Dawa ya kuwang'oa ccm ni maandamano kama tunisia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya kuwang'oa ccm ni maandamano kama tunisia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jan 22, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Wana JF na Watanzania wenzangu,

  Naandika kwa uchungu sana topic hii. Kwamba hapa tulipofikia sasa lazima Watanzania TUSEME ENOUGH IS ENOUGH na tuchukue hatua kama ndugu zetu wa Tunisia walivyoamua juzi kwa KUFANYA MAANDAMANO NCHI NZIMA KUPINGA UTAWALA WA KIFISADI NA KIUONEVU WA DIKTETA BEN ALI AMBAYE KWA SASA AMEIKIMBIA NCHI.

  Tanzania ya sasa ilipofikia hakuna tofauti na yale yaliyokuwa yakifanyika Tunisia. Kwamba DIKTETA BEN ALI alikuwa ameigeuza nchi kuwa ni sehemu yake BIASHARA na kujitajirisha. Aliingia kwa mbwembwe nyingi huku akisaidiana na Mkewe na kuanzisha sera ya ubinafishaji. Kwa kutumia sera hii aliweza kubinafsisha na kuuza Mashirika ya umma na Makampuni ya Serikali HUKU YEYE NA MKEWE AIDHA WAKIJIUZIA AU KUCHUKUA HISA KUBWA KWENYE MASHIRIKA AU MAKAMPUNI HAYO.Kama alivyofanya MKAPA na vigogo wenzake akiwa madarakani.

  Hali hii ilipelekea hali ya uchumi wa nchi kudorora na hivo kupelekea hali za kimaisha na kiuchumi za Wananchi wengi wa Tunisia kuwa ngumu sana! Kupanda kwa gharama za maisha na ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu na vyuo vya kati. Ukosefu wa ajira miongoni mwa wa TUNISIA hasa graduates uliwalazimisha kuanza biashara za kubangaiza ikiwemo umachinga!.

  Ni kijana mhitimu wa chuo kikuu(graduate)aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza mboga za majani mitaani ndiye aliyewasha MOTO WA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA hatimaye kupelekea kung'olewa kwa Dikteta Ben Ali. Graduate huyu tayari ni marehemu kwa sasa LAKINI YEYE ATABAKIA KUWA SHUJAA(HERO)KATIKA MAISHA YA WA TUNISIA WOTE KWA MAANA YEYE NDIYE AMEKUWA MWANZILISHI WA UKOMBOZI WA NCHI NZIMA. Habari zinasema Polisi walimvamia mitaani akiuza mboga zake na kumunyang'anya bidhaa na meza yake. Uamuzi aliochukua ilikuwa KUJIUA kupinga manyanyaso ya polisi wa Ben Ali. Huo ukawa ndiyo mwanzo wa maandanano na mapambano na polisi.

  Ukiangalia kwa undani utagundua kwamba yale yaliyotukia TUNISIA na yanayotukia TANZANIA kwa sasa hakuna tofauti. CCM hawana tofauti na chama cha Ben Ali kinachoitwa CDR(Constitutional Democratic Rally). Kama sera za Ubinafsishaji CCM awamu ya Mkapa walitia fora na wameendelea kutia fora kwa KUBINAFSISHA KILA kitu.Ilifikia mahali mpaka wakaanza kubezwa kuwa watabinafsisha mpaka magereza! Ukosefu wa ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu inatisha.Hali za maisha kwa Watanzania zinazidi kuwa ngumu kila siku iendayo kwa Mungu. Bei ya Umeme JUU,bei ya PETROLI na DIZELI iko juu. THAMANI YA SHILINGI inazidi kuporomoka!! CCM iko likizo inakula kuku!

  Serikali ya CCM imeshindwa kutatua kero hata moja kati ya zote hizi kwa kisingizio kuwa haina pesa. Wakti serikali ikidai haina pesa tunashuhudia Tshs.Bilioni 94/- tayari zinafanyiwa mchakato wa kulipwa kwa Kampuni hewa ya DOWANS tena kwa nguvu au lazima. CCM wameshindwa KUJALI AU KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANANCHI AMBAO NDIYO WENYE FEDHA kwa maana ya WALIPA KODI. Hii ni dharau kwa WANANCHI waliowapa ridhaa ya kuwaongoza. Huu ni uhuni!

  Kama hili la DOWANS halitoshi CCM vilevile wameziba masikio kwa makusudi kuhusiana na KUPANDA KWA GHARAMA ZA UMEME. Serikali imetia pamba masikioni kana kwamba haisikii wala haielewi kuwa KUPANDISHA KWA GHARAMA ZA UMEME KWA 18% kutapandisha gharama za kila kitu kwa maana umeme ndiyo chanzo cha uzalishaji wa bidhaa kwa maana ya vyakula,mavazi,vipuri,vifaa vya nyumbani n.k vyote vinatoka viwandani.

  Kuna hili la MAUAJI YA WATU 3 WASIOKUWA NA HATIA HUKO ARUSHA. CCM kupitia CC yao hawakutoa tamko lenye kutoa mwelekeo wa kumaliza mgogoro huo!. Badala yake wametumia ubabe na udikteta ule ule wa kusema anayeona uchaguzi haukuwa halali aende mahakamani. Hii ni jeuri ya chama cha CCM! Kwa CCM watu kupoteza maisha kwa mgogoro huo ni sawa tu maana walishinda kihalali. This is purely dictatorship ruling.

  Kwa kuhitimisha hebu niseme hivi.Kwama CCM kinathibitisha kuwa kimegeuka kuwa chama cha KIDIKTETA. Kwamba CCM kwa sasa hakitaki kusikia MAONI wala USHAURI kutoks kwa VIONGOZI,WANACHAMA na WANANCHI kwa ujumla! Inashangaza CCM kupitisha uamuzi wa kuwalipa Kampuni hewa ya Dowans wakti kuna Mawaziri ndani ya CCM wameshauri Dowans wasilipwe! Kuna vijana wa CCM-UVCCM wametoa tamko kuhusu Dowans kuwa wasilipwe! CCM wamepuuza maoni na ushauri huo. M/kiti Kikwete anajifanya kuweka pamba masikioni wakti ukweli wote anaujua kuhusu Dowans.

  Kitu ambacho ni dhahiri hapa ni kwamba CCM WALITUMIA MABILIONI YA SHILINGI WAKTI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2010. KWAMBA WALIKOPA AU WALIFADHILIWA HIYO PESA NA MTU KAMA ROSTAM AZIZ-RA. Kwa hiyo wanachofanya kwa sasa ni kutafuta PESA KWA NGUVU HATA KAMA NI KWA KUIBA,KUUA,KUDHULUMU au KUWABEBESHA MZIGO WATANZANIA ili wawalipe waliowakopesha au kuwafadhili kwenye Uchaguzi Mkuu. Hivi unafikiri gharama ya zile Helikopta 2 zilizokuwa zinamsafirisha Dikteta Kiwete wakti wa kampeni zilitoka wapi???Yale mabango yaliyotapakaa kila kona ya nchi hii nani aliyagharamia???Ni wazi kuwa MALIPO YA DOWANS NI KULIPIA GHARAMA HIZO ZA CCM. Huo ndiyo ukweli.

  CCM wameshindwa kusoma alama za nyakati. Wameshindwa kupata somo kutoka TUNISIA. Kwa hili la DOWANS CCM wamejichimbia shimo jingine la kifo. Hizi Bilioni 94 zitawa-cost kisiasa huku mbeleni. It is gonna determine their political destiny. Kukataa ushauri,maoni,mawazo ya watu unaowaongoza ni tabia ya vijiserikali vya KIFISADI na KIDIKTETA. Hapa ndipo walipotufikisha CCM. Dawa yake ni kung'olewa kwa MAADAMANO YA KUSHINIKIZA NCHI NZIMA.

  Mungu ibariki Tanzania.

  Nawasilisha.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Usihangaike nauli wakati gari yenyewe ni ya bure.
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi ya democrasia uwezi fananisha na serikali ya Bin Ali, hapa tunatumia freedom of experession na ballot paper
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Ni serkali ya wezi
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,945
  Trophy Points: 280
  maisha yanapozidi kuwa magumu,gap linapozidi kua kubwa kati ya mwenye nacho na asiyekua nacho,gharama za maisha kupanda,uonevu na kutokua na usawa,maamuzi ya kutatanisha,mikataba mibovu, na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwa manufaa ya watu wachache itatufikisha huko..Ngoja tuangalie huu ukimya wa huyu bwana utatufikisha wapi!
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,237
  Trophy Points: 280
  Wazo lako nizuri ila je ninani wakumfunga paka kengere??
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />

  Ni ugumu wa maisha ndo utamfunga paka kengele! Kukosa matumaini ni jambo la hatari kweli kweli, kimshahara ni kile kile lakini bidhaa madukani zinashindana kupaa bei, huduma za jamii zinahama toka zero zinaelekea negative, haki haipatikani wala haitolewi kwa wakati; unategemea watu waendeleee kuimba Ndiyo mzee! Thubutu
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu ccm wajiandae kutia maji watanyolewa mda wowote akuna lisilowezekana chini ya jua limewezekana tunisia litawezekana tanzania
   
 9. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,945
  Trophy Points: 280
  Yule Mtunis hakulipua ikulu,hakuamuru watu watoke majumbani mwao,hakupigana na polisi wala kuhujumu chochote kilichowekwa kihalali na serikali yake dhalimu...baada ya kuona hana kimbilio na akiba yake ndogo aliyojiwekea kuvurugwa na waliojipa mamlaka aliamua kujilipua mwenyewe...na mchakato wote ukaanzia hapo...kwa hivyo hakuna kumvika paka kengele wala nini...muda ukifika huyo paka atavaa kengele mwenyewe....
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pls fafanua vzuri kunademocrasia ipi tanzania? Au upo nje ya tanzania. Hapa kunademocrasia ya kuwalinda mafisadi na ufisadi wao
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  thnx mkuu
   
 12. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni democrasia gani kama uchaguzi ni wa mizengwe, kura zina chakachuliwa, matokeo ya urais hayaruhusiwi 'kikatiba' kuhojiwa mahakamani, Rais anakuwa na madaraka ya kifalme au kisultani ambapo anateuwa kuanzia waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Majaji woote, Mahakimu, wakuu wa majeshi, Uaslama wa Taifa, Wakuu wa Mikoa, wilaya hadi mameneja wa asasi; hivi kuwa na mwanya wa kuwaweka washikaji wake woote na nafasi chache zilizobakia kuwapa wakuja ili kuwatupia changa la macho wananchi?
  Kikwete ana tofauti kweli na Ben Ali? Kwani kuna jambo gani asilolifanya na familia yake? Si hata kwenye Kampeni uliiona familia yake ilivyochangamkia kampeni ili 'Mzee' arudi ikulu kwa hali na mali huku familia yake ikitumia rasilimali za nchi kumfanyia kampeni? unaweza kutufafanulia jinsi Ridhwani alivyotajirika haraka namna hivi wakati ni kijana ambaye hana hata miaka kumi ya kazini? Mimi nasema Ben Ali anaweza kuwa na afadhali kidogo kuliko huyu wa hapa kwetu kama madudu yote anayofanya yataanikwa.
  Hivi nchi hii kuna 'Freedom of expression' kweli kama hata wabunge wa CHADEMA waliposusia hotuba ya Rais kusajili dukuduku lao la namna alivyoingia madarakani kwa njia za kihaini kupitia Tume na vyombo vya dola waliishia kutishwa, kutukanwa kubezwa na kukebehiwa na vyombo vya propaganda vya CCM? Si walitishiwa kunyimwa nafasi ya kuteuliwa kwenye kamati mbalimbali utadhani fedha za mishahara na marupurupu ya kamati hizo zinalipwa na ruzuku inayotoka CCM? Nasema hakuna tofauti na kwa Ben Ali, kwani hatukuona wote jinsi CCM ilivyotumia vyombo vya dola kugandamiza maandamano ya amani Arusha na kuwaacha mamia wakiwa na majeraha ya risasi na watatu wengine kupigwa risasi hadi kufa? Je hakuna unyanyasaji wa machinga hapa nchini? Kawaulize machinga popote mijini watakupa jibu. Ukweli ni kwamba machinga ni kundi lisilo na mtetezi, hunyang'anywa mali zao, kupigwa, kufunguliwa mashtaka na kuharibiwa mali na mabanda yao kwa visingizio vya kuweka miji safi; si ndivyo ilivyotokea kule Tunisia?
  Jambo moja ni wazi, nalo ni hakuna refu lisilo na ncha; kwa hiyo CCM inafikia ukingoni sasa na muda si mrefu itabaki kwenye historia kama chama kilichobadilika toka kuwa cha mapinduzi hadi utusitusi baada ya kutekwa na mafisadi na mabeberu wa ndani. Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Tanzania.
  A Luta Continua!
   
 13. S

  Shingo Senior Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Watanzania wameandamana polisi wakaua watu hadi Kikwete akakimbia nchi. Baada ya Kikwete kuondoka Pinda anachukua nchi halafu anamteua Lowassa kuwa Waziri Mkuu, Anamteua Rostam Aziz kuwa waziri wa fedha halafu anampa Andrew Chgne uspika. Nimrod Mkono anateuliwa waziri wa sheria na Katiba!!!!

  Hicho ndo kinachoendelea Tunisia, ndo maana maandamano na vurugu hazijaisha. Waandamanaji wanataka makkuadi wote wa Ben Ali watoke, ingawa bado wengi wameng'ang'ania!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Time will tell
   
 15. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu yote uliyosema ni haki na kweli kabisa, lakini ili tuweze kuwaiga wenzetu wa Tunisia inabidi mmoja wetu ajitolee kwanza kujichoma kwa petroli afe halafu ndio nchi ilipuke! sasa mwenzetu kama uko tayari kujitolea roho yako kwa ajili ya faida ya Watanzania wote basi mimi nakuunga mkono!

  Wala usijali kuhusu familia yako! hawatapata shida yoyote, nguvu ya umma itakuwa nyuma yao! wewe jitoe mhanga na ujilipue kwa Petroli hapo Jijini Dar halafu kazi iliyobakia tuachie sisi tumshuulikie JK & co.
   
 16. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  aaaah!drphone ni nani atakaye wanyoa ccm kama sio wewe?wote kwa ujumla wetu tunapaswa kujitoa kwa dhati tena bila woga kupambana na hawa mabaradhuli mpaka waikimbie nchi hii...Muda ndo huu lakini nashangaa jinsi tulivyo waoga..tutakubali mateso haya mpaka lini?
   
 17. B

  Bull JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Democrasia tuliyo nayo TZ uwezi fananisha na nchi za North africa au za kiarabu, mabadiliko TZ yataletwa kwa kutumia Sanduku la kura

  Tatizo lililopo ni kuwa hakuna chama cha upinzani kinachokubalika na kuamininiwa na wananchi wa Tanzania, either udniniudini au ukabila na wanamaamuzi ya kukurupuka,

  chama kama cha chadema unategemea kitaipeleka tanzania wapi? mbona viongozi wao ni vichekesho ?
   
 18. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Tanzania kwanza,

  Nashukru kwa maoni yako.

  Mimi nimetoa mfano tu wa vuguvugu lililoanzishwa na ndugu zetu wa Tunisia kupinga utawala wa Serikali dhalimu ya Rais Ben Ali aliyeondolewa madarakani. Kwamba kwa mfano huo wa Tunisia na sisi Watanzania tunaweza kuchukua uamzi kama huo wa kuishinikiza Serikali dhalimu ya CCM inayoongozwa na Rais Kiwete.

  TUNISIA MTU MMOJA AMEJILIPUA WATU WAKAINGIA MITAANI KUPINGA SERIKALI. TANZANIA WATU 3 WAMELIPULIWA NA POLISI HATUJACHUKUA HATUA ZOZOTE. SASA HAPA NANI ANAYEONEKANA KAPATA HASARA ZAIDI?

  Hatuwezi kufanya mambo kwa COPY AND PASTE method! Nina maana kuwa hatuwezi kufanya kila kitu kama mambo yalivyo Tunisia. Kuna mambo muhimu ambayo nimeyataja hapo juu ambayo YANATOSHA KABISA KUANZISHA VUGUVUGU LA MAANDAMANO YA KUISHINIKIZA SERIKALI YA CCM KUONDOKA MADARAKANI.

  Kuna mazingira ambayo tayari CCM wameshayatengeneza ambayo yanatosha kabisa kuwasha moto nchi nzima. Sikubaliani na wewe kuwa ili tuanze maandamano lazima mtu mmoja ajilipue. No! Tayari mpaka sasa hivi KUNA DAMU YA WATU 3 TAYARI IMESHAMWAGIKA KULE ARUSHA. HII ILIKUWA INATOSHA KABISA KUANZISHA MOVE YA NCHI NZIMA WATU KUANDAMANA KUPINGA UDHALIMU,UONEVU NA UKATILI WA SERIKALI YA CCM.

  Marehamu Mao-Tse-Tung mwanzilishi wa Taifa la CHINA aliwahi kusema wakti wa uhai wake kwamba, namnukuu:''CHECHE MOJA YAWEZA KUANZISHA MOTO MBUGANI.'' mwisho wa kunukuu. Hakika huu ni ukweli usiopingika hata katika mazingira halisi ya namna moto ambavyo huwa tunaona unateketeza misitu kwa misitu kwa cheche ndogo ya mchoma mkaa au mvuta sigara.

  Kwa hiyo hapa kwetu Tanzania cheche za kuwasha moto ziko kibao kama nilivyo ainisha huko mwanzo. Tatizo la Watanzania tulio wengi TUMEJAA UOGA (COWARDICE)WA KUSHINDWA KUTHUBUTU KUCHUKUA MAAMUZI MAZITO DHIDI YA SERIKALI KWA AJILI YA MSTAKABALI WA TAIFA LETU. Uoga huu ndiyo unaotutafuna.
   
 19. K

  Kipre tchetche JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali ilivyo sasahivi hakuna cha kuzuia
  Tena maandamano tayari milipuko ya
  hamasa kila kona ya nchi inarindima
  hakuna miezi miwili Tena utasikia tu.
   
 20. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :A S kiss:.....chini ya ccm kuna domokrasia na sio demokrasia.......
   
Loading...