David Kafulila ndani ya kipindi cha DAKIKA 45 ITV

David Kafulila ndani ya kipindi cha DAKIKA 45 ITV

Mkuu hata ile issue ya kubakia kwenye chama alipotaka kung'olewa na viongozi wake wa chama waliomtetea abaki ni mafisadi wanaomtumia kama Remote!
 
Mkuu Kinjikitile mbona mambo anayo ongea yanaeleweka, hii nchi watumishi na viongozi tulio wapa dhamana ni wavivu kufanya kazi na kufikri balaa, hakuna ubunifu wala bidii ktk kazi. Hili ni tatizo wengi wanawaza wizi tu, na hii inasababishwa na viongozi ovyo na legelege tulio nao.
 
Hana majibu ya maswali anayoulizwa anatumika tu na Bado atatumika sana Maana Mzee Mengi na yeye wanasomana kwenye frequency moja!

Kijana Kafulila anasomeka vizuri sana ila uelewa wa mfuatiliaji ni muhimu. Upeo mdogo uelewa mdogo. Wanakigoma chondechonde Hakikisheni Kafulila anarejea bungeni uchaguzi wa oktoba, ni kichwa kinachowakilisha mamilioni ya watanzania wanyonge wa nchi hii.
 
Kijana Kafulila anasomeka vizuri sana ila uelewa wa mfuatiliaji ni muhimu. Upeo mdogo uelewa mdogo. Wanakigoma chondechonde Hakikisheni Kafulila anarejea bungeni uchaguzi wa oktoba, ni kichwa kinachowakilisha mamilioni ya watanzania wanyonge wa nchi hii.

Tatizo hakuna alichofanya jimboni kwake, labda mafisadi wakamuingize ili awatete!
 
Wewe naona utakua Kafulila teh teh njaa zitakuua elezea posho ya ubunge umekaataa kuchukua?

Wacha propaganda za kitoto hizo zimepitwa na wakati...kuliko kutumika vibaya ni kheri ungewashauri wanaokutumia vibaya wajiandae kisaikolojia kukabidhi nchi kwa UKAWA kwa amani na utulivu ifikapo Oktoba 2015
 
Na huyu Mwanahabari Huru aliyeandika hii thread ni nani?
Dunia hii kweli watu ni wawili wawili kwa sababu hata heading ya thread yake inafanana na heading ya thread yako!


Kwa mwendo huu, sidhani kama Jamiiforums ina member 268, 717!
Mkuu hii ndo JF, Yaani never take JF serious, utaumia na moyo wako.
Maana mtu akipigwa ban huku anafunua ID nyingine
 
Akiwa katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa na Independent Television (ITV) jumatatu hii ya tarehe 22/6/2015, mbunge wa Kigoma kusini na Waziri Kivuli wa viwanda na biashara Ndg David Kafulila pamoja na kuiongelea tena na tena kashfa ya ufisadi wa IPTL - Tegeta Escrow Account na kuonesha kutoridhishwa na bunge ambalo kimsingi linaundwa na wabunge wengi wa CCM kuisimamia serikali kwa kuhakikisha kuwa inaleta taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya bunge kabla ya uhai wa bunge hili la kumi haujafikia ukingoni wiki mbili zijazo.

Alisema hajaona ktk ratiba ya shughuli za bunge kuwa hiyo ni moja ya shughuli zitakazofanywa na kwa mtazamo wake ni kuwa hizo ni harakati Spika wa bunge Anna Makinda na wasaidizi wake kina Job Ndugai, Mussa Zungu, Lediana Mng'ong'o na Samia Suluhu kuibeba na kufunika uozo na ufisadi wa serikali hii chini ya CCM kwa maelezo kuwa ukurasa wa ishu ya Escrow Account ulishafungwa rasmi!!..

Kilichonifurahisha zaidi na kumpa credit huyu bwana ni pale alipoulizwa na mwendesha kipindi Emmanuel Buhohela swali hili ambalo hata wafuasi wa CCM pamoja na viongozi wao wamekuwa wakiliimba sana kwamba; Nyie UKAWA au Upinzani kwa ujumla mmejiandaa kwa kiwango gani kuunda serikali kwa sababu inasemwa na wapinzani wenu kwamba hawaoni na hamna human resource ya kutosha kwa maana ya watu wenye uwezo wa kuja kuwa mawaziri, makatibu wakuu wa wizara nk ili kufanya shughuli za serikali? Na mtakuja kufanya nini cha tofauti zaidi ya haya yanayofanywa na serikali chini ya CCM ili kuleta ufanisi zaidi wa serikali katika kuhudumia wananchi na kukomesha ufisadi, rushwa nk?

Response ya Kafulila ilinifurahisha sana na kwa kweli na kwa mtazamo wangu ndivyo ilivyo.

Alisema hiyo ni hofu ya mabadiliko tu kwa wenzetu na watu wengine. Aliendelea kutiririka kwa kusema kuwa hata Julius Kambarage Nyerere wakati yuko mstari wa mbele kudai uhuru wa watanganyika wa kujitawala, wakoloni walikuwa na propaganda kama hizihizi zinazofanywa na CCM chini ya viongozi wake wa leo wakiungwa mkono na mamluki na wafuasi wao.

Alisema UKAWA itafanya kama nchi zingine zilivyofanya kama Rwanda, Kenya, Malawi, Zambia ambako vyama vikongwe vyenye mentality ya ukoloni vilipigwa chini na sasa havipo tena, na kwamba UKAWA haina kuwa itakuja na watu wake toka sayari nyingine kwa maana ya makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa idara na taasisi za serikali mbalimbali, madaktari, walimu, wahasibu n.k ili kufanya kazi katika serikali yao bali watu na watumishi wa umma ni hawahawa waliopo bali kitakochofanyika ni kubadili "MINDSET" na "MIFUMO" ya utendaji kazi wa watu na hasa watumishi wa umma ili kuleta tija na ufanisi katika uzalishaji na utendaji ili kutoa huduma bora, za haraka na kwa wakati kwa wananchi.

Akamuuliza mtangazaji hili; Kwamba unafikiri ni kwa nini wewe una rafiki yako mmemaliza naye shahada ya chuo kikuu katika fani ileile, yeye akaajiriwa serikalini na wewe katika taasisi binafsi labda VODACOM na wewe ukawa na ufanisi wa hali ya juu na mwenzio wa serikalini ikawa ni opposite?

Ni kwa sababu ya usimamizi na mifumo ya utendaji kuwa tofauti, katika sekta binafsi watu wanapimwa katika utendaji wao na kulipwa vyema ili hali chini ya serikali hii system nzima iko corrupted kuanzia kwa Rais mwenyewe hadi huku chini kabisa, hakuna wa kumfunga paka kengele, wote wameoza!.

Kwa hili tu nilimpa credit Kafulila na nilimkubali na namwombea arudishwe tena bungeni na wana Kigoma Kusini na panapo majaliwa aje kuwa Waziri kamili chini ya Serikali itakayoundwa na UKAWA.
 
Kafulila ni miongoni mwa wale National MP.Kigoma kusini muelewa Kafulila hadhi yake tena sio jimbo hivyo hapo jimbo anapitia tu.. but his for the national interest.
 
Dogo anao uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuielezea Tanzania kiufasaha sana
Maana anaeleza sababu na solutions
 
Ningependekeza kafulila awe anapewa kila tuzo inayotolewa TZ...kuanzia za kili na kuendelea ili watu tusisahau mchango wake kwa taifa hili
 
Ningependekeza kafulila awe anapewa kila tuzo inayotolewa TZ...kuanzia za kili na kuendelea ili watu tusisahau mchango wake kwa taifa hili

Haka kajamaa kako vizuri kwa kweli
 
Kwa kweli nimemvulia Mhe. Kafulila kofia pale alipotuamsha kutoka usingizini kuhusu Makampuni ya Simu yanavyotuibia. Ameendelea kusema kuwa aliwashauri Serikali kuwa Makampuni haya kwanza yajisajili katika Masoko ya Hisa ili Watanzania pia yapate kuyamiliki lakini mpaka leo hilo halijafanyika. Pili, aliwashauri Serikali kuwa inunuliwe mtambo utakaorekodi gharama ya simu yeyote itakayopigwa ili iwezeshe Serikali kupata kodi stahiki lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika na ameenda mbali kuwa nchi kama Rwanda wanao mtambo kama huu wa kurekodi gharama ya simu yeyote inayopigwa. Mimi nadhani kuna tatizo hapo. Mawazo mazuri kama hayo kwa nini Serikali isiifanyie kazi?.
 
Kwa kweli nimemvulia Mhe. Kafulila kofia pale alipotuamsha kutoka usingizini kuhusu Makampuni ya Simu yanavyotuibia.

Ameendelea kusema kuwa aliwashauri Serikali kuwa Makampuni haya kwanza yajisajili katika Masoko ya Hisa ili Watanzania pia yapate kuyamiliki lakini mpaka leo hilo halijafanyika.

Pili, aliwashauri Serikali kuwa inunuliwe mtambo utakaorekodi gharama ya simu yeyote itakayopigwa ili iwezeshe Serikali kupata kodi stahiki lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika na ameenda mbali kuwa nchi kama Rwanda wanao mtambo kama huu wa kurekodi gharama ya simu yeyote inayopigwa. Mimi nadhani kuna tatizo hapo.

Mawazo mazuri kama hayo kwa nini Serikali isiifanyie kazi?.
 
Acha waswahili waibiwe tu,tumechoka.
 
Back
Top Bottom