Mabobish
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 367
- 282
Dawa yenye picha hapa chini kama inavyojieleza ni dawa Magumashi kabisa, inavyoelekea imewekwa tu majani ya makavu ya kunde au majani ya maharage kisha kuwekwa kwenye karatasi ya rangi na kuuzwa kama dawa ya kutibu maradhi yalioandikwa katika hiyo karatasi.
Dawa hii nimeinunua Dodoma kwa binti mmoja anajiita Subira kwa maelezo yake anasema anaishi maeneo ya Makole lakini siku alipokuwa akiuza alinikuta maeneo ya ChakoniChako Bar, kwa kweli kanilamba takribani 45,000/= kwa paketi moja na niliwachukulia na wenzangu 2 kwa maana ya jumla ya paketi 3 na maelekezo ni kwamba dozi yake ni siku 3 kwa maana ya kijiko cha chai 1x1 kwa siku 3 tu kwa kunywea ktk kinywaji chochote, na matokeo yake yataanza kuonekana Massa 2 na kuendelea tangu kuanza kutumika.
Cha ajabu na kusikitisha tangu tumeitumia zimepita siku 6 hakuna matokeo yoyote chanya zaidi tumetapeliwa na huyo Dada Subira akipigiwa simu japo atoe ufafanuzi tangu alipoelezwa tatizo hapokei simu na wala hajibu meseji jambo linaloashiria anafanya utapeli wa kukusanya hela za watu kwa kuuza dawa fake na huenda ikichunguzwa kiundani inaweza kuwa na madhara makubwa kwa matumizi ya binadamu.
Chonde wenye tatizo kama langu chukueni tahadhali na dawa hiyo hususani na huyo Binti muuzajiView attachment 864987