DAWASA wabadili siku ya kusoma Mita za Maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,745
11,872
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wateja wake wa Jiji la Dar es Salaam na miji ya Pwani juu ya mabadiliko ya usomaji wa mita za maji na upokeaji wa bili za maji uliofanywa hivi karibuni.

Hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya usomaji wa mita yaliyofanywa na Mamlaka kutoka tarehe 1 hadi 15 kwenda tarehe 20 hadi 30 ya kila mwezi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juu ya mabadiliko hayo, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Pwani wamepongeza mabadiliko hayo na kusema yamefanyika wakati muafaka na yataleta tija kwa Mamlaka na Wananchi kwa ujumla.

“Tunaishukuru DAWASA kwa mabadiliko haya ya usomaji mita kwa tarehe za mwisho wa mwezi, sisi wananchi tulishasema sana kuhusu kuletewa bili tarehe tofauti tofauti wakati vipato vyetu vinatofautiana” alisema ndugu Ramadhan Abdul mkazi wa Kinondoni Shamba.

Zakia Mrisho mkazi wa kitongoji cha Sanze, wikaya ya Kisarawe anasema mabadiliko hayo yamewasaidia sana wananchi wanaotegemea vipato vyao mwisho wa mwezi.

“mfano sisi watumishi wa umma kipato chetu kikuu ni mshahara unalipwa mwisho wa mwezi, vile DAWASA walikuwa wanatusomea bili na kutuma message muda wowote halikuwa jambo zuri, tuliishia kugombana nao na wakati mwingine kuleteana vitisho mbalimbali. Lakini kwa mabadiliko haya tunajua wamesikia kilio chetu na wakaamua kujirekebisha” alisema bi Zakia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara na huduma kwa wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda amesema mabadiliko hayo yaliyofanywa na Mamlaka yalifanyiwa utafiti wa kina na shirikishi yaliyolenga kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira.

"Mara kwa mara huwa tunatenga muda wa kuongea na wateja wetu,hivyo mabadiliko haya ni miongoni mwa sauti za wateja wetu walizotushauri juu ya uboreshaji wa huduma zetu ili kuweza kuwafikia wengi zaidi" alisema Bibi Lwabulinda.

1621512929995.png
1621512948405.png
 
Kikubwa wakija kusoma hizo meter wajitahidi na wenyeji wawepo sio kutuvizia hatupo.
Tafadhali, Kwa sisi tunaolipa bili kwenye mitandao tunaomba bili zije kuanzia tarehe 25 ya mwezi sio tarehe za katikati, maana deadline inakuwa siku 7
 
Kikubwa wakija kusoma hizo meter wajitahidi na wenyeji wawepo sio kutuvizia hatupo.
Dawasa wanapaswa wa train wasoma mita, wajifunze customcare, wengi wao sio wastaarabu na wasumbufu, hawana maadili,
wanasababisha serikali kupoteza mapato bure bila sababu ya msingi.

wanasoma mita bila kumtaarifu mteja ni kosa, lazima mteja ataarifillwe kwa kupigiwa simu kuwa wanankuja kusoma mita.
 
Hivi Dawasa hamtoi maelekezo kwa watumishi wenu wasoma mita mtaani?

Mbona tunamsikia waziri Aweso akisema wasoma mita wasome mbele ya wenye mita au family members?

Kwanini wasoma mita hawazingatii hayo maelekezo ?

Kwanini wana wadharau family members?

Wakiwauliza vipi mnasoma mita nije kuona wanakataa.

Tena wanaaambia Kwani bill itatoka kwa jina lako? Haikuhusu!

Meneja wa dawasa Tegeta na Kawe ongeeni na watumishi wenu wanaosoma mita, hawana customer care though hili ni tatizo kwa watumishi wa dawasa wengi hata Viongozi wao ,
Kuwaona wananchi kama wateja na wateja kuwa wafalme kwao haipo!

Wanataka wananchi wawanyenyekee.

Wakali wakali tu na majibu ya mkato mkato.!

Kuwa mtumishi wa Umma siyo kuwa Boss kwa wale unaowatumikia!
 
Mita za luku za maji zimeishia wapi? Ujanja ujanja tu Ili kupoteza mapato na kubambikia bili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom