Decoder ni Kisimbuzi na sio King'amuzi

Decoder ni Kisimbuzi na sio King'amuzi

Baba Mtu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2008
Posts
870
Reaction score
170
Leo BAKITA wameujulisha umma tafsiri sahihi ya maneno kama ifuatavyo:

Decoder............. Kisimbuzi (kusimbua -decode)

Detector........... King'amuzi (kung'amua - detect)


Kwa mujibu wa mjadala ulioendeshwa kupitia radio 1 katika kipindi cha ulimwengu wa kiswahili, kinachurushwa kuanzia saa 1:30 asubuhi (MUHIMU: kipindi kilirushwa siku ya jumamosi ya tarehe 5/1/2013); DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.
Decode ni muunganiko wa maneno mawili, CODE na DE, na neno DE limetumika kama kikanushi/kinyume. Mfano: KWELI na SI KWELI. CODE linatafsirika kama SIMBA (sio simba mnyama) kwa lugha ya kiswahili. Na DECODE linatafsirika kama SIMBUA wa lugha ya kiswahili. SIMBA (sio simba mnyama) kinyume chake ni SIMBUA. Na kifaa kinachotumika kusimbua kinaitwa KISIMBUZI, yaani DECODER kwa kingereza.
Lakini neno DETECTOR tafsiri yake ni KING'AMUZI. Na ving'amuzi viko vya aina nyingi, mfano:
Metal, X-rays, Uranium, Gas, Moisture, Blood sugar na Bomb DETECTORS; yaani ving'amuzi vya kung'amua metali, miale ya X, madini ya Uranium, Gesi, Unyevu, sukari ya damu na mabomu.
Kumbuka DECODER = KISIMBUZI na DETECTOR = KING'AMUZI.


Chanzo:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kisimbuzi-na-sioi-kingamuzi.html#post5396891
 
simba=code
kusimbuka=coding
haya wapiga simba ni wakati wa kusimbuka ki Java!
sweet kiswahili!
 
Haya sasa, wote mlionunua ving'amuzi nendeni mkavitupe dampo, muanze kununua visimbuzi
 
hawa jamaa kwa ku-force matumizi ya mijina yao wanayo tunga!
af Mijina yenyewe mibayaaa
 
Back
Top Bottom