Nimejikataza kuuamini msemo huu uliyosheheni midomoni mwa wanajamii .
Nalazimika niamini waanzilishi wa msemo huo wakati wanauanzisha kama hawakua na kilevi vichwani , Basi hawakufikiri vya kutosha .
Ni kama walitumia 30% ya uwezo wao .
Mke awe mbogo na mme awe mbogo!
Matokeo yake?
Mwalimu yuko mbogo na mwanafunzi mbogo!
Suluhisho lipo?
Boss amefyum na staff amefyum!
Ufanisi wake?
Baba ako hot na mtoto hot ! Baba V mbogo! Erickb52 mbogo!
Tarajio lake?
What next ?
Mimi nitaendelea kuamini dawa ya moto ni fridge (baridi)
Aidha hapa jamvi incase yupo aaminie "dawa ya moto ni moto!"
Mlango u'wazi anipe ushawishi ambatano vigezo , nione kama naweza badili maono dhidi ya semi hii .