Mimi nadhani mpaka DC anaingilia, na kwa kuwa umesema umepata maelezo ya upande mmoja tu, basi kunaweza kuwa na assumptions nyingi;
Kwa mfano:
1. Inawezekana hiyo adhabu ilikuwa kubwa kiasi ambacho hailingani na kosa hata kumletea madhara ya kimwili mwanafunzi huyo
2. Kuna muongozo wa utoaji adhabu kwa wanafunzi na hivyo walimu hao hawakufuata mwongozo huo
Mathalani mwongozo unasema;
✓• Mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya kuchapa viboko mwanafunzi ktk shule yoyote ni Mwalimu mkuu au Mkuu wa shule pekee.....
Ama la, basi atoe (akasimu) mamlaka hayo kwa mwalimu mwingine yeyote kwa maandishi, kwamba ameruhusu adhabu itolewe......
✓• Wavulana wachapwe viboko hivyo matakoni na wasichana mikononi.
✓• Wanafunzi wa kike sharti waadhibiwe (wachapwe) na mwalimu wa kike na vivyo hivyo wa kiume na mwalimu wa kiume
✓• Maximum ya idadi ya viboko kwa kila kosa ni sita (6) kwa siku. Ukichapa zaidi ya hapo unakuwa unavunja sheria. Kama mwanafunzi imepitishwa kuwa achapwe viboko 12, maana yake atachapwa 6 leo na kesho amalizie vile vingine 6
✓• Lazima kabla ya kutolewa adhabu hiyo ithibitike kuwa kosa hilo linastahili adhabu hiyo na njia zingine zozote zimeshindikana kutumika kurekebisha tabia ya mtoto huyo.....
Kwa lugha rahisi ni kuwa FIMBO iwe ni the highest resolution of solving the problem kabla ya final resolution ambayo ni kumwondoa mwanafunzi shuleni kwa muda (temprarily suspension) au kumfuta shule moja kwa moja (expulsion)....
✓• Mwisho, sheria ya CORPORAL PUNISHMENT inataka adhabu hiyo iwe recorded kwenye kitabu cha kumbukumbu ya adhabu (Black book) na ielezwe wazi aina ya kosa lililotendwa na mtoto, aina ya adhabu aliyopewa, jina la mwalimu aliyetoa adhabu, sahihi yake na sahihi na jina la mwanafunzi aliyepokea adhabu hiyo
3. Ni bahati mbaya kuwa wengi wa walimu wa siku hizi wakiwemo hata walimu viongozi wa shule nyingi za sasa ama hawajui haya na hivyo kujikuta wanaendesha shule kwa desturi na utamaduni wa mapokeo tu bila kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.....
Hii imeleta shida sana kwenye nyingi ya shule hususani za umma na hivyo kuonekana shule sasa ni kama uwanja wa mapambano kati ya walimu na wanafunzi wao....
Hili linathibitishwa kesi mbili za juzi kati hapa ambapo mkuu wa shule moja alimwadhibu mwanafunzi kwa fimbo zisizo na idadi...
Hata baada ya kuwa amechapa vya kutosha, hakuridhika bado, akamfungia mwanafunzi ndani ya kasiki (strong room)
na mwanafunzi huyo kukosa hewa na baadaye kufariki dunia....!!
Kesi ya pili ni ile ya walimu wawili wa kiume kumshambulia mwanafunzi wao kwa fimbo na mateke kwa tuhuma kuwa aliiba pochi ya mwalimu mwenzao wa kike ambaye ilikuja kuthibitika kuwa kumbe pochi hiyo ilikuwa mis-placed tu somewhere na mwalimu mwenyewe...
Matokeo yake ni kuwa walimjeruhi kijana huyo, akalazwa hospitali na badaye kama sijakosea alifariki dunia...!
KWA KESI HII TUNAYOJADILI HAPA, MAONI YANGU NI:
1. Kosa la kuvaa viatu visivyokuwa sare ya shule halikustahili kufikia hatua ya mwanafunzi kuadhibiwa kwa viboko....
Je, mwalimu/walimu husika walijaribu kufuatilia kujua ni kwanini mtoto huyo alikuja na viatu hivyo ambavyo siyo sare ya shule?
Inawezekana kabisa tatizo haliko kwa mwanafunzi bali liko kwa mzazi/wazazi/walezi wake labda hawana fedha ya kununua kiatu kinachotakiwa ama matatizo tmengine ya kifamilia....
Kama ndivyo ilivyo hapo juu, hawa walimu wetu kabla ya kuanza kumshushia fimbo walimpa nafasi mtoto huyo kujirekebisha?
Waliwashirikisha wazazi/walezi wa mwanafunzi juu ya tatizo la mtoto la kutokuwa ktk proper school uniforms?
2. Kwa upande wa DC na kama tu ilivyoelezwa hapa ndivyo ilivyo kweli.....basi naye ana makosa tena makubwa sana!!
Binafsi naweza kusema kwa hakika kabisa kuwa hana BUSARA wala HEKIMA za kiuongozi..
Wote tunafahamu kuwa zipo mamlaka za kiutumishi kwenye kila kada ya utumishi....
Alipaswa kwa kuagiza kama walimu hao wamekiuka kanuni za kiutumishi kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za utumishi....
Hata kama ishu yao ilishakuwa na sura ya jinai, bado angechia mamlaka zinazohusika kuchunguza na kuchukua hatua...
DC kujigeuza kuwa yeye ndiye polisi na ni mahakama pia siyo sawa hata kidogo hata kama walimu hao wametenda kosa kwa mtazamo wake....!