Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo mchana amefika mahakama ya Rufaa akiongoza ujumbe wa viongozi mbali mbali akiwemo Meya wa manispaa ya Kinondoni Mstahiki Boniphace Jacob kuhakikisha kuwa rufaa dhidi ya kesi ya Coco beach ambayo kampuni ya Q-Consult inayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji ilipewa ushindi mapema mwishoni mwa mwaka 2015.
Hali hii inafuatia kile kinachoonekana kama ni njama za kuihujumu serikali ili muda wa rufaa upite bila ya Manispaa ya Kinondoni kukata rufaa dhidi ya ushindi wa Q Consult. Leo Ijumaa ndiyo ilikua siku ya mwisho ya kukata rufaa na wanasheria wa manispaa ya Kinondoni tangu hukumu itolewe mwaka jana walikua hawajakata rufaa.
Rais Dr. John Magufuli alitoa agizo mwishoni mwa mwaka jana kuwa ufukwe wa Coco beach uachwe kama ulivyo ili wananchi wa kawaida na wanyonge waendelee kufurahia rasilimali hiyo bure.
Kutokukata rufaa ya kesi kungesababisha mgongano wa agizo la Rais na utekelezaji wa hukumu ya mahakama jambo ambalo lingeiweka rehani fukwe ya Coco beach.
Hivi karibuni mwanasheria wa manispaa ya Kinondoni alisimamishwa kazi kwa makosa ya kutotimiza wajibu wake vizuri hali iliyoisababishia manispaa hiyo hasara.
"Baadhi ya wanasheria wasio waaminifu na Wazalendo wamekua wakinunuliwa na wafanyabiashara na kupindisha mambo hali inayosababishia serikali hasara. Katika hili nilimwambia Mkurugenzi kuwa rufaa isipokatwa ajiandae kubeba mzigo huo yeye mwenyewe...Hili ni jambo lenye maslahi ya wanyonge na halina itikadi ya chama. Serikali iko pamoja na wananchi. "
Alisema Mh. Hapi.