Walimu wawili wa Shule ya Sekondari Musa Akasha iliyoko wilayani Rorya Mkoa wa Mara wamesota mahabusu kwa wiki moja bila dhamana kwa amri ya Mkuu wa Wilaya kwa kosa la kuadhibu mwanafunzi ambaye alifika shukeni akiwa amevalia viatu vya plastiki ambavyo si sare ya shule.
Walimu hao walikamatwa tangu alhamisi tarehe 22/08/2019,wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime jana na kuachiwa kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na viongozi wa CWT Rorya.
Taarifa zinadokeza kuwa DC Chacha alitoa onyo kali kwa Mwalimu yeyote atakayekwenda kuwajulia hali wenzie huko mahabusu na hata kuwawekea dhamana ndo Chama Cha Walimu CWT kilijitosa kuwadhamini mahakamani.
My take..
Inawezekana walimu Hawa wamefanya kosa kweli maana Ni taarifa ya upande mmoja pekee ndo tunayo
Sijui ni kwa nini vyombo vya habari Rorya vimekaa kimya juu ya kadhia hii.Walimu wa nchi hii wamegeuka kuwa ngazi kwa watawala uchwara kutafuta umaarufu na hatimaye kupanda vyeo.
Huu ni mwendelezo wa manyanyaso ya watawala dhidi ya walimu wa nchi hii.Sijui ni lini haya yatakuwa na mwisho? Ikumbukwe tu kwamba mwalimu huyu anayetendewa haya ameelemewa na changamoto lukuki ambazo zinaathiri utendaji wake wa kazi.
Walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu,hawana nyongera ya mshahara kwa miaka kadhaa sasa,hawalipwi madeni yao lakini kwa watawala wetu njia pekee ya kuwafariji na kuwatia moyo walimu ni kuwasweka mahabusu na kuwanyima dhamana.
Tatizo la yote haya ni sababu tunatawaliwa na viongozi ambao hawana hofu ya Mungu ndani yao.Kwao vyeo ni Mungu,hawaoni shida kukuumiza ilimradi tu waifurahishe mamlaka ya uteuzi ili wafikiriwe kwa nafasi za juu zaidi.
Poleni Walimu wa Musa Akasha.Lakini pia hovyo kabisa Mkuu wa Shule hiyo uliyeogopa hata kwenda kuwajulia hali walimu wako wakiwa mahabusu kwa siku zote hizo.
Wanajukwaa Je hii Ni kweli? Je Ni kweli DC mamlaka ya kutoa amri ya kumuweka mtu rumande kwa wiki nzima bila kumpeleka mahakamani?