Dawa ya Wabunge kuwajibika hii hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya Wabunge kuwajibika hii hapa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Indume Yene, Jul 7, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Watanzania tumekuwa tukipigwa danadana na vyenga kuhusu maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu. wengi wa wabunge wetu (Collectively) wamekuwa wanatoa ahadi bila responsibility yoyote. Wengi wao wamekuwa wakijisahau sana na hata wengine kusahau majimbo yao yanavyofanana baada ya kukaa mijini kwa muda mrefu.

  Wabunge wengine wamediriki hata kutoa maoni yao binafsi bungeni kinyume na constituents wao. Wamekuwa wakijiamini sana kufanya mambo kinyume na yale waliyotumwa bungeni. Lakini inapofika au inapokaribia wakati wa uchaguzi ndipo utaona wanaanza kuwajibika, kuuliza maswali ya msingi, kutoa hoja zilizokwenda shule. Ziara za majimboni haziishi, mawaziri watatafutwa at least wawe na ziara hata ya siku moja majimboni mwao ili mradi tu kumdanganya Mdangayika kuwa mbunge anafanya kazi.

  Hivyo utagundua kuwa dawa ya wabunge wa aina hii ni uchaguzi. Na kama hii ndiyo dawa mie nilikuwa nina hoja au ushauri kuwa muda wa ubunge kutumika upungue kutoka miaka 5 hadi 2 au 3 ili hawa wabunge wawajibike vizuri na kuhakikisha kuwa kuna maendeleo fulani ndani ya miaka hiyo aidha 2 au 3. Na kama hawezi kuleta maendeleo kwa kipindi hicho basi kuna wengine watakuwa na nafasi hiyo.

  Naamini hii HOJA itaweza kupingwa kwa madai ya fedha za uchaguzi zitatoka wapi kama uchaguzi utafanya every 3 yrs. Kama kutakuwa na maendeleo katika majimbo naamini hata kodi inaweza kukusanywa vizuri ethically. Vilevile wananchi wataweza ku-compare hayo maendeleo pamoja na costs za uchaguzi. Naamini vile vile HOJA yangu itakuwa na mapungufu lakini huo ni mtazamo wangu tu, na wewe vilevile unaweza changia katika hili.

  Naamini muda ukipunguzwa, wabunge watakuwa very much responsible kwa wananchi. Mfano mnauona hasa kupindi hiki. Hata wabunge wa SISIEMU wanadiriki kukomalia chao. Kisa wanajua uchaguzi hauko mbali.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Miye maoni yangu ni kwamba kipindi cha vyama kuongoza serikali kiwe miaka minne, nikimaanisha Rais na wabunge wawe katika nafasi zao kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine kufanyika.

  Miaka mitatu mimi naona ni michache sana kuweza kutekeleza baadhi ya sera na kuweza kupima utekelezaji huo. Minne is just average na pia kuona kuwa inatumika pahala pengine duniani.

  SteveD.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Tupunguze Marupurupu Ya Ubunge, Ili Yeyote Anayewania Ubunge Kwa Nia Ya Ku-make Money Asiende Huko, Waende Watu Makini Tu. Ukiona Wahindi Wanagombea Ubunge Kwa Kasi Ujue Hiyo Ni Sawa Na Business
   
Loading...