Dawa/ jinsi ya kuangamiza mdudu aina ya konokono

Dawa/ jinsi ya kuangamiza mdudu aina ya konokono

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
10,161
Reaction score
11,559
Wakuu,

Ninaomba kujuzwa namna ya kumuondoa huyu mdudu aina ya KONOKONO kwenye mazingira ya nyumba yangu, hali ya hewa ya jiji la Arusha ni baridi na hata wakati wa kiangazi unaweza kuta mvua inanyesha kidogo muda wa alfajiri,sasa hali ya ubaridi inapotokea hawa wadudu huibuka kwa wingi na ni wakubwa sana mpaka inatia kinyaa.

Hawa wadudu wamefanya niache kabisa bustani za mboga kwa kuwa utawakuta wamelaliana kwenye hizo mboga na kufanya ukose hamu ya kula. Tafadhali anaejua jinsi ya kuangamiza wadudu hawa anajulishe.

Please wananikera sana
 
Labda uangalie kwa upande wa pili wa shilingi, niliona BBC kuna dada Mkenya anawafuga na kuuza kwa kitoweo (ingawa naongea tu..lakini looh...)
 
Mwaga chumvi kwenye njia zao, au yeyusha chumvi kwenye maji( chumvi iwe kwa wingi) wamwagilie.
 
Labda uangalie kwa upande wa pili wa shilingi, niliona BBC kuna dada Mkenya anawafuga na kuuza kwa kitoweo (ingawa naongea tu..lakini looh...)

Mh. hapana kabisa, hilo siwezi.
 
Mwaga chumvi kwenye njia zao, au yeyusha chumvi kwenye maji( chumvi iwe kwa wingi) wamwagilie.
Tatizo huwezi kujua wanajificha wapi, utaona tu wanaibuka na kupotea.
 
Fanya urafiki na wanaigeria, nakupa siku tatu ama wiki ukiwaona basi jua hao wametumwa, ni mboga ya heshima kama wahaya na senene. Sisi kulikuwa na vyura wanasumbua tukashauriwa kufanya urafiki na jamaa wa nchi jirani tunayotunishiana nayo misuli juu ya ziwa fulani. Basi tukazingatia ushauri, vyura walipotea ndani ya muda mfupi.
 
hahahaaa pole jmn maana ni kero balaa... Mimi walikuwa wanasumbua na niko Ar pia ila chumvi nilimwagaa mpk bustani zikaungua. Jijengee tabia ya kufanya famigesheni unaenda TFA unawaelezaa mazingra na wadudu wanaokusumbua dawa zipo za kupuliza unapewa mtu kwa wewe kumgharamia anakuja anapuliza dawa ndani ya nyumba, njee na mazingira yote utakavyo na kama unawatoto itabidi uwapeleke kwa bibi yao kama mimi nifanyavyo maana dawa ni kalii mnoo wee mwenyewe utalewa na kuanguka kwa kizunguzungu na kipnd kzuri ni cha jua na ukiipuliza kama mimi nakaa karibu mwaka mzima hakuna cha nzi,mbu nk na huyo konokono akitokea au hao nzi ni 1 mmoja wala hawakupi keroo maana kajua utamtoa,utammwagia kachumvi ama utamflash choonii akafie mbelee. Pia kama unavustani ya maua kama mie mwenye garden kubwa namweka mtu wa kazi hiyoo nina kijana anakuja kwa wiki mara 2 au tatu ama mara 1 inategemeana anakatia,anapga dawa na kutengeneza na saa zngine hata mara 2 kwa mwezi na mwisho wa mwezi nampa 30000 nachogharamia ni kununua maua apandee na siku ya dawa anapga nampa 5000 ya maziwa mbali kingne nasikia blue copper inawafukuza sasa mimi katka dawa za kupuliza ktk bustani naweka blue coper,buster na nyinginezo. Ila bustani ya mboga sitii dawa yoyoteee mboga zangu kama vidudu vmezdi nawagia mkojo wa ng,ombe na mbolea nzuri ni ya kuku wa kisasaaa
 
Back
Top Bottom