Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 754
- 3,097
Teknolojia inayotumika kuwakamata senene mjini Bukoba imepigwa marufuku kwa madai kuwa inasababisha uchafuzi wa mazingira na inahatarisha usalama kutokana na mfumo wa umeme kufungwa kinyemera kwenye mitego hiyo ya kuzinasa senene
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amekataza kufanyika shughuli za uvunaji wa senene katikati ya mji wa Bukoba kwa kutumia teknolojia inayotumika ya kuegesha mabati kwenye ndoo au mapipa na kuwasha taa zenye mwanga mkali na kisha kukoka moto kwa lengo la kupata moshi wa kulewesha senene watakaokuwa wakiruka kufuata mwanga wa taa,na kueleza kuwa moshi huo umekuwa kero na unasababisha athari kiafya kwa watu.