Dear future wife...

Dear future wife...

Mkuu future wife?😀😀😀😀😀 Unapoamua kuvaa uhusika wa kiume kwenye movie, jitahidi kufuata script ya kiume.....sasa wewe unatoka nje ya script.....hii ndio mara ya kwanza kuwa na aidiii mchepuko?🙁🙁🙁🙁🙁🙁 Sarcasm.
Hujaeleweka unahisi mimi ni demu?
 
Dear FUTURE SON,
......................................
........................................
......................................

your lovely Dad!
 
Tamu kusikia mtu akisema mwanzo ,msg kama hii inakufanya unaingia Mazima,mziki wake utauwona pale utakapo maliza kusema I do, utasikia unadhani kila siku bado tuna tongozana sasa ujue wewe ni mke usitegemee yale mapenzi yazamani,unabaki uso mduuuuchuu..
 
Natamani kukuonesha zaidi ni kiasi gani maisha yako yatakuwa yenye furaha kuanzia siku ambayo nitafunga pingu za maisha nawe. Nimepanga uione kila dakika katika maisha yako ya ndoa, kuwa ni nyakati nzuri za kukumbukwa. Nitakusifia kwa uzuri na tabia, siku zote kwa sababu umekuwa wa thamani sasa mpaka siku hiyo ambayo utakuwa ukimiliki sehemu kubwa ya maisha yangu.

Sijambo rahisi kusema nimekubali kukukabidhi maisha yangu, na kuwa nitatumia miaka yangu iliyobaki kuwa na wewe peke yako. Naahidi kukukabidhi funguo za moyo wangu wa upendo nilioufunga; ukiamua unaweza kuzimeza au kuzitupa ili nisiweza kufungua kwa mwingine.

Sitaki hata kufikiria maumivu yatakayoletwa na siku hiyo ambayo tutagombana. Nahisi moyo wangu utasimama na kuacha kufanya kazi yake kwa muda kama injini iliyokataa kuwaka. Lakini katika kila nyakati mbaya zitazopita, naahidi kusimama imara kukuonesha ni kiasi gani nimeamua kuwa na wewe mpaka siku nitakayotangulia.

Nakupenda kiasi ambacho umeweza kuwa shahidi wa penzi langu kwako, naahidi sintakuumiza.
So lovely words
 
Naandika kwa hisia pia Maisha ya ndoa na malengo yake ni kama Maisha tu ya kuzaliwa mpaka kufa,,Hakuna mtu akiwa mdogo ukimwambia hiki hutatimiza anaweza kukubali coz they know bado kuna muda but when its comes to reality huanza punguza expectations zao za utoto kama alipanga awe Dr anajikuta kashindwa na Ndoa ni hivyo ,Unapanga nitaowa bint mrefu mzuri na sifa kibao but Unajikuta Umeowa tofauti hata kama sura na urefu ndio yeye he? Tabia Unajikuta hiyo ahadi yakusema nitakupenda milele na kukulinda zinasahalika Maisha ya ndoa ni Fumbo jingine ngumu mungu kaliweka Japo wachache Wanaishi Ndoto zao ,Ila Wengi ni Ke na sio Me
 
Back
Top Bottom