DC aumbuka kumfukuza diwani wa CHADEMA jukwaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC aumbuka kumfukuza diwani wa CHADEMA jukwaani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 20, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MKUU wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Meja mstaafu Bahati Matala, nusura avuruge kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika wilayani hapa, baada ya kumtimua jukwaani Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura, hali iliyopingwa na wafuasi wa chama hicho. Sakata hilo lililotokea juzi saa 5:00 asubuhi kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya, Matala alipanda jukwaani na kuanza kuwatambulisha viongozi waliojumuika akiwamo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Masanje, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Eliza Bwana na Mwenyekiti wa halmashauri, Alfred Mhanganya.

  Matala baada ya kumwona diwani huyo akiwa amekaa na viongozi hao jukwaani, kwa kutumia kipaza alitangaza akimtaka Wambura kuondoka mara moja. “Bobson ondoka jukwaani mara moja,” alifoka Matala. Hatua hiyo iliwakasirisha watu wengi waliokuwa wamehudhuria na kuanza kuguna, hali ambayo ilitulizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Masanje ambaye alichukua kipaza sauti haraka kutoka kwa Matala, huku akimtaka diwani huyo kurejea mara moja jukwaani na kusalimia wananchi.

  “Bobson tafadhali rudi uwasalimie wananchi wako, sioni sababu ya kumfukuza diwani wa Chadema kwenye jukwaa hili, leo tunasherekea miaka 50 ya uhuru wakati mwaka 1961 tunajitawala, uhuru ulikuwa wa Watanzania wote siyo Chadema wala CCM, sherehe hizi ni za watu wote,” alisema Masanje huku akishangiliwa na wananchi. Licha ya Masanje kupinga uamuzi wa mkuu huyo wa wilaya, alirudia tena upya utambulisho wa madiwani wote akiwataka wasimame na kuwapungia mkono wananchi.

  “Waheshimiwa madiwani popote mlipo pamoja na Bobson simameni muwapungie mikono wananchi,” alisema Matala.Akizungumzia hatua hiyo, baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Wambura alisema alisikitishwa na kitendo cha mkuu wa wilaya kumfukuza jukwaani, ilhali maadhimisho hayo yalikuwa yanafanyika kwenye eneo lake na kwamba, atafikisha suala hilo kwa wananchi.

  Katika hatua nyingine, utoaji zawadi kwenye kada mbalimbali zilizoshiriki maadhimisho hayo nusura uingie dosari baada ya mwanamke mmoja, kuangua kilio mbele ya mgeni rasmi kutokana na kuchakachuliwa kwa zawadi yake ya Sh100,000 aliyoahidiwa kwa kushinda mbio za baiskeli upande wa wanawake.

  Kilio hicho kilianza baada ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kapteni mstaafu James Yamungu, kutangaza Sh50,000 iliyomfanya mwanamke huyo kupinga na kuangua kilio.Baada ya kuona hali hiyo Yamungu alitaka kuongeza fedha yake kuokoa jahazi, lakini Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Orest Mushi, alianzisha mchango wa papo kwa hapo.


  Source: Mwananchi
   
 2. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Katika hali ya kuonyesha chuki na ubaguzi wa hali ya juu, DC wa Shinyanga Meja Bahati Matata amtimua katika jukwaa Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura. Jamani, tunaelekea wapi ?

  Pata habari kamili :
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MKUU wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Meja mstaafu Bahati Matala, nusura avuruge kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika wilayani hapa, baada ya kumtimua jukwaani Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura, hali iliyopingwa na wafuasi wa chama hicho.

  Sakata hilo lililotokea juzi saa 5:00 asubuhi kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya, Matala alipanda jukwaani na kuanza kuwatambulisha viongozi waliojumuika akiwamo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Masanje, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Eliza Bwana na Mwenyekiti wa halmashauri, Alfred Mhanganya.

  Matala baada ya kumwona diwani huyo akiwa amekaa na viongozi hao jukwaani, kwa kutumia kipaza alitangaza akimtaka Wambura kuondoka mara moja.

  “Bobson ondoka jukwaani mara moja,” alifoka Matala. Hatua hiyo iliwakasirisha watu wengi waliokuwa wamehudhuria na kuanza kuguna, hali ambayo ilitulizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Masanje ambaye alichukua kipaza sauti haraka kutoka kwa Matala, huku akimtaka diwani huyo kurejea mara moja jukwaani na kusalimia wananchi.

  “Bobson tafadhali rudi uwasalimie wananchi wako, sioni sababu ya kumfukuza diwani wa Chadema kwenye jukwaa hili, leo tunasherekea miaka 50 ya uhuru wakati mwaka 1961 tunajitawala, uhuru ulikuwa wa Watanzania wote siyo Chadema wala CCM, sherehe hizi ni za watu wote,” alisema Masanje huku akishangiliwa na wananchi.
  Licha ya Masanje kupinga uamuzi wa mkuu huyo wa wilaya, alirudia tena upya utambulisho wa madiwani wote akiwataka wasimame na kuwapungia mkono wananchi.

  “Waheshimiwa madiwani popote mlipo pamoja na Bobson simameni muwapungie mikono wananchi,” alisema Matala.Akizungumzia hatua hiyo, baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Wambura alisema alisikitishwa na kitendo cha mkuu wa wilaya kumfukuza jukwaani, ilhali maadhimisho hayo yalikuwa yanafanyika kwenye eneo lake na kwamba, atafikisha suala hilo kwa wananchi.

  Katika hatua nyingine, utoaji zawadi kwenye kada mbalimbali zilizoshiriki maadhimisho hayo nusura uingie dosari baada ya mwanamke mmoja, kuangua kilio mbele ya mgeni rasmi kutokana na kuchakachuliwa kwa zawadi yake ya Sh100,000 aliyoahidiwa kwa kushinda mbio za baiskeli upande wa wanawake.

  Kilio hicho kilianza baada ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kapteni mstaafu James Yamungu, kutangaza Sh50,000 iliyomfanya mwanamke huyo kupinga na kuangua kilio.Baada ya kuona hali hiyo Yamungu alitaka kuongeza fedha yake kuokoa jahazi, lakini Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Orest Mushi, alianzisha mchango wa papo kwa hapo.
  Habari hii imeandikwa na gazeti la Mwananchi.
  DC amtimua jukwaani diwani wa Chadema
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hao ndio wanaijenga CCM?!
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  E bwana kumbe bongo tuna madikiteta?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  ccm yajenga nchi
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Meja mstaafu ni mkuu wa wilaya na kapteni mstaafu ni mkuu wa mkoa na luteni mstaafu ni waziri. Ni mwendo wa amri kwa amri
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninawasiwasi mkubwa kuwa hizi zawadi za uDC na uRC wanapewa watu wasiostahili kabisa na kutofahamu majukumu yao. Haikuhitaji kwenda shule ili kuwa na busara kwenye hili. Inaonyesha jinsi wanavyowachukulia wapinzani ni wahalifu. Diwani anachaguliwa na anatambulika kikatiba, DC /RC sijajua wapo kwa mujibu upi.
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  DC = DoaChangu
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Habari za ndani ni kwamba Bobson ni maarufu sana hapa Kahama na alikuwa kaandaa maandamano ya kumpinga mkuu huyo wa Wilaya kwa kuchakachua mahindi ya msaada
   
 10. e

  ebrah JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  teh teh teh hajui moto wa nguvu ya uma huyo
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi vyeo vya Ukuu wa Mikoa na Wilaya ni byeo vya KISIASA hapa nchini kwetu au ni vyeo vya KI-UTUMISHI wa kiserikali kuhudumia wananchi wote bila kuendeleza misingi fulani fulani za kisiasa??????????

  Kwa mambo kama haya na yale yaliotokea kule Igunga, inabidi watu tufike mahala tuone sababu KUFANYA VYEO HIVI VIWE VYA KIUTUMISHI ZAIDI, watu kutuma maombi ya kazi kiushindani kama kazi nyinginezo ili tuondokane kabisa na hawa watu wenye kuwakera wananchi kiasi hiki.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  matala ni miongoni mwa ma dc wapumbavu sana.hana upeo hana akili..jimewahi kuganya naye kazi nikiwa buzwagi mine..he is bogus
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wakipata funzo kutoka kwa wananchi, tunaisingizia cdm! Mkuu wa wilaya mpumbavu namna hii wananchi wanaweza kumchukulia hatua gani wakati hawamfahamu wala hawajui alipowatokea zaidi ya kuambiwa tu ameteuliwa na rais. Tafakari...
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ccm zaidi ya uijuavyo
   
 15. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MaDC wengine bwana! Wanaendelea kucheza ngoma ya CCM ambayo mdundo wake ulishaisha siku nyingi.
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,939
  Trophy Points: 280
  Nadhani dawa iwe ileile aliyopewa Kimario kule Igunga ndio watajua wanapaswa kutenda kwa haki dhidi ya waajiri wao ambao ni wananchi na si CCM
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nashindwa kuelewa hawa Ma-DC wanafanya kazi kwa maslahi ya nani kwa kweli,wako pale kulinda maslahi ya chama au wananchi,kisa nini mpaka amfukuze diwani wa CDM...huu ni uchafu wa wazi na udhalilishaji ambao nilitegemea DC akamatwe haojiwe kwanini anamdhalilisha kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wakati yeye kateuliwa na Raisi tena kimagumashi magumashi....Viongozi wa CCM wanapaswa kufahamu ipo siku watatoka madarakani,na wanayoyafanya kwa wananchi sasa watafanyiwa pia baada ya chama kingine kuingia madarakani..tuwe na nidhamu kabla atujapewa nidhamu kwa lazima...Huyu mkuu wa wilaya anahitaji kipigo cha kumnyoosha adabu...
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hayo ndiyo yanayowastahili madiwani wasiojua protokali!
   
 19. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Nikitoka Igunga nakuja hapo.
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Protokali ipi unazungumzia wakati Diwani wa peopleez ndiye mwenyeji? Pumbav zenu!
   
Loading...