Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 740
- 828
Naam Habari zenu waungwana.
Namzungumzia ambaye sasa ni mkuu wa wilaya ya kigoma mjini ndugu Dkt Rashid Chuachua, ambaye pia amewahi kufanya kazi chini ya ndugu Albert Chalamila. Chalamila alipokuwa mkuu wa mkoa wa mbeya Chuachua alikuwa ni mkuu wa wilaya ya mbeya mjini, kama nimekosea mtanirekebisha hapa.
Dkt Rashid Chuachua ni mwanasiasa ambaye Mwenyezimungu kwanza, amembariki kibali cha sauti yenye mamlaka ya kuzungumza na wananchi, lakini kama hii haitoshi, ni uhodari wake wa kutatua migogoro ya kijamii kwa kutumia akili kubwa ya kibinadamu bila matumizi ya nguvu nyingi, hili ni jambo ambalo limewashinda wanasiasa wengi wa kiafrika wanapopewa madaraka.
Chuachua, pamoja na uhodari wa utatuzi wa migogoro hapo ofisini kwa mkuu wa wilaya, ni mwanasiasa ambaye kila neno linalotoka kinywani mwake basi hujitahidi liwe angalau limepitishwa kwenye mamlaka ya udhibiti viwango ya kichwani kwake, ndio maana utamsikia akiongea taratiibu saana na matokeo yake ni kuwa, yeyote atakayemsikiliza basi atamuelewa kwa haraka sana.
Hatuyasemi haya kwa bahati mbaya hapana, hebu tuangazie namna alivyotuliza ghasia kati ya waendesha bodaboda na askari polisi pale mkoani kigoma miezi mitatu tu iliyopita.
Kwa hapa Dar Es Salaam na mikoa mingine imezoeleka likitokea la kutokea linalohusu vurugu ama migomo basi haraka sana mkuu wa mkoa ndiye huja kutuliza maneno, wakuu wa wilaya wote hujifungia maofisini huku wakiwa wanatetemeka tete hawajui nini cha kusema ispokuwa kwa Paul Makonda tu alipokuwa DC.
Ukisikiliza mahojiano kati ya waandishi wa habari na bodaboda waliofanya vurugu hizo pale rondabout ya mwanga, malalamiko yao makubwa ni kuwa polisi walikua wanawakamata bila ustaaraabu kwa sababu za kukosa leseni, side mirror na kitambulisho cha utaifa, huku kamanda wa polisi wa mkoa huo akikazia kuwa wengi sio raia.
Ukilinganisha pande mbili za sarafu, wanamigogoro wote hawa wanazohoja za kutetea upande wao, bodaboda wa ujiji ambao wengi wao hata taaluma ni hafifu, fedha ya kwenda VETA kusoma ni ngumu kwa sababu kwanza mzunguko wa fedha pale mkoani kigoma ni mdogo sana, wananchi wa kigoma ujiji wana umasikini mkubwa kiasi cha kuomba hata nauli ya tsh 500 apunguziwe kwa mia mbili na konda hakatai kwa sababu akikataa nani atapanda ? gari iende irudi wazi? sasa niambie katika sehemu ya namna hiyo ni wananchi wangapi watapanda bodaboda?
Licha ya hivyo vijana wale wameona fursa angalau ya bodaboda ili wasikae bila kazi na ndo inafanya waoe na kuendesha familia kulingana na vipato vyao, halafu unamkwapua bodaboda akatafute leseni ambayo alishindwa mwanzo kuipata kwa sababu ya ugumu wa maisha, je kijana huyu ataenda wapi? familia itabaki vipi? je kumkwapua bodaboda ni kujenga au kubomoa?
Binafsi nadhani jeshi la polisi lina hoja za kisheria lakini hoja za kisheria hazipaswi kuwa na nguvu dhidi ya hoja za kijamii zinazotetea ahueni ya maisha ya mwanadamu yeyote hususani mwanadamu wa kitanzania.
Hii social economic situation tunayoiona leo, bila ubishi ni tatizo la kimfumo lililosababishwa na dola yenyewe, hivyo hizi ndizo zitakuwa consequences zake, ni lazima tufanye "RIGHTING THE WRONG"
Habari ya kujitafutia chakula licha ya a poor economic situation inayoweza kusababishwa na dola ni suala la mtu binafsi, vijana wa kigoma ujiji baada taabu nyingi wameiona fursa kwenye bodaboda waacheni wafanye, kama kuna makosa basi yashughulikiwe kwa upole na sio kuharibu social order inayotaka kujirestore, ikiwa vijana hawa watanyang'anywa bodaboda zao kwa kisingizio cha hoja za kisheria basi bomu la ukabaji, vijana wa mtaani na ujambazi litakuwa tayari kulipuka na hiyo tutaiita kushindwa kwa sheria.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo alipaswa kujiuliza kuwa, pamoja na vijana hao kuwa na makosa ya barabarani je kuwanyang'anya bodaboda zao kungetengeneza socio economic order ya aina gani?. bila kupepesa tu, jeshi la polisi lingekuwa limejipa home work ya ziada ambayo ni ngumu na ukizingatia ni mwaka wa uchaguzi na tungeiita kufeli kwa jeshi la polisi.
Katika kulitambua hilo, Mkuu wa wilaya ya kigoma mjini Dkt Chuachua akaja ma mwarobaini wa aina yake na ndio maana hapo awali nikasema Rashid Chuachua anatufaa mkoa wa Dar Es Salaam hivyo apewe nafasi ya kutuongoza.
Chuachua badala ya kuwaletea vurugu na maneno makali ya kiutawala, kwa kutambua taabu za kiuchumi zilizopo wilayani hapo, akawaombea bodaboda wote programu ya mafunzo VETA kwa punguzo la bei, yaani kutoka tsh 40,000/= hadi tsh 30,000/=, huku fomu ya kuombea mafunzo ikitolewa bure. hii si juhudi ndogo hata kidogo, VETA ni taasisi inayohitaji faida.
Kwa kutambua ajali zinazotokana na bodaboda wilayani hapo ambazo zinasababisha vifo ama ulemavu wa kudumu na wakati mwingine majeraha makubwa yanayohitaji fedha nyingi kugharamia, Chuachua akawataka wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha wanawatafutia bima ya afya madereva hao ili kulinda nguvu kazi ya taifa. Vilevile akawatwika jukumu lingine matajiri wa vijana hao la kuhakikisha wanapata leseni, huku akikazia kuwa 'ni serikali isiyowajibika peke yake inayoweza kuona jambo hili ni la kawaida'.
DC Chuachua akawaasa bodaboda waanze kwanza kutafuta namba za NIDA ili kujihakikishia upatikanaji wa leseni hizo baada ya mafunzo ya wiki moja tu, na ili kutimiza hilo vijana waliombwa kuwasilisha taarifa zao mamlaka husika ili washughulikiwe kwa haraka iwezekanavyo.
Pamoja na utii wa sheria, Chuachua alitangaza sera ya mlango wazi kwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya kigoma, na mtu yeyote mwenye tatizo basi amfikie bila kusita. haya tulizoea kuyasikia kwa Paul Makonda peke yake sasa na Chuachua tunaye.
Aina hii ya uongozi na utawala ndiyo ambayo watanzania wanahitaji kuiona, ni lazima kiongozi aoneshe kuguswa na matatizo yanayoikumba jamii yake badala ya kula kiyoyozi na kuenjoy pwekepweke.
Matatizo haya ya bodaboda yanapatikana mikoa yote, nitumie tu jamvi hili kuzitaka mamlaka kuwalea bodaboda wote na kufanya deep analysis ya mambo kabla ya kuchukua hatua za jumlajumla.
Kwa weledi huo aliouonesha DC Chuachua katika kutatua mgogoro kati ya bodaboda na jeshi la polisi, ni wazi kuwa Dkt Rashid Chuachua anaweza kuliongoza taifa katika kipindi cha state crisis na kwa sababu hiyo, ninayo haki ya kutoa maoni kwa wino wa zafarani kuwa mkuu wa wilaya ya kigoma mjini Dkt Rashid Chuachua anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuanzia sasa na kwa wakati mwingine wowote.
Si kwa sababu awe mkuu wa mkoa bali kwa sababu ya uwezo wake binafsi wa kudeal na migogoro ambayo kwa asilimia kubwa upatikanaji wake upo ndani ya jiji la Dar Es Salaam.
Asante.
rajarajabu99@gmail.com