Kuna wakati huwa najiuliza ni kitu gani kimepungua kwenye bongo zenu? Mnakwama wapi? Thamani yeny mbona hamuipi thamani? Hivi ni kweli utandawazi ni chanzo cha haya yote mnayofanya? Kwanini mapenzi yanawafanya mziwekee password akili zenu alafu mzisahau hadi mnashindwa kutambua kwamba mahali mlipo si sahihi? Ni ubaya gani wanaume wenu wawafanyie ili mjue hawana nia njema na nyie?
Haiwezekani mwanaume amekutongoza na amekwambia ana mke wake au mchumba wake ila bado unakubali kuanzisha nae mahusiano huo ni uzembe na ushetani wenye level ya PHD. Au hata kama hajakwambia kwamba anamtu ila anakuonesha kila aina ya dalili kwamba yupo kwenye mahusiano na mtu mwengine ila bado tu umemganda kama ruba huku ukijipa moyo atabadirika au atatulia, huo ni UTAHIRA. Jiongeze.
Ifikie kipindi msiziweke shida zenu mbele kiasi kwamba mkashindwa kutambua thamani zenu. Wanaume huwa na kawaida ya kuwachukulia kama mnajichukilia, ukijichukulia wewe ni cheap ndivyo hivyo hivyo mwanaume atakavyokuchukulia. Shida zako za kifedha na kihisia zisikufanye uwe choo kwamba kila mwanaume atakapobanwa mkojo anakuja kukukojolea.
Wewe sio dampo kwamba kila takataka ya mwanaume unaipokea, wewe sio wa level hiyo. Uzembe wenu wa kufikiria na umbumbumbu wenu kwenye mapenzi ndio unawafanya muwe vyombo vya burudani kwa wanaume. Inafikia hatua mwanaume anakutumia hadi anashindwa akutumie kwa njia gani nyengine, anaishia kukurikodi ukiwa uchi. Kwakuwa akili yako ina password na password hizo umeisahau, akilo haifunguki na kila kitu unaona sawa.
Unajiachiiia, unajitanuuua, unajisambaaaza huku ukichukuliwa video ukiliwa uroda. Inauma sana. Kama ukitambua mapema mtu ulienaye si sahihi bila shaka hutokubali kuendelea kutumika kiasi hiki.
View attachment 1232641