Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Baadhi ya dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi

  Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.

  Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.

  Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
  Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.

  Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.

  Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa.

  Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.

  Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.BBC Swahili - Habari - Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi
   
 2. Justin Dimee

  Justin Dimee JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 1,148
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Mbona wanasema uko dawa wamesha ipata au ni longo longo hawa wamarekan bna.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Mkuu Justin Dimee Wamarekani Uchumi wao umekufa sasa wanatanga tanga wanatafuta mbinu za kuweza kupata pesa hizi ni mbinu zao za kila siku wakishindwa huku wanatafuta kule Wamarekani ni kama vile sungura wa porini huwezi kuwakamata kirahisi .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...