DC aumbuka kumfukuza diwani wa CHADEMA jukwaani

Huyo jamaa analidharirisha jeshi hata kama ni mstaafu. Askari aliyestaafu na cheo cha Major anafanya mambo kama kihiyo! Alikwenda kozi za uongozi kweli? Hivi vyeo vya maDC na RC kama havitaondolewa ktk Katiba mpya basi viwekewe vigezo na sifa. Nimemkumbuka mzee Mkapa,maDC wapuuzi kama huyu alikua anafuta uteuzi wao.

Yaani hawa MADC SIJUI WAMEOKOTWA WAPI!!! Jana alikuwa DC Igunga, leo Kahama!!! Kweli wadau tujiandae tu vizuri kwa katiba mpya ndo mkombozi pekee wa hawa watu wanaojifanya mangi meza!!!!!!!!??????????

Sijui kuna mantiki gani ya kuwaweka maafisa wastaafu wa jeshi kwenye sehemu hizo..... Maana wanateuliwa na raisi, tena hii list ni ndefu tunao maofisa ubalozi, wakurugenzi, wenyeviti wa bodi.........

Meja mstaafu ni mkuu wa wilaya na kapteni mstaafu ni mkuu wa mkoa na luteni mstaafu ni waziri. Ni mwendo wa amri kwa amri

Unategemea nini kutoka kwa maDC?mtu anaamka asubuhi nyumbani anakutana na barua imetoka kwa JK,inasema hivi "swaiba mambo vipi nimeona nikupe ka ulaji kidogo utakuwa DC wa SHY" simple like that huu upuuzi wa vyeo vya PROMOTION UNATAKIWA UFE HATUUTAKI.

huyu angefanyiwa ile kitu aliyofanyiwa dc wa igunga. naona hawa watu bado hawajaijifunza

Wakipata funzo kutoka kwa wananchi, tunaisingizia cdm! Mkuu wa wilaya mpumbavu namna hii wananchi wanaweza kumchukulia hatua gani wakati hawamfahamu wala hawajui alipowatokea zaidi ya kuambiwa tu ameteuliwa na rais. Tafakari...

Hapo kwenye red! Na tuombe huyo DC awe wa dini nyingine ila akiwa wa dini ile hukawii kusikia viongozi wa dini husika wakitoa matamko kwamba anaonewa kwa dini yake!

Huu ni uthibitisho mwingine wa kuongozwa na watu ambao hawajui wanachokifanya. Badala ya kusimamia sheria na kuhimiza amani na mshikamano hata baada ya miaka 50 ya uhuru, yeye anabomoa. Huyu ni adui namba moja wa Utanzania!
Hafai kuwa DC , wananchi wamkatae kwani anajenga chuki zisizo na sababu miongoni mwa wananchi.

Tunao viongozi wengi tu wa namna hii. Mtu kufikiria kwamba, chama chake ndiyo kilikuwa miliki wa maadhimisho ya kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ni hatari sana. Kizuri huyo DC yeye ameamua kujionyesha hadharani kwa umma. Hongereni watoa hii kwa kazi nzuri. Maana kuwafahamu watu wa tabia kama ya huyo DC ni muhimu sana katika siasa zetu za leo, maana tunahitaji tija na kwa huyo bwana, hana nafasi kabisa kuwa kwenye timu ya watu watakaohamasisha tija ndani ya taifa letu, bali kubomoa tu.

MKUU wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Meja mstaafu Bahati Matala, nusura avuruge kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika wilayani hapa, baada ya kumtimua jukwaani Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura, hali iliyopingwa na wafuasi wa chama hicho.

Matala baada ya kumwona diwani huyo akiwa amekaa na viongozi hao jukwaani, kwa kutumia kipaza alitangaza akimtaka Wambura kuondoka mara moja. "Bobson ondoka jukwaani mara moja," alifoka Matala. Hatua hiyo iliwakasirisha watu wengi waliokuwa wamehudhuria na kuanza kuguna, hali ambayo ilitulizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Masanje ambaye alichukua kipaza sauti haraka kutoka kwa Matala, huku akimtaka diwani huyo kurejea mara moja jukwaani na kusalimia wananchi.

kuna mdau mmoja aliuliza humu ndani, wakuu wa wilaya/mikoa huapa nini viwanja vya ikulu?
baadhi ya majibu yaliyotolewa ni sehemu ya yaliyotokea huko Kahama.

my not. Tupambane kuhakikisha nafasi hizi zinafutwa kwani zimevaa kofia ya utendaji wa serikali wakati chupi zao zimejaa harufu ya CCM

MKUU wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Meja mstaafu Bahati Matala, nusura avuruge kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika wilayani hapa, baada ya kumtimua jukwaani Diwani wa Kata ya Majengo (Chadema), Bobson Wambura, hali iliyopingwa na wafuasi wa chama hicho. Sakata hilo lililotokea juzi saa 5:00 asubuhi kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya, Matala alipanda jukwaani na kuanza kuwatambulisha viongozi waliojumuika akiwamo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Masanje, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri, Eliza Bwana na Mwenyekiti wa halmashauri, Alfred Mhanganya.

Matala baada ya kumwona diwani huyo akiwa amekaa na viongozi hao jukwaani, kwa kutumia kipaza alitangaza akimtaka Wambura kuondoka mara moja. “Bobson ondoka jukwaani mara moja,” alifoka Matala. Hatua hiyo iliwakasirisha watu wengi waliokuwa wamehudhuria na kuanza kuguna, hali ambayo ilitulizwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Masanje ambaye alichukua kipaza sauti haraka kutoka kwa Matala, huku akimtaka diwani huyo kurejea mara moja jukwaani na kusalimia wananchi.

“Bobson tafadhali rudi uwasalimie wananchi wako, sioni sababu ya kumfukuza diwani wa Chadema kwenye jukwaa hili, leo tunasherekea miaka 50 ya uhuru wakati mwaka 1961 tunajitawala, uhuru ulikuwa wa Watanzania wote siyo Chadema wala CCM, sherehe hizi ni za watu wote,” alisema Masanje huku akishangiliwa na wananchi. Licha ya Masanje kupinga uamuzi wa mkuu huyo wa wilaya, alirudia tena upya utambulisho wa madiwani wote akiwataka wasimame na kuwapungia mkono wananchi.

“Waheshimiwa madiwani popote mlipo pamoja na Bobson simameni muwapungie mikono wananchi,” alisema Matala.Akizungumzia hatua hiyo, baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Wambura alisema alisikitishwa na kitendo cha mkuu wa wilaya kumfukuza jukwaani, ilhali maadhimisho hayo yalikuwa yanafanyika kwenye eneo lake na kwamba, atafikisha suala hilo kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, utoaji zawadi kwenye kada mbalimbali zilizoshiriki maadhimisho hayo nusura uingie dosari baada ya mwanamke mmoja, kuangua kilio mbele ya mgeni rasmi kutokana na kuchakachuliwa kwa zawadi yake ya Sh100,000 aliyoahidiwa kwa kushinda mbio za baiskeli upande wa wanawake.

Kilio hicho kilianza baada ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kapteni mstaafu James Yamungu, kutangaza Sh50,000 iliyomfanya mwanamke huyo kupinga na kuangua kilio.Baada ya kuona hali hiyo Yamungu alitaka kuongeza fedha yake kuokoa jahazi, lakini Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Orest Mushi, alianzisha mchango wa papo kwa hapo.

Source: Mwananchi

huyo Dc angefanyiwa kama yule mwenzake wa igunga, kwanini wanashindwa kusoma alama za nyakati.? Anatoa tu amri anadhani jeshi

huyu DC anakumbuka shuka kumekucha aibu ndio hayo ya katiba hao wote nikutokana na katiba endapo tutafanikiwa kuibadili yote yataisha maana sioni haja ya DC kuchanguliwa na rais

Back
Top Bottom