Hagwila
Member
- Apr 18, 2019
- 80
- 97
Mheshimiwa DED MAGU salaam,
Napenda kukueleza machache kuhusu Idara yetu ya Elimu msingi kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Magu kama ifuatavyo:
Idara ya Elimu wilayani Magu imeyumba tangu alipohama Yesse Kanyuma, aliyekuwa Afisa Elimu Msingi (W) Magu.
Baada ya Kanyuma kuhamishwa aliletwa Salyankanga kujaza nafasi hiyo. Mzee huyu Salyankanga (sasa amestaafu) alikuwa mla rushwa aliyekithiri; rushwa ya fedha kwa waalimu wa kiume, na rushwa ya ngono na fedha kwa waalimu wa kike.
Huduma zenye maslahi kwa waalimu wa shule za msingi iwe ualimu mkuu, uratibu au huduma yeyote yenye maslahi kwa Mwalimu, mzee huyo alikuwa haitoi bila rushwa, ama ya fedha au ngono. Ilikuwa heri sana Salyankanga kustaafu maana chini ya uongozi wake aliwanyanyasa sana waalimu wa shule za msingi.
Bazazi huyo Salyankanga, alikuwa akifanya mambo yake hayo akishirikiana na watumishi kadhaa idarani hapo ambao ndio walikuwa kama mawakala wake hususani Johari na Prisca katika kuzikanyaga haki na stahili za waalimu.
Ameondoka Salyankanga ameletwa Madam Glory kuchukua nafasi hiyo, akitokea Ilemela ambako alikuwa Afisa Elimu Taaluma (Msingi).
Glory (mwenye digrii moja) amefika idarani amekutana na Johari na Prisca; wamempika ameiva, wamempa mikakati yao ovu, ameikubali na sasa rushwa na ukandamizaji dhidi ya waalimu wa msingi vinaendelea.
Glory hajiamini kwenye nafasi hiyo; anajua hatoshi, anawapiga vita maofisa wengine wenye elimu (masters) kumzidi yeye mwenye digrii moja akidhani watampoka cheo chake. Anatuamia "kufahamiana" kwake na R.E.O. Mwanza (kama na Johari "anavyofahamiana" nae) kuwasambaratisha maofisa idarani hapo, na anafanikiwa maana tayari ameshamhamisha Afisa Vifaa na Takwimu kwenda Misungwi; na anatamba eti bado mmoja!!
DED Magu, tafadhali shughulikia ofisi hiyo ya elimu maana usipofanya hivyo, hatimaye hawa wadada watakuharibia. Yule Afisa aliyehamishiwa Misungwi ni mchapakazi mzuri, na wewe unajua; sasa manpower hiyo imeondolewa kwa sababu ya majungu tu. Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Madiwani; msaidieni DED wetu kupangua watendaji vichomi kama hao wanaotuondolea watumishi mahiri katika wilaya yetu kwa kutumia influence zao na R.E.O. Mwanza.
Naamini hata matokeo ya darasa la VII mwaka huu Magu kushika nafasi ya tatu kimkoa, huyo afisa Vifaa na Takwimu amehusika pakubwa maana alikuwa anatembelea sana mashule na kuhimiza ufundishaji; tarajia mabadiliko Misungwi.
Naomba kuwasilisha, asante.