Hali ilivyo sasahivi hakuna cha kuzuia
Tena maandamano tayari milipuko ya
hamasa kila kona ya nchi inarindima
hakuna miezi miwili Tena utasikia tu.
Kipre tchetche hakika umeronga.
Kama nilivosema hapo juu. CCM tayari wameshajiundia mazingira ya KUNG'OLEWA AT ANY COST.
Kuna hot ISSUES zinazowatesa CCM kwa sasa kama:
- KUBARIKI MALIPO YA DOWANS
- MAUAJI YA POLISI ARUSHA
- KUBARIKI KUPANDA KWA BEI YA UMEME
- UCHAKACHUAJI WA MATOKEO YA URAIS,2010 n.K.
Ni dhahiri kabisa kuwa haya mambo ni msumari wa moto kwa CCM. Kwanza kabisa ndani ya CCM wamesha jichanganya na hawaelewani wao kwa wao. Kila mtu anaropoka kivyake. Rais KIWETE(siyo Kikwete) maana kiwete siku zote ni mtegemea misaada na ombaomba. Ndivyo alivo Rais wa CCM. Inavoonekana Kiwete hana hata maamuzi ndani ya CCM. Yupoyupo tu anapelekwa kama ndege isiyokuwa na rubani! Hii si dalili nzuri ya Chama Makini kilichoshika Dola!!!
Nimewahi kusoma makala moja kwenye gazeti fulani ikisema KIWETE ameiweka nchi kwenye AUTO PILOT. Amelala usingizi huko ndege iliyokuwa ikisemwa na MKAPA kuwa inapaa iko anga za juu kwenye auto pilot! Inavoonekana KIWETE kama PILOT amewaachia wahudumu(STEWARDNESS)kuendesha hiyo ndege ya Serikali ya CCM. Bila shaka AJALI YA ANGUKO LAKE HAKUNA ATAKAYEPONA!!!
Tumesikia wahudumu kina MAKAMBA,TAMBWE HIZA,JOHN CHILIGATI, VUAI NAHODHA,IGP MWEMA na wengineo wakiachiwa kujaribu kuendesha ndege hii ya CCM iliyoko kwenye Auto pilot. Tumewasikia UVCCM wakibwabwaja eti wanawapinga Baba thao na mama thao wasilipe 94B/Tshs. kwa DOWANS. Mimi niliwashangaa kwa kweeri! Kama SItta na Mwakyembe wamepiga kelele mpaka POVU likawatoka lakini kwenye CC wakagwaya,UVCCM ni nani muwazuie Baba zenu?????
UVCCM subirini pigo la mwisho la shoka la UMSLOPAAGAS linaloitwa INKOSIKAZI. Hapo ndiyo utakuwa mwisho wa CCM.
Natoa ushauri wa bure kwa UVCCM wale wanao ona uchungu wa malipo ya DOWANS pamoja na Waheshimiwa Sitta na Mwakyembe waanze KUJITOA MAPEMA sana na kujiunga na KAMBI YA UPINZANI. The choice is theirs, either waende CHADEMA,NCCR-Mageuzi,TLP au chama chochote chenye NIA NJEMA NA NCHI HII!
Wasalaam.