DED Magu angalia sana Idara ya Elimu Msingi

Hagwila

Member
Apr 18, 2019
80
97
Mheshimiwa DED MAGU salaam,

Napenda kukueleza machache kuhusu Idara yetu ya Elimu msingi kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Magu kama ifuatavyo:

Idara ya Elimu wilayani Magu imeyumba tangu alipohama Yesse Kanyuma, aliyekuwa Afisa Elimu Msingi (W) Magu.

Baada ya Kanyuma kuhamishwa aliletwa Salyankanga kujaza nafasi hiyo. Mzee huyu Salyankanga (sasa amestaafu) alikuwa mla rushwa aliyekithiri; rushwa ya fedha kwa waalimu wa kiume, na rushwa ya ngono na fedha kwa waalimu wa kike.

Huduma zenye maslahi kwa waalimu wa shule za msingi iwe ualimu mkuu, uratibu au huduma yeyote yenye maslahi kwa Mwalimu, mzee huyo alikuwa haitoi bila rushwa, ama ya fedha au ngono. Ilikuwa heri sana Salyankanga kustaafu maana chini ya uongozi wake aliwanyanyasa sana waalimu wa shule za msingi.

Bazazi huyo Salyankanga, alikuwa akifanya mambo yake hayo akishirikiana na watumishi kadhaa idarani hapo ambao ndio walikuwa kama mawakala wake hususani Johari na Prisca katika kuzikanyaga haki na stahili za waalimu.

Ameondoka Salyankanga ameletwa Madam Glory kuchukua nafasi hiyo, akitokea Ilemela ambako alikuwa Afisa Elimu Taaluma (Msingi).

Glory (mwenye digrii moja) amefika idarani amekutana na Johari na Prisca; wamempika ameiva, wamempa mikakati yao ovu, ameikubali na sasa rushwa na ukandamizaji dhidi ya waalimu wa msingi vinaendelea.

Glory hajiamini kwenye nafasi hiyo; anajua hatoshi, anawapiga vita maofisa wengine wenye elimu (masters) kumzidi yeye mwenye digrii moja akidhani watampoka cheo chake. Anatuamia "kufahamiana" kwake na R.E.O. Mwanza (kama na Johari "anavyofahamiana" nae) kuwasambaratisha maofisa idarani hapo, na anafanikiwa maana tayari ameshamhamisha Afisa Vifaa na Takwimu kwenda Misungwi; na anatamba eti bado mmoja!!

DED Magu, tafadhali shughulikia ofisi hiyo ya elimu maana usipofanya hivyo, hatimaye hawa wadada watakuharibia. Yule Afisa aliyehamishiwa Misungwi ni mchapakazi mzuri, na wewe unajua; sasa manpower hiyo imeondolewa kwa sababu ya majungu tu. Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Madiwani; msaidieni DED wetu kupangua watendaji vichomi kama hao wanaotuondolea watumishi mahiri katika wilaya yetu kwa kutumia influence zao na R.E.O. Mwanza.

Naamini hata matokeo ya darasa la VII mwaka huu Magu kushika nafasi ya tatu kimkoa, huyo afisa Vifaa na Takwimu amehusika pakubwa maana alikuwa anatembelea sana mashule na kuhimiza ufundishaji; tarajia mabadiliko Misungwi.

Naomba kuwasilisha, asante.
 
Hapo DED achukue hatua, lakini pia walimu nao wamezidi wanashindwa kuyaanika hayo maovu? Mbona viongozi wapo wengi wa kupelekewa taarifa?
 
Johari huyu nasikia alimpa tenda ya kuchapa mitihani wa MOCK (W) Magu 2019 MEK mmoja anaitwa "Pochi" Jamaa alienda kuchapishia mitihani hiyo Dar kwa pesa ndefu; mitihani hiyo iliahirishwa mara mbili kutokana na kuchelewa kwa maandalizi.
 
Hata Geita DC imewaka moto matokeo ya Std VII 2019 kimkoa imeshika nafasi ya mwisho kutokana na DEO Said kuwavuruga walimu wakuu na kuwapoka madaraka. Rushwa ya ngono na kuwapa cheo walimu wakuu kwa M.1 kwake kawaida.

Mbaya zaidi kwenye kikao cha wenyeviti wa walimu wakuu kilichofanyika Dodoma alimuacha Mwenyekiti aliochaguliwa na walimu wakuu na kumpeleka Rafiki yake Mkuu kutoka katoro.

Kwa hiyo walimu wamekufa moyo wa ufundishaji. Jamaa anajiita yeye ni Afisa usalama. Serikali kazi kwenu.

Takukuru changamkeni.
 
SACO,
Hayajakukuta ndugu yangu; siku utakayonyanyasika kisawasawa utaelewa, japo sikuombei. Fikiria, una vigezo vyote vya kukustahilisha kupata nafasi au huduma fulani; badala ya kupewa hiyo nafasi au huduma, unaambiwa toa laki 3 hadi 5 ndipo upate hiyo nafasi au rushwa ya ngono (kwa wanawake). Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
 
Hapo DED achukue hatua aisee ,lakini pia waalim nao wamezidi umbulula wanashindwa kuyaanika hayo maovu? Mbona viongozi wapo wengi wa kupelekewa taarifa?
Wanaogopa kudukuliwa na kushikishwa adabu!

Kuvuliwa madaraka, uhamisho wa NIKOMOENI, kunyimwa stahili zao n.k; wanaamua kufa kibudu (wala siyo kiofisa).

Mimi naamini kama waalimu wangekuwa jasiri, wakatafuta namna yoyote ya kuwasilisha masaibu yanayosababishwa na ofisi ya DEO kwa DED (ilimradi yawe ya kweli, wangesaidiwa)

Sasa hivi kuna waalimu wakuu wame-surrender posho yao ya ualimu mkuu au wanagawana na baadhi ya maofisa wa idara ya elimu hapo Magu; wanachangishwa pesa zisizotolewa risiti kila mara, utadhani wao ndio wana mafungu ya kuendesha ofisi ya DEO wakati DEO ana OC yake.
 
Nani ataisimamia halmashauri ya wilaya ya Magu na kuwatiisha watumishi? Madiwani wako hoi na mbunge yuko busy na biashara ya kuuza mafuta! Magu ni wilaya kongwe iliyovurugwa na wenyeji, kwahivyo watumishi wanatumia nafasi zao kujipigia watakavyo.
 
Nani ataisimamia halmashauri ya wilaya ya Magu na kuwatiisha watumishi? Madiwani wako hoi na mbunge yuko busy na biashara ya kuuza mafuta! Magu ni wilaya kongwe iliyovurugwa na wenyeji, kwahivyo watumishi wanatumia nafasi zao kujipigia watakavyo.
Pity...!!
 
kaitamarogo,
Veronica Justine na Johannes John a.k.a. JJ walishaona ubovu wa Idara ya Elimu Magu mapema, wamehamia jijini Mwanza. Fundikira bado yupo Mamlaka ya Mji mdogo wa Magu na ni swaiba wa DED. Namwomba Chief Fundikira, amshauri DED to get rid of the duo viz:-
Johari and Prisca ambaye hana hata barua ya uteuzi kutoka TAMISEMI; aende darasani Magu Day au Itumbili akafundishe, japo skills na methodology za ufundishaji yuko shallow sana. Mwaka jana MMU walimkataa kufundisha Diploma pale Teachers Resource Centre Magu. Huyo Johari atafutiwe namna nyingine maana yeye ana barua. Kila kubwa ina kubwa yake; enough is enough.
 
KUMBE UALIMU MKUU UNATOA LAKI TATU MRATIBU MILIONI DUU SERIKALI YA WANYONGE kwa hiyo posho imesababisha kila mtu anatamani kupewa cheo
Kama hao maofisa wanatamani huo u-Mwalimu Mkuu au Uratibu; waombe wahamie madarasani wawanie u-Mwalimu Mkuu au Uratibu. Wasidhani kuwa Mwalimu Mkuu au Mratibu ni kazi nyepesi; hao ndio walioko field na wanafunzi na jamii kwenye mazingira magumu ya kazi. Hao maofisa wanacheza na keyboards za kompyuta, remote za viyoyozi na kuweka vishoka kwenye Land Cruiser Hard Top; ni sawa ndipo mahala pao, wasiwanyanyase waalimu; watende kazi zao kwa haki.
 
Wanaogopa kudukuliwa na kushikishwa adabu!!
Kuvuliwa madaraka, uhamisho wa NIKOMOENI, kunyimwa stahili zao n.k; wanaamua kufa kibudu (wala siyo kiofisa).
Mimi naamini kama waalimu wangekuwa jasiri, wakatafuta namna yoyote ya kuwasilisha masaibu yanayosababishwa na ofisi ya DEO kwa DED (ilimradi yawe ya kweli, wangesaidiwa)
Sasa hivi kuna waalimu wakuu wame-surrender posho yao ya ualimu mkuu au wanagawana na baadhi ya maofisa wa idara ya elimu hapo Magu; wanachangishwa pesa zisizotolewa risiti kila mara, utadhani wao ndio wana mafungu ya kuendesha ofisi ya DEO wakati DEO ana OC yake.
Awamu hii wakuu wanatabu sana kisa 200000!!!!! hafu hawana mshikamano
 
Kama hao maofisa wanatamani huo u-Mwalimu Mkuu au Uratibu; waombe wahamie madarasani wawanie u-Mwalimu Mkuu au Uratibu. Wasidhani kuwa Mwalimu Mkuu au Mratibu ni kazi nyepesi; hao ndio walioko field na wanafunzi na jamii kwenye mazingira magumu ya kazi. Hao maofisa wanacheza na keyboards za kompyuta, remote za viyoyozi na kuweka vishoka kwenye Land Cruiser Hard Top; ni sawa ndipo mahala pao, wasiwanyanyase waalimu; watende kazi zao kwa haki.
Mwalimu acha kulia lia. Yaani mtoto mdogo kama Johari na Glory ndio wana kuumiza kichwa. Kuna mwamba wangu mmoja kapiga chini hizo mambo za ukuu mpaka ameanza kunenepa. Tatizo mnajipendekeza sana na mnatoa hongo ya madaraka kwa hiari zenu wenyewe.
 
Mwalimu acha kulia lia. Yaani mtoto mdogo kama Johari na Glory ndio wana kuumiza kichwa. Kuna mwamba wangu mmoja kapiga chini hizo mambo za ukuu mpaka ameanza kunenepa. Tatizo mnajipendekeza sana na mnatoa hongo ya madaraka kwa hiari zenu wenyewe.
Mimi siyo Mwalimu, lakini haya yanayolalamikiwa hata mimi nayajua haya kwa sababu yako sehemu nyingi; tuko kwenye jamii pamoja na waalimu; so tunayajua mambo yao kama wewe ulivyoyajua ya huyo mwamba wako. Kufanya kazi ni haki ya mtu anayestahili kufanya hiyo kazi ilimradi ana vigezo.

Senior worker hana haki ya kumnyanyasa junior worker simply kwa sababu ana mamlaka kuliko yeye. It's not a matter of personalities kwamba ni Glory au Johari; issue is the positions they are holding versus what they are doing whilst exercising the powers; hawatendi haki. Hata ungekuwa wewe ukitenda visivyo utalalamikiwa tu!
 
BrAsMaRiLiSaShElMa,
Wapo waalimu wenye misimamo thabiti, lakini wanakwamishwa na wenzao wachache wanaovutwa masikio na hao maofisa hapo idara ya elimu kwa sababu zao binafsi kama kupewa favour mbalimbali kama kupewa wasimamizi wanaowataka kwenye mitihani ya darasa la saba ili wawasaidie watahiniwa kwenye shule zao.

Johari amekuwa akilifanya sana jambo hili la kupeleka wasimamizi maalum kwenye shule ambazo waalimu wake wakuu ana uswaiba nao. Kwa mfano, mwaka jana 2018 alipeleka wasimamizi aliowataka Mwalimu Mkuu wa S/Msingi Nyanguge. Wasimamizi hao ni waalimu ambao Mwalimu huyo amewahi kufanya nao kazi Magu S/Msingi akiwa Mwalimu Mkuu (wahusika mnaweza kufuatilia)

Mwalimu huyo alipewa ofa hiyo na Johari kwa sababu yeye alikuwa akimsaidia Johari kufanya kazi za IT ofisini, maana yeye Johari kwenye IT ni kilaza. Kukosa uwezo wa kumudu IT kwa Johari, kunamfanya ashindwe kusimamia kazi za kitengo cha taaluma; na amekuwa akichukua waalimu tofauti wenye uwezo wa IT ili wamfanyie kazi zake.

Hii inasababisha usumbufu mwingi kwa waalimu wakuu kwa sababu, wamekuwa wakipokea maagizo yasiyo kamili ambayo yanasababisha kururiarudia kazi, jambo ambalo linawaongezea gharama na kuwapotezea muda wa kukaa vituoni.

Kwenye kikao kimoja kilichofanyika Magu Day Sekondari kati ya DED na waalimu wakuu, DED alimkemea Mwalimu Mkuu wa Nyanguge S/Msingi kwa kushindwa kumudu kazi zake; lakini Johari alisimama na kumtetea kwa sababu yeye Johari alihusika kumteua Mwalimu huyo kwa rushwa kwenye nafasi hiyo.

Mwaka huu 2019, Johari amepeleka tena wasimamizi maalumu kwenye shule mbalimbali ili wakatoe usaidizi kwa watahiniwa wa darasa la saba; shule kama Nyambitilwa na shule zingine ambazo waalimu wakuu wake waliweza ku-compromise na Johari na kampani yake. Ofisi ya Ukaguzi inalijua hilo lakini wameshindwa kuingilia kwa sababu ofisi ya DEO imewatenga wakaguzi.

Sasa hivi nafasi za Mwalimu Mkuu zilizo wazi kama Bundilya na zinginezo, pamoja na uratibu elimu kata kwa nafasi zilizo wazi kama Isandula, waalimu wanapishana kupeleka mafungu ya pesa kwa DEO na mawakala wake Johari na Prisca.

DED na vyombo husika, mbunge na madiwani tafadhali kuweni macho ili nafasi hizo wasije wakapewa wasio na uwezo lakini wakabebwa na pesa zao.
 
namba force,
Ni kweli; acha na mimi nizungumze machache ninayoyajua kuhusu hiyo ofisi ya DEO Magu ambayo imekumbwa na kashfa nyingi tangu enzi za Saryankanga. Huyu DEO wa sasa ni mpiga hela tu; amekutana na mchagga mwezake Johari rushwa mtindo mmoja.

Naanza na mfano mmoja ambao hata DED Lutengano ataukumbuka. Hivi karibuni tu kuna Mratibu (mama mjane) alihamishiwa kata ya Itumbili kwa uhamisho wa malipo. Mama huyo baada ya kulipwa, DEO Glory na timu yake walimtoza yule mratibu pesa kama shukrani kwao!! Mama yule alikwenda kulalamika kwa DED Lutengano; sijui hatua zilizochukuliwa na DED kama zipo.

Wewe mwenyewe DED, siku za karibuni uliitisha kikao cha Finance ambapo wakuu wa idara walikuwepo. Uliwapongeza wajumbe kwa matokeo mazuri ya mitihani ya darasa la VII; na Katibu wa TSD alichangia kwa kuitaka ofisi ya elimu kuwa na ushirikiano miongoni mwao, badala ya kupigana majungu na kuchongeana hadi kufikia kuhamishwa baadhi ya watendaji chapa kazi kama SLO aliyehamishwa alivyopigwa jungu.

Baada ya kikao DEO Glory alimfuata Katibu huyo wa TSD na kuanza kumshambulia kwa maneno; mpaka sasa mahusiano ya watu hao wawili siyo mazuri; lakini pia mahusiano kati ya DEO na Mkaguzi Mkuu siyo mazuri vilevile kwa sababu ya ofisi ya DEO kupanga wasimamizi kwa mapatano na baadhi ya waalimu wakuu ili watahiniwa wa darasa la VII katika shule zao wasaidiwe. Kwa mahusiano haya hafifu kazi zitafanyikaje kwa ufanisi?

Palifanyika semina au kongamano la Juma la Elimu ya Watu Wazima kimkoa hivi karibuni kule Buchosa. Maofisa wanne wafuatao:- SLO aliyehamishwa, Afisa Elimu ya Watu Wazima, DEO Glory na Johari walilipwa posho kwa ajili ya kuhudhuria na kushiriki kongamano hilo la Juma la Elimu ya Watu Wazima.

Waliokwenda Buchosa ni wawilo tu; SLO aliyehamishwa na Afisa Elimu ya Watu Wazima. DEO Glory na Johari hawakwenda Buchosa licha ya kulipwa posho, wala hawakuwa ofisini Magu siku zote za kongamano hilo. Huyo ni ubadhirifu wa mali ya umma.

Uhamisho wa SLO kwenda Misungwi pia ni ubadhirifu kwa sababu umetolewa kwa majungu. Afisa huyo amekaa Magu kwa muda wa chini ya mwaka mmoja toka alipohamia Magu akitokea Ukerewe na alilipwa.

Kwa uhamisho huu amelipwa tena kumhamishia Misungwi kwa sababu tu Glory na Johari wamekwenda kulalamika kwa Afisa Elimu Mkoa Mwanza eti SLO huyo anawanyima raha!! R.E.O. Mwanza nae kwa sababu hao wawili wote ni wapenzi wake (kama hawajui wajijue sasa), akaamua kufanya alivyofanya TAMISEMI hatimae SLO amehamishwa!!

Mhe. Jaffo, Mhe. Ndalichako, Mhe. Mkuchika afande wangu, tafadhali fuatilieni mambo haya; kuna watu bado hawajamwelewa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli kwamba dhamira yake kwa dhati ya moyo wake amekusudia kuipeleka mbele nchi yetu.

Baadhi ya watendaji wanafanya yao tu bila kuzingatia Vision, Mission wala Spirit ya Rais wetu. Nitakwenda Magu kumweleza Rais uozo huu siku akija kuzindua mradi wa maji; tutaonana wabaya.
 
Back
Top Bottom