VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.
Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta,Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.
Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam