kipoke KIPOKE
Member
- Apr 20, 2015
- 54
- 9
Nichukue fulsa hii kuelezea huduma tunazopatiwa na DAWASCO kwanza kuhusu malipo wameintroduce malipo kulipa kwa mtandao ukienda kuuliza kwenye max malipo unaambiwa hudaiwi ila wakipita jamaa zetu wakata maji wanakutajia pesa tofauti na mashine za max malipo haya hilo tuliache tuje kwenye swala zima la customer care jamaa hawana customer care kabisa wanakuja wanakata maji bila hata kuwasiliana na anayetumia maji kumekua na utaratibu wa kutuma sms kwa wenye nyumba kuhusu bill za maji huo ni utaratibu mzuri lakini hawakufanyia utafiti wakati wanauimpliment walichukua namba za wenye nyumba na sio watumiaji maji ambao ndio walipa bill nashukuru wamejitahidi kupata customer care mzuri pale magomeni anayejitahidi kufukia madhambi ya ndugu zake hawa wa field ambao wanafanya kampuni ionekane mbaya haya sasa turudi kwenye majipu ukikatiwa maji ''unapigwa faini'' tena siku hizi ni 30,000/=sijui wamepata wapi huu utaratibu na kibaya zaidi bill tunalipa max malipo faini unalipa benki kwa nini organization moja lakini malipo yanaenda account tofauti wahusika angalieni hilo jipu mtu anadaiwa 16,000/ faini elfu 30,000/=na deni lenyewe ni la mwezi mmoja wa nyuma .
Jipu jingine ni kuhusu utengenezaji wa mabomba kumekua na ujenzi wa miundo mbinu ya mtandao, huku kwetu kampuni za simu zimepita na wamekata mabomba tukatoa taarifa baada ya siku jamaa wakaja baada ya kuangalia wananiambia gharama ya kutengeneza ni tshs 110,000/=bila hiyo hatutengenezi,nikalipa wakanunua vifaa wakatengeneza sasa nani wa kulipia gharama hizo please jirekebisheni
mkitaka maelezo zaidi ntapatikana