Dawa ya Wizi wa Mitihani IPO

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Waungwana,

Leo nimeona demonstration ya teknolojia itakayowezesha kukomesha wizi wa mitihani ya kitaifa ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Kitaaluma. Teknolojia hii inafaa hata kwa kuzuia nyaraka mbali mbali zilizoko kwenye tarakinishi (soma "computer") zisionekane na watu wasiotakiwa/wasiohusika.

Swali la Kwanza: Je, Serikali iko tayari kukubali teknolojia hii itumike kudhibiti wizi huo wa mitihani, ili Watanzania watakaohitimu masomo yao na kupata vyeti wawe wamehitimu kwa kustahili, na si kwa njia wizi?

Naomba jibu.

Swali la Pili: Je, iwapo Serikali itakuwa tayari kukubali teknolojia hii itumike, nimwone nani na kwenye taasisi gani, ili tuanze majadiliano ya kusonga mbele?

./Mwana wa Haki
 
Majibu ya maswali yako yanaweza kupatikana kutoka kwa serikali. Nakushauri peleka software yako kwenye wizara husika, ielezee faida zake na namna gani inafaa kutumika, hapo ndipo panaweza kupatikana jibu sahihi. Kwamba tunaweza kukuambia serikali inaweza kukubali wakati hata sisi hatujaona ni kitu gani unacho itakuwa ni kudanganyana na kupoteza muda.
 
Back
Top Bottom