DC Wanging'ombe atoa wiki moja kusaka watoto 231 ambao hawakuripoti kidato cha kwanza

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
DC.jpg

Ni heka heka kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe baada ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Ally Kasinge kutoa wiki moja uwe umewapata watoto 231 ambao hawajaripoti kidato cha kwanza mwaka huu na hawajulikani walipo.

Mwaka mpya wa masomo ulianza mwanzoni mwa Januari, lakini idadi hiyo ya wanafunzi waliopasi mtihani wa darasa la saba kitaifa mwaka jana mpaka sasa haijaripoti shuleni licha ya kuchaguliwa.

Kasinge alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza na ambao bado hawajaanza masomo katika kikao cha kamati ya maendeleo ya wilaya hiyo, DCC juzi.

Alisema watoto hao wote wajulikane walipo ndani ya wiki moja kupitia maofisa elimu ngazi zote katika halmashauri hiyo.Aidha aliwataka makatibu tarafa kushirikiana na maofisa hao, ili watoto hao 231 wajulikane waliko na kuanza masomo kwa ambao hawajajiunga na shule za sekondari za binafsi.

“Nawaagiza ndani ya wiki moja kila kata ijue watoto waliopo katika kata hiyo walipo na kwanini hawajaanza masomo," aliagiza Kasinge "na wapelekwe shule kuanza masomo.

"Mtendaji wa kijiji, kata na mzazi mtatakiwa kuja ofisini kwangu baada ya muda niliotoa kuleta maelezo.”

Alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure mpaka kidato cha nne, lakini kuna wazazi hawajapeleka watoto wao shule mpaka Machi.

Nipashe
 
Back
Top Bottom