DECI ni zaidi ya MAFISADI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DECI ni zaidi ya MAFISADI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lizzy, Jun 7, 2009.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dada yangu amepoteza zaidi ya laki nane kupitia DECI ila haijaniuma kufikia ya huyu bibi maskini......_mamadeci.jpg (image)Eti kauza ndizi zake jamani visenti akawapa hawa mafisadi sasa ona kabaki kapa.Inasikitisha sana kuona mtu kama huyu kajitahidi kujipatia riziki then mwisho wa siku ana baki kama vile hakuhangaika.[​IMG]
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  nadhani DECI ni vyema iangaliwe kwa mapana zaidi. asilimia 15 ya pesa zilizokusanywa ziripotiwa kupelekwa TRA kama kodi. Je, ni kwanini wanachama wa DECI hawazungumzii kuwa serikali ina pesa zao ambazo ''si halali'' kutokana na taarifa za BoT? Serikali ndio pekee wnye uwezo wa kuhakikisha viongozi wa DECI wanarudisha chochote kilichopo, sasa ni vyema wanachama wa DECI wakaibana zaidi serikali, ambayo ina asilimia 15 ya pesa zao.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jun 7, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Pole sana LilSun, ila ni kuwa hawakuwa wanalazimisha!
  Pili ni wajibu wetu sote katika jamii kulindana na kutokuwa bize katika mambo yetu binafsi, DECI iko siku nyingi sana kila aina ya watu walishiriki na inapotokea kamba inakatikia pembamba kawaida kuna maumivu

  Wakati unalia DECI mbaya kuna watu wamevuna mamilioni sijui kama watakuelewa sentensi yako--swala zima ni kama gambling

  kuna watu wamejenga nyumba , wakati kuna huyo analia, huoni kama kuna haja ya kulitazama hili swala in 3D kuliko kulalia upande mmoja??

  personally si-support DECI lakini inatakiwa kuwe na haja ya kuangalia ni nini kifanyike kuwaokoa hawa walioumizwa, DECI zipo kila siku kiaina ila hatupigi kelele!

  ushauri wangu ni wawe wanaunda vyama vitakavyokubalika kisheria, viwe imara na endelevu hata vizazi vya hao members ili LOOP inapokatika asilie mtu

  kwa kifupi DECI ni LOOP isiyoisha! wanaofaidika ni wale wa mwanzoni!
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  sasa kwa nini walipokuwa wanavuna hawakulalamika?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Najua kuwa kuna walio faidika nayo tena sana 2.....na hata waliopoteza wengine wana uwezo wakutafuta na kupata tena!Illa kuna mtu ukimwona inabidi roho ikuume ndugu!
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Jun 7, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280

  Sure wanaongia mkenge kama huo, serikali inabidi iwalinde na kuzuia mambo haya mapema sana usikute kuna Polisi walikuwa wanaweka pesa DECI!!!!
   
Loading...