DC Iringa Mjini, Richard Kasesela amelazimika kuomba radhi kwa umma baada ya kutoa taarifa feki ya kifo cha Dr. Salim Ahmed Salim

Kwa kiongozi kama yeye ni upuuzi wa hali ya juu alioufanya. Anyway, tushaelewa uwezo wake wa kufikiri na kuweka kitu kifuani
 

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela, amelazimika kuomba radhi kwa umma, baada ya kusambaza taarifa za uongo juu ya kufariki kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim.

Loading...
Hapo jana usiku Kasesela alichapisha taarifa kwenye mtandao wa Twitter, ukieleza kutokea kwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim zilizodai kuwa mauti hayo yamemfika akiwa nchini Uingereza, ambapo baadae alizikanusha.


Mapema jana Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping alimtunuku Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Tanzania Dkt Salim, kuwa miongoni mwa watu waliosaidia nchi hiyo kurejeshwa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Mataifa.

Huyu ni wa kutumbuliwa tu.
Kama mkuu wa wilaya anaamini habari za udaku, basi ata kuongoza watu itakuwa ni tatizo.

ALIKUWA ANAHITAJI WACHANGIAJI WENGI KWENY MTANDAO WAKE - FOLLOWERS
 
Kulikuwa na haja gani yakukimbilia kutangaza msiba wa watu? yeye ni msemaji wa familia? yeye ni msemaji wa Serikali? anastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa udaku
Unajua kiherehere ni kitu mbaya sana
 
Endapo kama habari hii ina ukweli, KWA mujibu WA Sheria ya Mawasiliano ya Kimtandao ya huko Tz (EPOCA), anastahili kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria ili apewe haki yake anayostahili kulingana na makosa yake
Hawatamfanya chochote ni wa kijani huyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom