Dawa ya malaria yatumika kurembesha nywele.....

Dawa ya malaria yatumika kurembesha nywele.....

kabanga

Platinum Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
37,649
Reaction score
19,042
Waungwana hii habari nimeikuta katika gazeti la mwananchi, hebu tupitie.......

Tabia ya kutumia vitu vyenye kemikali bila ya ushauri wa kitaalamu imeendelea kujijenga miongoni mwa Watanzania, ambapo sasa dawa ya malaria aina ya Metakelfin inatumika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.
images


Matumizi hayo hatari ya Metakelfin yamegundulika huku kukiwa na taarifa za maji ya betri za magari, kutumika kama malighafi ya kutengeneza mkorogo unaotumiwa na baadhi ya wanawake kuchubua ngozi zao.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini dawa ya malaria aina ya Metakelfin ni mojawapo ya kemikali inayotumika kienyeji katika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.

Kwa mujibu wa mtafiti Issai Sen’genge, Metakelfin ni miongoni mwa kemikali inayotumika kutengeneza mchanganyiko wa kulainisha na kurefusha nywele.

Alisema idadi kubwa ya waliohojiwa, waliitaja dawa hiyo ya malaria kuchanganywa ndani ya dawa nyingine za nywele ili kupata mchanganyiko ambao husaidia kurembesha nywele.

“Swali lilikuwa kama kuna vitu vinavyotumika katika kutengeneza mchanganyiko wa kupaka kwenye ngozi au nywele, waliohojiwa walikiri kuchanganya, Metakelfin, Jik, maji ya betri na kemikali nyingine,” anasema Seng’enge.

Kwa upande wake, Maria Kimiro ambaye ni mmiliki wa saluni ya wanawake iliyopo Makongo jijini Dar es Salaam, alikiri kusikia matumizi ya vidonge katika vipodozi lakini hana uhakika wa aina ya dawa hizo.

“Nakumbuka kuna mtu nimeshawahi kumsikia anazungumzia vidonge katika masuala ya vipodozi, lakini sina uhakika kama ndiyo hiyo Metakelfin au vidonge vingine,”anasema Kimiro.

Asha Rashidi mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam, alikiri kuwa katika kutafuta urembo wanawake wanatumia vitu mbalimbali hata vinavyohatarisha maisha ili mradi kutimiza azma yao.

Anasema kuwa hali hiyo mara kwa mara imekuwa ikisababishwa na kuiga au kusikia kutoka kwa wengine bila kufikiria madhara ya ambacho anatarajia kukifanya.

“Binafsi sijawahi kutumia hiyo Metakelfin kwa kuwa nafahamu ni dawa ya malaria lakini naamini kuna watu ambao wanaweza kuichakachua kwa namna wanavyoweza wakidhani kwamba inaweza kuwa na matokeo mazuri kwenye ngozi au nywele,” alisema.




karibuni tujadili....
 
Kumbe tunalalamika dawa hamna mahospitalini wengine wanatengenezea maurembo ya nywele mbombo ngafu!
 
^^
Hatari sana, hivi kuna wanawake hawatumii dawa za nywele kweli?
^^
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom