thebusdriverclassc
Senior Member
- Jan 16, 2014
- 146
- 66
Habarini za mchana wadau, natumai mpo salama mkiendelea kutimiza majukumu yenu ya kila siku. Niliwahi kuja na wazo biashara siku zilizopita. Biashara ya M-pesa, nashukuru kwani nilipata michango ya wadau wengi, ikieleza faida na hasara za hii biashara.
Mimi binafsi kutokana na michango niliyopata kwenu, bado nitaifanya sababu naamini "something is better than nothing" hata kama ni sh.100.
Sasa nirudi kwenye mada, wazo ambalo nimelipata sambamba na hilo ni kufungua kituo cha kuwaangalia na kuwahudumia watoto kipindi wazazi hawapo majumbani, (mchana-daycare centre). Nipo Arusha, mimi ni muajiriwa pamoja na mke wangu na hii ni kutafuta kipato cha ziada.
Naomba yeyote mwenye uzoefu, anayefanya au anayeweza kunifanyia mchanganuo wa hiki ninachotaka kufanya anisaidie, gharama na mahitaji muhimu katika kufanikisha hili. Nina mtaji wa million 1.5.
Asanteni sana.