PreGE2025 DC Songea, Kapenjama: Uchaguzi haujaiacha Afrika salama, Uchaguzi usiharibu amani ya nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanasimamia na kuhimiza amani nchini ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Akizungumza wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ruvuma, April 20, 2025 Mhe. Ndile alitoa salamu za serikali na kusisitiza umuhimu wa mshikamano wa kitaifa. Alieleza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi, hususan wa dini, kuhubiri na kulinda amani, kwa kuwa historia imeonesha jinsi baadhi ya mataifa ya Afrika yalivyoingia kwenye machafuko kutokana na mivutano ya uchaguzi.

“Nchi nyingi barani Afrika zimeathirika na machafuko yanayotokana na chaguzi, jambo ambalo linaweza kuzuiwa endapo tutadumisha maelewano, mshikamano na heshima kwa misingi ya demokrasia. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhakikisha haya hayaingii nchini mwetu,” Alisema Mhe. Ndile.

Pia Mhe Ndile ameongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani.

Chanzo: Manara TV
 
Mungu Ibariki Tanzania 🐒
 
Uchaguzi haujaiacha Africa salama kwa sababu madikteta wanakatalia madarakani pale ambapo wananchi walio wengi wanapowakaata kwa kura.
 
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanasimamia na kuhimiza amani nchini ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Akizungumza wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ruvuma, April 20, 2025 Mhe. Ndile alitoa salamu za serikali na kusisitiza umuhimu wa mshikamano wa kitaifa. Alieleza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi, hususan wa dini, kuhubiri na kulinda amani, kwa kuwa historia imeonesha jinsi baadhi ya mataifa ya Afrika yalivyoingia kwenye machafuko kutokana na mivutano ya uchaguzi.

“Nchi nyingi barani Afrika zimeathirika na machafuko yanayotokana na chaguzi, jambo ambalo linaweza kuzuiwa endapo tutadumisha maelewano, mshikamano na heshima kwa misingi ya demokrasia. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhakikisha haya hayaingii nchini mwetu,” Alisema Mhe. Ndile.

Pia Mhe Ndile ameongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanasiasa ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani.

Kisingizio ni amani, but hawaongelei haki
 
Back
Top Bottom