DOKEZO Magu S/Msingi: Biashara kazini saa za kazi kwa walimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kaji Bagome

Member
Nov 5, 2019
15
21
JMT; Kazi iendelee.

Nilishaandika mara kadhaa kuhusu udhaifu wa uongozi wa Shule ya Msingi Magu; nikiomba uongozi wa Elimu Msingi (W) urekebishe hali hiyo, lakini kila uchao inakuwa kama heri ya jana.

Sasa hivi baadhi ya waalimu wanafanya biashara shuleni hapo (wao wenyewe), tena wakati wa kazi; wakirusha biashara zao kwenye mitandao ya kijamii.

Ujasiriamali sawa Ni kuongeza kipato; lakini kuufanyia eneo la kazi wakati wa kazi siyo sawa. Hayo yanafanyika Mwl. Mkuu akiwepo ofisini kwake bila kukemea mwenendo huo ili ukomeshwe.

Shule imechakaa kimazingira, kitaaluma, kiuongozi, kimahusiano, uchafu umekithiri vyooni, maji hakuna wakati bomba lipo n.k.

Yote hayo yanaendelea, licha ya kuyaweka bayana kwa Afisa Elimu Msingi (W) Magu kwenye jukwaa hilihili mnamo tarehe 17/11/2022 na hata kabla ya hapo.

Huenda Afisa Elimu Msingi (W) anakwamishwa na baadhi ya maofisa wake hapo ofisini kumchukulia hatua Mwl. Mkuu Njalla, maana ofisi yake ina maofisa wakongwe kuliko yeye na ni wala rushwa wakubwa; ambao huwa wanachukua pesa kwa waalimu na kuwapigania ili wapate ualimu mkuu.

Afisa wa aina hiyo ofisini hapo ni Bw. Nyagabona; ambaye ni Afisa Taaluma asiye hata na barua ya uteuzi kutoka TAMISEMI, lakini anayumbisha sana ofisi hiyo.

Huenda Mwl. Mkuu Ezekiel Njalla, alitoa chochote kwa Bwn. Nyagabona; hivyo DEO Msingi Magu kila anapotaka kuchukua hatua anakwamishwa.

Najua DED Magu mambo ni mengi, Idara zote yeye ndiye overseer, mambo mengine haelewi hata yanakwendaje kwenye vituo.

I wish Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Mr. Msonde angepita ghafla hapo shuleni Magu akajionea hali halisi, yeye angesema na mambo yangerekebishwa.

Wahusika tafadhalini chukueni hatua kurekebisha kasoro nyingi zilizoko kituoni hapo kama hizi:

Screenshot_20230126-180543.png
 
Huu ni wivu au uzalendo?
Anyway mkuu, wacha kiherehere, maisha ya walim n magum, waache watafte rizki.
Hata wewe ungekua unapata vijisenti kdg usingekua na makelele kias hiki.
Sipingi mtu kufanya ujasiriamali, hata kwenye maelezo yangu nimesema.
Hoja yangu ni kuwa, siyo sahihi mwalimu mwenyewe kusimama eneo la shule wakati wa kazi akauzia watoto vitu kama barafu. Angeweza kumpa mtu mwingine akauza badala yake.
Watumishi wengi tu wanafanya biashara zao kwenye maeneo yao ya kazi, lakini inategemea mazingira ya kazi na ofisi zao.
Mabango kama hayo ya kusemwa ni kiherehere, wivu, ukuda, roho mbaya n.k najua yatarushwa kwangu, lakini hoja yangu itafika kwa wahusika.
 
Mratibu Elimu Kata Yupo Anangoja Ya Kyerwa Yaje
Huyo Ndiyo Wale Waliokuwa Wanakenua Meno
 
Wapeni walimu posho ongezeni na mishahara muone kama watafanya hizo biashara. Sio mnawapiga majungu huku hamna msaada nao wowote
 
Sasa hizo barafu za mia mia ndio zinakunyima usingizi? Hao walimu vipindi vyao si wanafundisha?Watu wanauza twiga huko muda wa KAZI!!! Anyway Watu Kanda hiyo mna roho zenu flani hivi personal.
Jamaa ana roho nyeusi Sana. Vitu vidogo kama hivyo anakuja humu kuandika Uzi ulioambatana na picha kabisa daaah!??.
 
Jamaa ana roho nyeusi Sana. Vitu vidogo kama hivyo anakuja humu kuandika Uzi ulioambatana na picha kabisa daaah!??.
Yaani jiwe ameacha mabaki mabaki sijui yataisha lini. Yaani walimu wasiihi maisha ya mazingira Yao??

Mtoto anapenda kachori mwalimu aspike?? Simsemi vby lkn watu waliosemaga mwl asiehike Hela nawashangaa kila uchwao

Kuna mpuuzi mmj alikuwa Tamisemi na ameondolewa aliniharibia maisha. Kina watu wanakosa busara na kuharibu maisha ya wengine. Lkn ujue kila utendalo Lina majibu
 
Yaani jiwe ameacha mabaki mabaki sijui yaraisha lini. Yaani walimu wasiihi maisha ya mazingira Yao??

Mtoto anapenda kachori mwalimu aspike?? Simsemi vby lkn watu waliosemaga mwl asiehike Hela nawashangaa kila uchwao
Hii ni kawaida Sana tangu zamani mwalimu anakuja shuleni amebeba deli la Bagia au maandazi ambapo eidha anauza yeye au anamkabidhi mwanafunzi mmoja anayemuamini amuuzie.
Sasa ajabu ni nini hapo kwa mleta mada!!!? Apambane na maisha yake wakati Walimu wakipambana na maisha Yao pia.
 
Wivu tu unakusumbua tu... Kama hawafanyu majukumu yao ya kufundisha inapaswa kulalamika..

Afu maswala ya ukarabati wa shule, isime serikali ila sio mwalimu mkuu
 
Mleta mada huenda una hoia ila kuna mambo hayako wazi hapa.
..JHawa waalimu wanauza wakati gani?
...Watoto huwa wako nje muda wote?
...Je, kamati ya shule/wazazi na uongozi wa sehemu husika wanalifahamu hili na wamechukua hatua gani?
...wewe umechukua hatua gani za awali kama mzazi kuonana na uongozi wa shule kushughulikia tatizo hili?

Hebu jibu hayo ili isionekane kama ni majungu umeleta hapa.
 
Hiyo picha uliyoweka hapo inaweza mgharimu huyo mwalimu ukizingatia watu siku hizi wanafanya kazi na mitandao kubust status zao kwa mama...
Aisee iondoe
 
Back
Top Bottom