Ni vizuri wachangiaji mada, hoja ktk JF tukawa na nidhamu wakati wa kuchangia. Mtu anapotoa shida, hoja au mada unakuta ana shida ya kweli, hivyo kwa kuwa humu kuna watu wengi kutoka sehemu mbalimbali, wenye taaluma mbalimbali na ambao wanaishi na jamii inayowazunguka ni dhahiri kuwa inawezekana jambo lillilotolewa humu akawepo mmoja wetu anayejua suluhisho la tatizo hata kama aliwahi kusoma sehemu, kuona au ndugu yake aliwahi kukwamuliwa katika tatizo kama hilo. Sasa utakuta wachangiaji wengi wanatoa michango yao kwa mizaha na kejeli. Siyo lengo au maana iliyokusudiwa humu ndani. Tuisaidie jamii ndugu zanguni.......