DC Ludewa: Waliosusia kikao changu wakamatwe

DC Ludewa: Waliosusia kikao changu wakamatwe

Kuna yule mwingine alichapa walimu bakora na hakuna hatua aliyochukuliwa. CCMScrow ni walewle
 
Wananchi wakienda kufanya kazi hamtaki mnataka waje kwenye mikutano yenu kwa nguvu wakati wao kwenye mikutano yao wananyimwa.

Fanyeni mikutano yenu na watu wenu au kaazimeni watu kule Rwanda
 
Sasa utawalazimisha watu kuipenda serkali kipitia ccm????

Ninaamini HOJA si hivyo ilivyoletwa na kama ni kweli basi ipo shida !!! na ka ushauri nadhani waliostahili kukamatwa ni waandaaji wa mkutano huo, kwa kushindwa kwao
 
huo mwaliko wa kikao ulikuwa ni walazima au hiari ??

hiyo fidia haipo kisheria wala ki taratibu za mikutano... hiyo itakuwa mpya kufanyika...

dc anatumia madaraka yake vibaya.
 
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw. Andrea Tsere ametoa agizo la kukamatwa kwa wananchi wa kitongoji cha Ngalawale wilayani humo kwa kususia kikao cha mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha wananchi kususia vikao vya maendeleo vinavyoitishwa na serikali ambapo ikitokea tatizo au mradi ukiwa unafanyika katika eneo lao wanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba hawashirikishwi.

“Naagiza wananchi wa kitongoji hiki wakamatwe majumbani hadi walipe faini, haiwezekani tuitishe kikao cha kujadili maendeleo yanayowahusu na wao washindwe kujitokeza hii siyo dalili nzuri katika kuwashirikisha mambo yanayowahusu” Amesema Tsere.

Aidha tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya , Bw. Tsere amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo amesisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani kazi hizo anafanya kwa ajili yao.

Chanzo: IPP Media
Hiyo faini anapewa nani?kama wananchi hawashiriki kwenye vikao au mikutano suluhu ni kuangalia namna ya kuwahamasisha sio kuwakamata,utawakamata na baadae hawatakuja tena,au wanaweza kuja wasikupe ushirikiano kwa namna yeyote ile,utabak unaongea peke yao.
Jaman mbona haya mambo ni rahisi sana tu,hapo sijui watashtakiwa kwa kosa gani yaillah
 
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw. Andrea Tsere ametoa agizo la kukamatwa kwa wananchi wa kitongoji cha Ngalawale wilayani humo kwa kususia kikao cha mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika eneo la tukio mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha wananchi kususia vikao vya maendeleo vinavyoitishwa na serikali ambapo ikitokea tatizo au mradi ukiwa unafanyika katika eneo lao wanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba hawashirikishwi.

“Naagiza wananchi wa kitongoji hiki wakamatwe majumbani hadi walipe faini, haiwezekani tuitishe kikao cha kujadili maendeleo yanayowahusu na wao washindwe kujitokeza hii siyo dalili nzuri katika kuwashirikisha mambo yanayowahusu” Amesema Tsere.

Aidha tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya , Bw. Tsere amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jambo ambalo amesisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani kazi hizo anafanya kwa ajili yao.

Chanzo: IPP Media
hii ni dharau ya wazi waliyoonyesha kwa mh. DC. wakamatwe mara moja.
 
Huyu DC nilishawahi kuonana nae mara moja katika mazungumzo yake pamoja na uvaaji wake nikaona hayupo sawa kiakili..ngoja tuone
 
Walishaambiwa mikutano mpaka 2020, walikuwa kazini, labda awalaumu kwa kushindwa kutofautsha mikutano ya siasa na maendeleo
 
Hivi huyu Tsere ni mtoto wa Mzee Tsere,aligombea Ubunge Jimbo la Karatu 2005 na baadae akawa Mkuu wa Wilaya ya Ilala?
Nadhani ndio huyu..ila mkuu naona kama hayupo sawa kichwani nilishawahi kuonana nae
 
Hakuna mwananchi ambaye ana weza akakimbia kikao ambacho ana jua kina faida kwake,ukiona wananchi wanamkimbia mkuu wa wilaya ujue kuwa mkuu wa wilaya ni chengachenga,kwa hiyo asiwalazimishe wananchi kwenda kusikiliza pumba zake.
 
Kuna mkuu wa mkoa Fulani alitangaza kuanza kukamata watu wote wasio na kazi mkoani mwake. Lakini watu hao hao ndiyo wakiokuja kumsitiri wakati wa ziara aliyofanya mkoani humo. Maana wasio na kazi ndiyo walijitokeza na kujazana kwenda kumsikiliza.
Ama kweli usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 
Back
Top Bottom