hatua yoyote.

Wallahi nimemkumba hayati Magufuli haya yasingewezekana. kuna mkuu wa Wilaya, RAS na Mkuu wa Mkoa tena Brigedia Jenerali wa JWTZ Mkurugenzi wa Wilaya ni nyau wa aina gani ktk nchi hii? Halafu anaongea lugha ya kibaguzi eti watu wa kaskazini siwataki ktk Halmashauri yangu, kwanza ana Hamashauri au ni mtumishi tu? Watu wa kaskazini wameikosea nini nchi hii?

Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaomba msaada wako tunaweza hata kumpoteza huyu mtanzania hali yake ni mbaya sana. Mhalifu Walter (mwanasheria aliyechukua pesa za walimu wanyonge) na maafisa utumishi wilaya ya Tunduru ndio wamemwandalia hati ya mashtaka mtu innocent ambaye hajui hata kinachoendelea ktk mitandao ya kijamii.
 
Mwambie huyo mtumishi aachane na Utumishi wa Umma, achukue kadi ya CHADEMA.

Utumishi wa umma na uanaharakati uchawara haviendi pamoja unless utumie AKILI.
 
Inavyoonekana hawa wakurugenzi wenye viburi Ummy anawalinda, Hata wa jiji la Tanga ni shida tena yuko ktk jimbo la waziri wa TAMISEMI lakini hagusiki, nafikiri hata huyo wa Tunduru naye kuna mkubwa anamlinda na kote ni ukanda wa waswahili sijui km tutapona na Magufuli hatunaye tena nani watamwogopa? Si tulisema wanawake wanaweza? Kosa alilofanya Magu kumteua mgombea mwenza mwanamke akijua hatafia madarakani. Sasa angalia huyu mama wanamdharau kupita kiasi hana anachoweza kufanya. Jamii forums ilinoga kipindi cha JPM maana kila kiongozi alikuwa anaogopa kurushwa siyo ktk awamu hii ya wanawake wanadharauliwa.

Tukiendelea hii nchi hii itavunjika vipande hatuwezi kuvumila ubaguzi km huu kila mtu ana sehemu amezaliwa. Huyo mwalimu kwanini wamsort kati ya walimu wengine wote? kisa katoka kanda ya kaskazini? Ni maagizo kutoka juu kwamba wanyanyaswe? Na polisi nchi hii akili zao wamekabidhi wapi? wanahangaika na mwananchi myonge km huyo wanajisikiaje? hawana ndugu? hawazajaliwa?, hawana watoto? Mtu ana watoto wadogo mnamlaza rumande watoto wake hamjui wamekula wamelala wapi na tena kule porini kuna wanyama.

Tunaambiwa moja mdogo anaumwa nani atamhudumia? Mtoto afe kisa mmekula hela ya Mkurugenzi siyo? Issue hapa Mkurugenzi analinda uovu wa watumishi wake ambao amekuwa akila nao kwa kumwaga damu ya innocent woman. Laana ya mwenyenzi Mungu haitawabakiza salama mlaaniwe. Mmenunua polisi lakini hamuwezi kumnunua Mungu. Mmenunua mamlaka za juu yenu lakuni Mungu hanunuliwi siku zenu si nyingi za kuendelea kufanya huo uovu wenu.
 
Mwambie huyo mtumishi aachane na utumishi wa umma, achukue kadi ya CHADEMA.

Utumishi wa umma na uanaharakati uchawara haviendi pamoja unless utumie AKILI.

Tutamwambia mmeo aache huo uanaharakati usije kushhindwa kupelekwa chooni.
 
Kama ilivyoripotiwa jana mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru amempeleka mwl. wa shule msingi Mrusha polisi ameteswa huko polisi ameshinda njaa na mateso mengine yasiyoelezeka.

Tangia asubuhi alishinda polisi usiku wa saa 4 alipelekwa na gari ya Halamashauri nyumbani kwake kupekuliwa wakarudi naye mjini na kulala rumande hawakumpa taarifa hata mkuu wake pale shuleni. Hawaruhusu mdhamana, yamekuwa km ya Mbowe. Kisa ni taarifa iliyoandikwa hapa JamiiForums juu ya walimu wapya pale Tunduru kunyanyaswa kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Utumishi na Mwanasheria wa Halmashauri aitwaye kwa jina moja Walter.

Huyu bwana kiukweli ndio kawaida yake kuchukua pesa za walimu wapya kiasi cha Shs 82,000/ kila moja kwa vitisho kuwa usipoitoa hutasajiwa ktk mfumo wa ajira. Tulitegemea Mkurugenzi angewachukulia hatua kinyume chake waliochukuliwa pesa wamegeuziwa kipande wakishirikiana na polisi wasio waaminifu pale wilyani Tunduru. Ni walimu wengi waliwatoa pesa kwa njia ya vitisho kuwa wasingesajiliwa, sijui kigezo gani wametumia kumzushia kesi ya uwongo huyu moja.

Mwalimu wetu bado ameshikiliwa polisi hakuna mdhamana hatakiwi mtu kumsogelea wamemchukulia simu yake. Nijui km atatoka akiwa mzima tumwombee. Ana watoto wadogo wawili moja yuko chekechea na anaumwa mwingine yuko darasa la kwanza haijulikani wako ktk hali gani na km wanapata chakula na wamelala wapi ukizingatia moja mdogo ndio mgonjwa. Huu unyama anaoufanya Gasper Zahoro Balyomi(Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru) haujafanywa hata na Adolf Hitler.

Tuna viongozi wanawake lakini inaonekana hawana hata huruma, Rais mama, waziri wa Elimu mama, waziri wa TAMISEMI mama lakini tumeandika hatuoni hatua yoyote.

Wallahi nimemkumba hayati Magufuli haya yasingewezekana. kuna mkuu wa Wilaya, RAS na Mkuu wa Mkoa tena Brigedia Jenerali wa JWTZ Mkurugenzi wa Wilaya ni nyau wa aina gani ktk nchi hii? Halafu anaongea lugha ya kibaguzi eti watu wa kaskazini siwataki ktk Halmashauri yangu, kwanza ana Hamashauri au ni mtumishi tu? Watu wa kaskazini wameikosea nini nchi hii?

Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaomba msaada wako tunaweza hata kumpoteza huyu mtanzania hali yake ni mbaya sana. Mhalifu Walter (mwanasheria aliyechukua pesa za walimu wanyonge) na maafisa utumishi wilaya ya Tunduru ndio wamemwandalia hati ya mashtaka mtu innocent ambaye hajui hata kinachoendelea ktk mitandao ya kijamii.
Imekula kwake.
Huu ndio mwanzo wa mwisho wa mkurugenzi...
 
Back
Top Bottom