Dawa 'inapunguza' maambukizi ya HIV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa 'inapunguza' maambukizi ya HIV

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mtu anayeishi na virusi vya HIV na anayetumia dawa za kupunguza makali punde tu anapogundua,kuliko wakati ambao afya yake imezorota kabisa,anaweza kupunguza kumuambukiza mtu ambaye hana virusi hivyo kwa asilimia 96%, haya ni kwa mujibu wa utafiti.

  Taasisi ya kitaifa ya afya ya Marekani ilifanya utafiti huo kwa wapenzi 1,763 huku katika kila kundi la wapenzi kukiwa na mmoja anayeishi na virusi vya HIV.

  Kutokana na mafanikio yake makubwa,utafiti huo ulisitishwa miaka minne kabla ya muda wake uliopnagwa.

  Shirika la afya duniani WHO linasema utafiti huu ni "mafaniko muhimu".

  Utafiti ulianza mwaka 2005 katika vituo 13 barani Afrika, Asia na Marekani.

  Wanaoishi na virusi vya HIV waliwekwa katika makundi mawili.Katika kundi moja,watu walipewa dawa za kupunguza makali ya HIV mara moja.

  Kundi lengine wakapewa dawa hizo baada ya muda kidogo.

  Makundi yote mawili walipewa ushauri ya kutumia mbinu salama wakati wa kujaamiana,mipira ya kondomu bila malipo na kutibiwa magonjwa yanayopatikana kwa kujaamiana.

  Miongoni mwa wale ambao walianza kutumia dawa hizo mapema kulikuwa na tukio moja tu la wapenzi kuambukizana.

  Katika kundi lengine kulikuwa na matukio 27 ya maambukizi.

  BBC Swahili - Habari - Dawa 'inapunguza' maambukizi ya HIV
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  God The Almighty pleeease deliver us from AIDS..... Dawa mpaka ipatikane watatumia the next two generations.... inakua kama mambo ya bubonic plague miaka ya nyuma ... sometimes naona everything is just the same since the start of time, tunazunguka tu in a circle.... AIDS is our black death....
   
Loading...