Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 235
- 411
Leo December 1 2024 ni siku ya UKIMWI duniani.
Mpaka sasa kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) kuna zaidi ya watu milioni 39.9 duniani kote wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU).
Ni muhimu kuelewa kwamba si kila mwenye VVU ana UKIMWI. UKIMWI hutokea katika hatua za mwisho za maambukizi ya VVU ambapo virusi hao wamezaliana kwa wingi hivyo kinga ya mwili kuelemewa.
Hakuna tiba ya UKIMWI lakini tunaweza kupunguza maambukizi ya VVU kama ifuatavyo:
-kuepuka ngono zembe, kutumia kondomu
-kuepuka kushirikiana vitu vya ncha kali kama nyembe na sindano
-kupima VVU na maambukizi mengine nk
Kwa kulinda haki ya kila mmoja wetu wa kuwa na afya njema pamoja na kupunguza maambukizi mapya ya VVU tunaweza kuwa na jamii isiyokuwa na UKIMWI.
Tuungane pamoja kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua katika kupambana na VVU.