DC Humphrey Polepole ajutia uongozi wa awamu hii

DC Humphrey Polepole ajutia uongozi wa awamu hii

Ameyakuta madudu ambayo hakutegemea, amegundua viongozi wengi wanatenda kinyume Na wanayoyahubiri kwenye majukwaa.

Ukitaka uende sambamba Na utawala huu, nusu uwe mnafiki nusu uwe mkweli.

Pole Ndugu Polepole, chagua moja kuwa Moto au kuwa baridi maana unaonekana uvuguvugu huuwezi.!
Kama alivyoamua slaa kuwa ccm
 
Mtoto akililia wembe mpe, alitaka kuteuliwa na ameteuliwa kweli sasa analia lia nini? Kama vipi aachie ngazi kuna wakina lizaboni wanaitolea udenda hiyo nafasi hawalali usiku kucha wanatunga ngonjera humu ili wakumbukwe.
 
Ameyakuta madudu ambayo hakutegemea, amegundua viongozi wengi wanatenda kinyume Na wanayoyahubiri kwenye majukwaa.

Ukitaka uende sambamba Na utawala huu, nusu uwe mnafiki nusu uwe mkweli.

Pole Ndugu Polepole, chagua moja kuwa Moto au kuwa baridi maana unaonekana uvuguvugu huuwezi.!
ameambiwa anyanganye sumaye shamba amwache mkapa wakati shamba la sumaye liko jirani na shamba la mkapa
 
Nakubaliana na wewe mkuu, kwenye rasimu ya katiba waliweka wazi kabisa kwamba cheo cha mkuu wa wilaya na mkoa ni kubebesha walipa kodi mzigo havina ulazima wa kuwepo. Sasa yeye angeonesha mfano kwa kukataa hicho cheo. Lakini kwa vile aliamua kula matapishi yake lazima tumbo liume, hakuna namna nyingine!
Katiba haikuandaliwa na Polepole au warioba bali wao walichofanya ni kukusanya maoni ya wananchi na kuyaweka pomoja na kuandika kwenye mtiririko mzuri. Kumbuka yapo mambo mengine yapo kwenye rasimu ya tume ya warioba ambayo hata baadhi ya wajumbe wa tume hawayakubali lkn waliamua kuyaweka kwakuwa ndio matakwa ya wananchi. Alichokuwa anafanya warioba na Polepole na baadhi ya wajumbe ni kutetea maoni ya wananchi dhidi ya uharamia wa wanasiasa na sio kutetea maoni yao binafsi.
Tuache tabia ya kuwalisha watu maneno. Naamin Polepole ni moja ya watu wazuri sana katika uongozi. Anayo hekima ya uongozi na anapenda haki sana.
 
Kuwa chini ya Makonda na JPM ni mtihani , unaweza kuwa creative na mawazo yako yakabaunciwa.Binafsi siwezi kafanya kazi chini ya hao watu . Unatakiwa uwe unaswagwa kama kondoo , Makonda hataki kupitwa . lazima aweke figisu ili yeye aonekane ndo anafanya kazi .
 
Pole Pole anaongea Sana na ana point nyingi sana muhimu Za kuisaidia Ubungo na hata Dsm kwa ujumla, kinachotokea ni kwamba Makonda anahakikisha anakosoa kila ushauri na proposal ya Humphrey...

Makonda kamfunga domo kwa bandeji na Siku si nyingi Pole Pole anatumbuliwa.

Lizaboni jiandae kuwa Dc Ubungo.... Mungu amesikia kilio chako mkuu
 
Huyu bwana polepole, Umaarufu wake ulitokana na taaluma yake ya sheria kuiwakilisha tz, yote(mchakato wa katiba mpya) lakini kwa sasa, anaiwakilisha wilaya mpya ya UBONGO ni lazima apwaye kimawazo na atweet vitu kama hivyo
 
Mhe. Polepole hongera sana kwa kuanzisha ofisi za Wilaya ya Ubungo ktk eneo la kibamba, hii itasaidia kupatikana kwa maendeleo ya haraka pembezoni mwa Mji.

Sasa ni wakati wa wana Ubungo kuungana na kuleta maendeleo ktk Wilaya yao!
Binafsi namkubali sana Mhe Polepole ni kiongozi makini na mwenye maono, naamini ataleta mabadiliko makubwa.

Hata hivyo amekuwa kimya sana!!!
 
Tatizo nafsi inamsuta kwa unafiki alikuwa anajifanya kutetea wananchi kapewa madaraka amekuwa kimya
 
Kutumwa umchune ngozi binadamu mwenzako ni kazi sana ukizingatia huoni hatia yake.
 
Huyu ni mnafiki sana,angekuwa mkweli asingekubali hicho cheo alichopendekeza kiondolewe kwenye katiba mpya..poor him
 
kama anaona kuna baadh ya maamuz hayaend sawa c apge chn mzgo arudi kwene kaz yake ya unna alikopgwa pchwa ktk kuhubir uwongo alousoma kwene Ds,au huko njaa kali kama mwenzie Machali baada ya maisha kubana karud kichakan!
 
Alishapewa kijiti, mwache ashiriki na walamba asali wenzake!!
 
c1ea768d92ac8f742ea8d46cc72276d8.jpg
5c011279ea3516c02871d1f47601f3df.jpg
 
Back
Top Bottom