Mnyenz
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 2,041
- 6,289
Jamani ndugu zetu wa dawasco jiji letu pendwa la Dar limezidiwa na baridi hivyo nina ombi maalumu, tunaomba kuanzia mida ya saa kumi alfajiri mpaka saa nne asbuhi mabomba yawe yanatoa maji moto, ili wateja wenu tuoge kwa raha, kwanza ninaamini hata matumizi ya maji yataongezeka na nyinyi mtapata hela ya kutosha ya bill, maana siku hizi mtu akiingia kuoga Anatoka fasta, ila mkiweka maji moto hata lunch time nitakua natoroka job ili nikaoge.