Dawa ya Deni Kulipa

Dawa ya Deni Kulipa

Hmaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
346
Reaction score
86
Mdai: Hodi nyumbani!
Mtoto: Karibu!
Mdai: Hujambo?
Mtoto: Sijambo, shikamoo mgeni!
Mdai: Marahabaa, baba yako yupo?
Mtoto: Hayupo
Mdai: Sijamwona siku nyingi, kwani amekwenda wapi?
Mtoto: Subiri nikamuulize aniambie niseme amekwenda wapi!
Mdai: Ukamuulize nani?
Mtoto: Baba, kwa vile aliniachia maagizo kuwa mtu akija kumuulizia niseme hayupo lakini hakunipa maelezo niseme amekwenda wapi.
Palepale mzee nayedaiwa akajitokeza huku akivaa shati na kuanza kusema maneno ya kujikanyagakanyaga: mara ooh najisikia vibaya ndo maana nilikuwa nimejipumzisha, mara oh sijui nini. Kifupi alikamatwa. Kwa hiyo dawa ya deni kulipa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom