Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametoa wito kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa kata na polisi kata wilayani humo kuhakikisha vijana, hususan wale wanaojishughulisha na ubodaboda, umachinga na saluni; wanalelewa na kuratibiwa ipasavyo ili kuepusha uwezekano wa kutumiwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani kama ilivyoshuhudiwa wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Akizungumza hivi karibuni katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, kilichowahusisha viongozi wa polisi wa mkoa na wilaya, Watendaji wa Kata na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, DC Mpogolo amesema vijana wengi waliojiajiri katika sekta mithili ya hizo wako katika mazingira yanayoweza kuwafanya kutumiwa kirahisi pale changamoto zinapotokea.
“Yanapotokea matatizo kama haya vijana hawa ndipo huwa wanatumika, wanaweza wakatumika sio kwa sababu yeye anataka kufanya uhalifu ule ila anatumika kwa sababu analipwa ile pesa”, amesema Mpogolo.