David Kafulila ndani ya kipindi cha DAKIKA 45 ITV

David Kafulila ndani ya kipindi cha DAKIKA 45 ITV

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Mkumbushe na mwenzio asikose kabisa kusikiliza kipindi hiki muhimu.

Leo saa tatu usiku katika kipindi cha Dk45 cha ITV atakuwepo Mh. Kafulila(MB) akifanya tathimini ya miaka kumi ya JK, Uchumi, Bajeti na Ufisadi na Kwanini UKAWA inatosha Oktoba!

USIKOSE KUMSIKILIZA

Akiwa katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Independent Television (ITV) jumatatu hii ya tarehe 22/6/2015, mbunge wa Kigoma kusini na Waziri Kivuli wa viwanda na biashara Ndg David Kafulila pamoja na kuiongelea tena na tena kashfa ya ufisadi wa IPTL - Tegeta Escrow Account na kuonesha kwamba bunge limeshindwa kuisimamia serikali kwa kuhakikisha kuwa inaleta taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kabla ya uhai wa bunge hili la kumi haujafikia ukingoni wiki mbili zijazo.

Alisema hajaona kuwa hiyo ni moja ya shughuli zitakazofanywa katika ratiba ya shughuli za bunge na kwa mtazamo wake ni kuwa hizo ni harakati Spika Anna Makinda na wasaidizi wake kuibeba na kufunika uozo na ufisadi wa serikali hii chini ya CCM kwa maelezo kuwa ukurasa wa ishu ya Escrow Account ulishafungwa rasmi!!..

Kilichonifurahisha mimi zaidi na kumpa credit huyu bwana ni pale alipoulizwa na mwendesha kipindi Emmanuel Buhohela swali hili ambalo hata wafuasi wa CCM pamoja na viongozi wao wamekuwa wakiliimba sana kwamba; Nyie UKAWA au Upinzani kwa ujumla mmejiandaa kwa kiwango gani kuunda serikali kwa sababu inasemwa na wapinzani wenu kwamba hawaoni na hamna human resource kwa maana ya watu wenye uwezo wa kuja kuwa mawaziri, makatibu wakuu wa wizara nk ili kufanya shughuli za serikali? Na mtakuja kufanya nini cha tofauti ili kuleta ufanisi wa serikali katika kuhudumia wananchi na kukomesha ufisadi, rushwa nk?

Response ya Kafulila ilinifurahisha sana na kwa kweli na kwa mtazamo wangu ndivyo ilivyo.

Alisema hiyo ni hofu ya mabadiliko tu kwa wenzetu na watu wengine. Aliendelea kutiririka kwa kusema kuwa hata wakati Nyerere, Julius Kambarage wakati yuko mstari wa mbele kudai uhuru wa watanganyika kujitawala, wakoloni walikuwa na propaganda kama hizihizi zinazofanywa na CCM chini ya viongozi wake wa leo wakiungwa mkono na mamluki na wafuasi wao.

Alisema UKAWA itafanya kama nchi zingine zilivyofanya kama Rwanda, Kenya, Malawi, Zambia ambako vyama vikongwe vyenye mentality ya ukoloni vilipigwa chini na sasa havipo tena, kwamba UKAWA haitakuja na watu toka sayari nyingine kwa maana ya sijui makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa idara na taasisi za serikali mbalimbali, madaktari, walimu, wahasibu n.k kuja kufanya kazi katika serikali yao bali watu ni hawahawa waliopo bali kitakochofanyika ni kubadili "MINDSET" na "MIFUMO" ya utendaji kazi wa watu na hasa watumishi wa umma ili kuleta tija na ufanisi katika uzalishaji na utendaji ili kutoa huduma bora, za haraka na kwa wakati kwa wananchi.

Akumuuliza mtangazaji hili; kwamba unafikiri ni kwa nini wewe una rafiki yako mmemaliza naye shahada ya chuo kikuu katika fani ile, yeye akaajiriwa serikalini na wewe katika taasisi binafsi labda VODACOM na wewe ukawa na ufanisi wa hali ya juu wakati mwenzio ikawa opposite? Ni kwa sababu ya usimamizi na mifumo ya utendaji kuwa tofauti, katika sekta binafsi watu wanapimwa katika utendaji wao na kulipwa vyema ili hali chini ya serikali hii system nzima iko corrupted kuanzia kwa Rais mwenyewe hadi huku chini kabisa, hakuna wa kumfunga paka kengele, wote wameoza!.

Kwa hili tu nilimpa credit Kafulila na nilimkubali na namwombea arudishwe tena bungeni na wana Kigoma Kusini na panapo majaliwa aje kuwa Waziri kamili chini ya Serikali itakayoundwa na UKAWA.
 
Mkumbushe na mwenzio asikose kabisa kusikiliza kipindi hiki muhimu.

Leo saa tatu usiku katika kipindi cha Dk45 cha ITV atakuwepo Mh. Kafulila(MB) akifanya tathimini ya miaka kumi ya JK, Uchumi, Bajeti na Ufisadi na Kwanini UKAWA inatosha Oktoba!

USIKOSE KUMSIKILIZA
 
Watu kama hawa vichwa wa ukawa ndio wakuwasikiliza
Maana akianza ni kutema madini mwanzo mpaka mwisho
Na leo anamvua JK nguo kwa mara ya pili.
 
Mimi niko safari kwa kweli natamani kulia huyo dogo huwa anaongea kama mwalimu vile yaani
Huwa kuna marudio?
 
Mkumbushe na mwenzio asikose kabisa kusikiliza kipindi hiki muhimu.

Leo saa tatu usiku katika kipindi cha Dk45 cha ITV atakuwepo Mh. Kafulila(MB) akifanya tathimini ya miaka kumi ya JK, Uchumi, Bajeti na Ufisadi na Kwanini UKAWA inatosha Oktoba!

USIKOSE KUMSIKILIZA
Na huyu Mwanahabari Huru aliyeandika hii thread ni nani?
Dunia hii kweli watu ni wawili wawili kwa sababu hata heading ya thread yake inafanana na heading ya thread yako!

Kwa mwendo huu, sidhani kama Jamiiforums ina member 268, 717!
 
Siasa bwana za Tanzania lazima uwe mwendawazimu nafikiri ndio maana tunasuasua maana kuna uwendawazimu mwingi.

LEO SISIMIZI ana mashiko kwa upande wa pili, duu.

Hii inatafsri moja tu nayo nii....
 
Namsikiliza hapa anaongelea anazungumzia escrow na mwenendo wa bunge
 
Wakuu kama hamtajali nasi mutujuze kiaina maana wengine tupo mbali na luninga.
 
Na huyu Mwanahabari Huru aliyeandika hii thread ni nani?
Dunia hii kweli watu ni wawili wawili kwa sababu hata heading ya thread yake inafanana na heading ya thread yako!

Kwa mwendo huu, sidhani kama Jamiiforums ina member 268, 717!

Ndio utandawazi huo mkuu
 
Huyu jamaa ni kichwa aisee, yani ana vitu vingi tena vya msingi, hata akihojiwa siku nzima, huwezi choka kumsikiliza, big up bro D.Kafulila
 
Hana majibu ya maswali anayoulizwa anatumika tu na Bado atatumika sana Maana Mzee Mengi na yeye wanasomana kwenye frequency moja!
 
Hana jipya zaidi ya escrow aliyoiokota kwenye gazeti la citizen
 
Mkuu na hiyo alikua anachomekewa na mafisadi wanaomfadhili, nenda uvinza jimboni kwake ndo utajua huyu anatumika!

Yeah hata harusi yake ilifadhiliwa na kitengo cha mafisadi walionyimwa acces ya kuzipiga zile hela, hadi gari la harusi.
 
Back
Top Bottom