Dawa ya hili tatizo ni wanawake wenyewe

Dawa ya hili tatizo ni wanawake wenyewe

The activist

Senior Member
Joined
Aug 9, 2014
Posts
113
Reaction score
67
Habari wana jamvi,

Tatizo la wanawake kulalamika na kukimbia kwenye vyombo vya usalama na habari kuelezea namna ambavyo wamezalishwa na wanaume kisha kuwaachia majukumu ya kulea familia limekuwa likiongezeka kwa kasi sana hapa nchini.

Mi binafsi naamini watu wanapofanya tendo linalosababisha kupata mtoto ufahamu kabisaaa kitakachofuata.Nawauliza wanawake kama hauko vizuri kulea kwa nini ufanye ngono isiyo salama? Kwanini ukubali pekupeku? Ni wakati sasa wa wanawake kubadilika.

Wakichukua tahadhari hiyo kamwe tatizo litakuwa limekwisha. Nimeandika haya kufuatia taarifa ya habari ya ITV leo saa mbili kufuatia wanawake watano watu wazima kufika kwenye ofisi za ITV kuomba msaada baada ya waume zao kupotea.

Chonde chonde wanawake mjiongeze tumalize hilo tatizo hapa nchini.

Karibuni kwa majadiliano
 
Waambiwe hao wavulana wanaojiita wanaume, kiujumla hawafai kuitwa baba waitwe sperm donors... katika jamii zetu suala la matumizi ya njia za uzazi wa mpango bado na mbaya zaid wanawake wanajiachia wakiamini mimba ni one way ticket to ndoa kumbe neno ndoa ilikuwa chambo
 
Wa kwako ni sperm donor au mume?
 
Wanaume wote wanaotelekeza watoto kwa kujifanya sperm donor na kukimbia majukumu wakamatwe na kuasiwa si wanajifanya wanajua kukojolea Sana papuchi.
 
Wanaume wote wanaotelekeza watoto kwa kujifanya sperm donor na kukimbia majukumu wakamatwe na kuasiwa si wanajifanya wanajua kukojolea Sana papuchi.

It takes two to tango.

Kila mmoja anatakiwa awajibike kwa upande wake.

Mwanamke kama hayuko tayari kulea mtoto bila mwanaume basi asiendekeze ngono zembe.

Mwanaume naye kama hayuko tayari kuwajibika kwa matokeo ya matendo yake basi na awe mwangalifu kutokuendekeza ngono zembe.

Sasa, natambua kuwa kusema ni rahisi sana na zaidi kuliko kutenda. Lakini hilo halina maana kwamba watu waache kuwa waangalifu.
 
Ni kweli kila mmoja kwa upande wake Hao wamama wameachiwa majukumu ya kulea wenyewe wanaume wame sepa.Hivi na Hao kina wamama watelekeze watoto wa kimbie wawaache watoto. Hizi tabia za wanaume kuteleza familia na kukwepa majukumu linaongeza kwa wanaume suruali na Jina.
 
You are absolutely right. Two wrongs don't make a right.

Mimi ninaraghbika zaidi na uzuizi/ kinga ya matokeo ya hivyo na hapo ndo nikaingiza suala la uwajibikaji kabla ya matokeo.

Lakini matokeo yakishatokea hakuna jinsi tena. Kama mmoja kasepa aliyebaki ni lazima tu aubebe mzigo wa uwajibikaji peke yake (ingawa si haki).

Mzazi kuwajibika peke yake ni bora zaidi kuliko kutelekeza.
 
ni wanaume wenye ndoa ndo wanawakimbia family zao so wanawake wajrekebishe nini? USIPOZAA MGUMBA UKIZAA MALEZ HAMUYAWEZI.......HEY TENA MLETA MADA RUD KAJIPANGE UPYA:rockon:
 
kwa hiyo tuseme imeshatokea sasa,mtu anamimba..uwezo hana..so unamshauri mtu kama huyo atoe mimba au..
 
Wanaume bwana eti wanawake wabadilike, ina maana na nyie mnapotaka kufanya pekupeku hamkumbuki kwamba matokeo yake ni mimba? na baba wa mtoto utakuwa ni wewe?, na lazima utaletewa mzigo wako? Mnafurahisha kwaaaa kweliiiiii
 
Ni suala la kuwajibika tu, vinginevyo hakuna jinsi tutaendelea kulalamikiana tu....
 
Back
Top Bottom