DC wa Kigoma Estha Mahawe ameongea mambo ya Msingi sana

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,951
Hoja zenye nguvu kwa taifa (Mkuu wa wilaya ya kigoma).

Pia ameshauri kufanyika kwa mabadiliko ya sheria kwa watumishi wa serikali kwa kupewa mikataba ya muda ya ajira ili waache kufanya kazi kwa mazoea.

Mahawe aliyasema hayo juzi wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwataka viongozi kujibu kero zilizowasilishwa na wananchi.

Mahawe alisema awali alikuwa anafanya kazi sekta binafsi kabla ya kuteuliwa na kuweka bayana kwamba kama kweli wanataka kuijenga Tanzania ya watu waadilifu na wachapa kazi, ifike wakati kubadilishwe sheria za ajira.

“Zisiwe hizi za ‘permanent and pensionable’ (ajira za mkataba wa kudumu). Sheria hii inawaumiza wateuliwa wa Rais hasa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi. Watu ambao hawatekelezi majukumu yao katika Halmashauri ni wakuu wa idara,” alisema.

Kwa mujibu wa Mahawe, watu hao hawatekelezi majukumu yao kwa sababu wanajua mkurugenzi atatumbuliwa na mkuu wa idara ya elimu, afya na mhandisi wa majengo wao watabaki.

“Ninaomba ifike mahali Mkurugenzi anavyotumbuliwa aondolewe na wakuu wa idara wote kwa sababu tunawaumiza watu wasio na hatia. Mkurugenzi ni mtu mmoja, chini yake ana wakuu wa idara 14. Wakiamua kumkwamisha, gurudumu haliendi. Watu hawa wanafanya kazi kwa mazoea kwa sababu wanajua hawawezi kuondolewa. Tufanye tu kama sekta binafsi mtu anaajiriwa kwa mkataba maalum,” alisema.

“Utakuta mtumishi ameajiriwa akiwa na miaka 25, anasubiria kufa au kustaafu. Watu wa namna hiyo wamekuwa wakwamishaji wakubwa wa maendeleo,” aliongeza.

“Hapa kwetu kwa mfano, tumepata changamoto ya wizi wa dawa kwenye halmashauri yangu. Zahanati 10 zimeibiwa dawa ambazo zinafanana na zinauzwa mtaa wa pili watu wapo na wanaendelea kula mshahara.

“Makamu Mwenyekiti bunge lipo na mimi nilishapita bungeni. Bunge lipo kwa ajili ya kubadilisha sheria. Tusiendelee kuishi kwa mazoea. Kama kweli tumepanga kumsaidia Rais, tubadilishe sheria badala ya watu kusubiri kustaafu , basi wafanye kwa mikataba,’ alisema.

MADUDU BANDARI

Mkuu huyo wa wilaya alisema kero zilizoko bandarini ni nyingi kutokana na kuwapo kwa tozo nyingi na kusababisha kukosekana kwa mapato.

“Nikiangalia fedha inayopotea hapa na Rais anaenda nje kutafuta fedha, ninaumia sana. Ushauri wangu hizi taasisi kubwa mfano TRC (Shirika la Reli Tanzania), TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) ifike mahali wawekwe watu ambao wana uzoefu wa biashara.

“Serikali inapata hasara na mtu hajali ilimradi anakula ana gari lina kiyoyozi maisha yake yanaendelea na watoto wanasoma Ulaya. Kwa namna hii hatutatoboa,” alisema.

Alisema kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo na anapoteuliwa hajawekwa hapo kama sofa. Kazi yake ni kuishauri serikali jambo gani la kufanya na kama kuna kikwazo anaeleza ili mambo yaende.

Alisema jambo jingine linalokera ni wakala wa serikali wanaohusika kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.

“Huwezi kuamini maji ya kunywa au juisi yenye ithibati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama vinavuka kwenda Congo ni lazima watu wa mionzi wachukue kwenda kupima kabla ya kuruhusiwa.

WATUMISHI ARDHI WACHONGEWA

Pia alisema ana mwaka mmoja na miezi miwili tangu alipofika Kigoma na katika majukumu yake mengi anayoyafanya ni kusuluhisha kesi za ardhi.

“Mafaili mengi ni ya malalamiko ya ardhi katika kujifunza kwangu. Nilichogundua changamoto nyingi zilisababishwa na watumishi wa ardhi ambao hawakuwa waaminifu.

“Serikali imeshapata hasara kubwa kupitia watu wa namna hii. Nilishawahi kwenda kusuluhisha mgogoro ambao halmashauri ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh milioni 287 na Sh. milioni 100 imeshalipwa tukawa tunadaiwa Sh milioni 187,”alisema.

Mahawe alisema alipofuatilia na kwenda kufanya vikao na wazee wa eneo husika, ilionekana ni kesi ya kutengenezwa na waliokuwa watumishi wa ardhi walijificha kupitia kivuli cha wananchi ambao hawamiliki ardhi hiyo.

“Utapeli upo kupita kiasi, hao watu wanatengeneza na kujifanya wanafanya kazi ofisi ya Rais au TAMISEMI wanakupigia simu za vitisho. Hao ni watu waliotengenezwa na watumishi waliopita katika hii Halmashauri,” alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Hayo maoni ni wengi walisha yaongea tena mazuri zaidi ya haya, ila mwisho wa siku yakaishia kwenye server za jamii forum na hata waliojaribu kuyatekeleza walisha pata matatizo makubwa hii ndo Tanzania na Africa kwa ujumla hatujui tunataka nini.
 
Chanzo kikuu cha kudorora utumishi ni wanasiasa kama yeye sio watumishi wa umma. Yeye mara ngapi anaingilia utendaji wa Halmashauri na kutoa maagizo? Katika utendaji wa kazi kwanza kuna strategic plan ambayo ndiyo inatoa mwelekeo kwa miaka mitatu had mitano wapi taasisi iende;

pili kuna bajeti inapangwa kila mwaka kutekeleza kazi zilizokuballika kufanywa, je pesa zonatolewa kwa wakati? Watendaji wanaachwa wafanye kulingana na utaalamu wao au wanaingiliwa na MaDC na MaRC halafu mwisho wa siku kazi ikiharibika wanang'aka wakati wao ndio chanzo? Mfano ni manunuzi na tenda je wanaruhusu sheria ya nanunuzi ifuatwe au kutokana na uharaka wanashinikiza ivunjwe?

Ajira ya mkataba sio suluhisho kwa sababu ajira ya kudumu haizuii mfanyakazi kuondolewa kazini pake anapoharibu kazi na kukiwa na ushahidi wa kumtia hatiani. Pia huyo atakayekuwa anaanua kuwa mfanyakazi asiongezewe mkataba atakuwa na integrity kiasi gani ili asimuonee mfanyakazi kutokana na chuki zao binafsi? Mfano wakati wa uchaguzi ukifika maDED wanaachwa waendeshe uchaguzi kwa mujibu wa sheria au wanashinikizwa na hao hao MaDC wantangaze aliyeshindwa kuwa ndiye mshindi halafu baadae umlaumu DED au wa chini?
 
Hoja zenye nguvu kwa taifa (Mkuu wa wilaya ya kigoma).

Pia ameshauri kufanyika kwa mabadiliko ya sheria kwa watumishi wa serikali kwa kupewa mikataba ya muda ya ajira ili waache kufanya kazi kwa mazoea.

Mahawe aliyasema hayo juzi wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwataka viongozi kujibu kero zilizowasilishwa na wananchi.

Mahawe alisema awali alikuwa anafanya kazi sekta binafsi kabla ya kuteuliwa na kuweka bayana kwamba kama kweli wanataka kuijenga Tanzania ya watu waadilifu na wachapa kazi, ifike wakati kubadilishwe sheria za ajira.

“Zisiwe hizi za ‘permanent and pensionable’ (ajira za mkataba wa kudumu). Sheria hii inawaumiza wateuliwa wa Rais hasa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi. Watu ambao hawatekelezi majukumu yao katika Halmashauri ni wakuu wa idara,” alisema.

Kwa mujibu wa Mahawe, watu hao hawatekelezi majukumu yao kwa sababu wanajua mkurugenzi atatumbuliwa na mkuu wa idara ya elimu, afya na mhandisi wa majengo wao watabaki.

“Ninaomba ifike mahali Mkurugenzi anavyotumbuliwa aondolewe na wakuu wa idara wote kwa sababu tunawaumiza watu wasio na hatia. Mkurugenzi ni mtu mmoja, chini yake ana wakuu wa idara 14. Wakiamua kumkwamisha, gurudumu haliendi. Watu hawa wanafanya kazi kwa mazoea kwa sababu wanajua hawawezi kuondolewa. Tufanye tu kama sekta binafsi mtu anaajiriwa kwa mkataba maalum,” alisema.

“Utakuta mtumishi ameajiriwa akiwa na miaka 25, anasubiria kufa au kustaafu. Watu wa namna hiyo wamekuwa wakwamishaji wakubwa wa maendeleo,” aliongeza.

“Hapa kwetu kwa mfano, tumepata changamoto ya wizi wa dawa kwenye halmashauri yangu. Zahanati 10 zimeibiwa dawa ambazo zinafanana na zinauzwa mtaa wa pili watu wapo na wanaendelea kula mshahara.

“Makamu Mwenyekiti bunge lipo na mimi nilishapita bungeni. Bunge lipo kwa ajili ya kubadilisha sheria. Tusiendelee kuishi kwa mazoea. Kama kweli tumepanga kumsaidia Rais, tubadilishe sheria badala ya watu kusubiri kustaafu , basi wafanye kwa mikataba,’ alisema.

MADUDU BANDARI

Mkuu huyo wa wilaya alisema kero zilizoko bandarini ni nyingi kutokana na kuwapo kwa tozo nyingi na kusababisha kukosekana kwa mapato.

“Nikiangalia fedha inayopotea hapa na Rais anaenda nje kutafuta fedha, ninaumia sana. Ushauri wangu hizi taasisi kubwa mfano TRC (Shirika la Reli Tanzania), TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) ifike mahali wawekwe watu ambao wana uzoefu wa biashara.

“Serikali inapata hasara na mtu hajali ilimradi anakula ana gari lina kiyoyozi maisha yake yanaendelea na watoto wanasoma Ulaya. Kwa namna hii hatutatoboa,” alisema.

Alisema kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo na anapoteuliwa hajawekwa hapo kama sofa. Kazi yake ni kuishauri serikali jambo gani la kufanya na kama kuna kikwazo anaeleza ili mambo yaende.

Alisema jambo jingine linalokera ni wakala wa serikali wanaohusika kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.

“Huwezi kuamini maji ya kunywa au juisi yenye ithibati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama vinavuka kwenda Congo ni lazima watu wa mionzi wachukue kwenda kupima kabla ya kuruhusiwa.

WATUMISHI ARDHI WACHONGEWA

Pia alisema ana mwaka mmoja na miezi miwili tangu alipofika Kigoma na katika majukumu yake mengi anayoyafanya ni kusuluhisha kesi za ardhi.

“Mafaili mengi ni ya malalamiko ya ardhi katika kujifunza kwangu. Nilichogundua changamoto nyingi zilisababishwa na watumishi wa ardhi ambao hawakuwa waaminifu.

“Serikali imeshapata hasara kubwa kupitia watu wa namna hii. Nilishawahi kwenda kusuluhisha mgogoro ambao halmashauri ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh milioni 287 na Sh. milioni 100 imeshalipwa tukawa tunadaiwa Sh milioni 187,”alisema.

Mahawe alisema alipofuatilia na kwenda kufanya vikao na wazee wa eneo husika, ilionekana ni kesi ya kutengenezwa na waliokuwa watumishi wa ardhi walijificha kupitia kivuli cha wananchi ambao hawamiliki ardhi hiyo.

“Utapeli upo kupita kiasi, hao watu wanatengeneza na kujifanya wanafanya kazi ofisi ya Rais au TAMISEMI wanakupigia simu za vitisho. Hao ni watu waliotengenezwa na watumishi waliopita katika hii Halmashauri,” alisema.

Chanzo: Nipashe
Kwanini aongee Leo,au kanusa nini?
 
hahahaha Tanzania bwana, shida sana.

Shida imeanzia jui kwenye kichwa imeshuka mpaka mkiani, basi tafrani, tumebaki kurushiana mpira tu na kushikana uchawi.

Mawaziri, MaRcs nk wenyewe wanapog misele tu na mafuta ya serikali na kuendelea kupiga porojo za siasa huku mambo hayaendi
 
Hao wote na DC akiwemo,hayati J.K Nyerere alisema ni "manzi ganyanza".
 
Ajira za mikataba serkalini haziwezekani, too expensive. Huyo DC nadhani haelewi implications za ajira za mikataba, awaone wanasheria wamweleze
 
Kwan Mtumishi akiharibu SI anafukuzwa? MADC Wana wivu kwasababu wao wanatumbuliwa tu bila ushahidi au kama hajamfurahisha Bwana Mkubwa. Tukianzia kuwawekea watumishi mikataba tutatengeneza machawa weng sana.

Watu wa kusifu na kuabudi ili waongezewe mikataba.

CCM Ndio chanzo Cha matatizo kwenye hii nchi.

Tuiondoe CCM Kwanza
 
Hoja zenye nguvu kwa taifa (Mkuu wa wilaya ya kigoma).

Pia ameshauri kufanyika kwa mabadiliko ya sheria kwa watumishi wa serikali kwa kupewa mikataba ya muda ya ajira ili waache kufanya kazi kwa mazoea.

Mahawe aliyasema hayo juzi wakati Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwataka viongozi kujibu kero zilizowasilishwa na wananchi.

Mahawe alisema awali alikuwa anafanya kazi sekta binafsi kabla ya kuteuliwa na kuweka bayana kwamba kama kweli wanataka kuijenga Tanzania ya watu waadilifu na wachapa kazi, ifike wakati kubadilishwe sheria za ajira.

“Zisiwe hizi za ‘permanent and pensionable’ (ajira za mkataba wa kudumu). Sheria hii inawaumiza wateuliwa wa Rais hasa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi. Watu ambao hawatekelezi majukumu yao katika Halmashauri ni wakuu wa idara,” alisema.

Kwa mujibu wa Mahawe, watu hao hawatekelezi majukumu yao kwa sababu wanajua mkurugenzi atatumbuliwa na mkuu wa idara ya elimu, afya na mhandisi wa majengo wao watabaki.

“Ninaomba ifike mahali Mkurugenzi anavyotumbuliwa aondolewe na wakuu wa idara wote kwa sababu tunawaumiza watu wasio na hatia. Mkurugenzi ni mtu mmoja, chini yake ana wakuu wa idara 14. Wakiamua kumkwamisha, gurudumu haliendi. Watu hawa wanafanya kazi kwa mazoea kwa sababu wanajua hawawezi kuondolewa. Tufanye tu kama sekta binafsi mtu anaajiriwa kwa mkataba maalum,” alisema.

“Utakuta mtumishi ameajiriwa akiwa na miaka 25, anasubiria kufa au kustaafu. Watu wa namna hiyo wamekuwa wakwamishaji wakubwa wa maendeleo,” aliongeza.

“Hapa kwetu kwa mfano, tumepata changamoto ya wizi wa dawa kwenye halmashauri yangu. Zahanati 10 zimeibiwa dawa ambazo zinafanana na zinauzwa mtaa wa pili watu wapo na wanaendelea kula mshahara.

“Makamu Mwenyekiti bunge lipo na mimi nilishapita bungeni. Bunge lipo kwa ajili ya kubadilisha sheria. Tusiendelee kuishi kwa mazoea. Kama kweli tumepanga kumsaidia Rais, tubadilishe sheria badala ya watu kusubiri kustaafu , basi wafanye kwa mikataba,’ alisema.

MADUDU BANDARI

Mkuu huyo wa wilaya alisema kero zilizoko bandarini ni nyingi kutokana na kuwapo kwa tozo nyingi na kusababisha kukosekana kwa mapato.

“Nikiangalia fedha inayopotea hapa na Rais anaenda nje kutafuta fedha, ninaumia sana. Ushauri wangu hizi taasisi kubwa mfano TRC (Shirika la Reli Tanzania), TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) ifike mahali wawekwe watu ambao wana uzoefu wa biashara.

“Serikali inapata hasara na mtu hajali ilimradi anakula ana gari lina kiyoyozi maisha yake yanaendelea na watoto wanasoma Ulaya. Kwa namna hii hatutatoboa,” alisema.

Alisema kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo na anapoteuliwa hajawekwa hapo kama sofa. Kazi yake ni kuishauri serikali jambo gani la kufanya na kama kuna kikwazo anaeleza ili mambo yaende.

Alisema jambo jingine linalokera ni wakala wa serikali wanaohusika kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.

“Huwezi kuamini maji ya kunywa au juisi yenye ithibati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama vinavuka kwenda Congo ni lazima watu wa mionzi wachukue kwenda kupima kabla ya kuruhusiwa.

WATUMISHI ARDHI WACHONGEWA

Pia alisema ana mwaka mmoja na miezi miwili tangu alipofika Kigoma na katika majukumu yake mengi anayoyafanya ni kusuluhisha kesi za ardhi.

“Mafaili mengi ni ya malalamiko ya ardhi katika kujifunza kwangu. Nilichogundua changamoto nyingi zilisababishwa na watumishi wa ardhi ambao hawakuwa waaminifu.

“Serikali imeshapata hasara kubwa kupitia watu wa namna hii. Nilishawahi kwenda kusuluhisha mgogoro ambao halmashauri ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh milioni 287 na Sh. milioni 100 imeshalipwa tukawa tunadaiwa Sh milioni 187,”alisema.

Mahawe alisema alipofuatilia na kwenda kufanya vikao na wazee wa eneo husika, ilionekana ni kesi ya kutengenezwa na waliokuwa watumishi wa ardhi walijificha kupitia kivuli cha wananchi ambao hawamiliki ardhi hiyo.

“Utapeli upo kupita kiasi, hao watu wanatengeneza na kujifanya wanafanya kazi ofisi ya Rais au TAMISEMI wanakupigia simu za vitisho. Hao ni watu waliotengenezwa na watumishi waliopita katika hii Halmashauri,” alisema.

Chanzo: Nipashe
Zitto yuko wapi? Muislamu mwenzenu ni rais bara na visiwani hamsemi kabisa. wasaliti wakubwa nyie. matumbo yenu ......
 
Abdul huu ndio uzalendo
P
 
Wanasiasa wanapenda sana kujisafisha kwa wananchi. Wao ndio wakwamisha maendeleo wakubwa wa taifa hili wakianzia huko juu kabisa. Kazi yao ni kuitafuna nchi tu, mbona hawapigii kelele ziwepo sheria zinazowawajibisha!!!
 
Abdul Nondo na wewe akili zako kama huyo DC,hivi hujiulizi katika hii Dunia ni Taifa gani lina Watumishi wa umma ambao wapo kwa miktaba ya muda mfupi??,jibu ni hamna Serikali hata mmoja na hiyo ni kutokana na principle za kiuchumi .
Kama Watumishi wanafanya vibaya jua Utawala ndio shida,na sio Watumishi.Utawala wa Juu kuanzia SAMIA ni shida-mfumo mzima wa Utawala hauna uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom