David Jairo bado anatanua serikalini

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,280
310
Jamani leo asubuhi nimekutana na David Jairo, kilichonishangaza ni kumkuta anatumia gari la serikali Landcruiser V8 wakati nilijua ametolewa serikalini moja moja. nimeshindwa kuelewa sasa anatumia gari yetu, mafuta yetu, dereva wetu sisi watanzania walipa kodi ambao alitusaliti, anatumia kwa misingi gani hivi kapewa cheo gani cha siri huko serikalini ambako sisi watanzania ambao tunatakiwa kumiliki hiyo serikali hatuna SAUTI hata kiduchu mpaka wakati wa uchaguzi ndo tunaambiwa serikali ni yetu si kama inamilikiwa na watu wachache wenye jeuri na kiburi na wanatufanya tuzidi kuwa maskini siku baada ya siku.
 
Mabosi wake wote wapo kazini Ulitegemea nini Comrade? Siku yao inakuja usiwe na shaka coz ushahidi tunao basi kuna watu watasikika kwa Moreno Ocampo na wengine wataozea ukonga +keko
 
Nina hamu sana siku hiyo ifike, maana watu wamefanya serikali ni ya kikundi fulani tu cha watu ili kula na kusaza kodi zetu, huku wenye nchi halisi tupo tu nakuona sawa tu na kodi tunayotoa wala hatuionei uchungu utafikiri hatuipati kwa jasho, sijui ndo ujuha
 
ni mtumishi wa tiss tumefanya nae kazi dodoma zamani akiwa bado na mke wake mkubwa
 
I saw him recently "pulling" ML. I belive he is doing just fine. One thing that rulers in this country have lost is SHAME And what they have gained is IMPUNITY.
 
Jamani leo asubuhi nimekutana na David Jairo, kilichonishangaza ni kumkuta anatumia gari la serikali Landcruiser V8 wakati nilijua ametolewa serikalini moja moja. nimeshindwa kuelewa sasa anatumia gari yetu, mafuta yetu, dereva wetu sisi watanzania walipa kodi ambao alitusaliti, anatumia kwa misingi gani hivi kapewa cheo gani cha siri huko serikalini ambako sisi watanzania ambao tunatakiwa kumiliki hiyo serikali hatuna SAUTI hata kiduchu mpaka wakati wa uchaguzi ndo tunaambiwa serikali ni yetu si kama inamilikiwa na watu wachache wenye jeuri na kiburi na wanatufanya tuzidi kuwa maskini siku baada ya siku.
Tatizo ni TISS iliyochini ya ccm
 
Mambo aliyofanya Jairo, kama ni kweli alifanya, ni zao na system mbovu iliyopo
Tatizo letu ni kudhani Jairo akitoka mambo yatakuwa sawa
Kinachitakiwa kutoka ni system/mfumo mzima unaowezesha watu kuwa na jeuri hiyo na uthubutu wa kufanya yale anayotuhumiwa.
Mwenye mamlaka hayo ni Wa-tanzania
Tatizo la wa-Tanzania hawajui wana mamlaka hayo, hawajui nguvu ya kura ya kila mmoja wetu katika kuikabili mifumo miovu
Wewe na mimi na wengine wachache yawezekana tumezaliwa kabla ya wakati...tupo katikati ya watu wanaonunulika, wabadhirifu na wadhaifu na ni wengi
 
Mwache Jairo atanue. RACHEL WAKO WAPI? EPA, Rich- Mond..., Meremeta and the list goes..loh najisikia kutapika
 
Kwani alifukuzwa kazi lini?
Si Mkwele amempangia pengine pa kufisidi?
acha wenye nchi wale nchi yetu, wanywe jasho letu, walale kwenye mifupa yetu. lakini kwanini tusikatae kwa nguvu zote? hivi watanzania wote tukiamua kwenda ikulu kuchukua kura zetu hatuwezi kupewa? Mbona mbeya wakati fulani walikataa kunyanyaswa wakaweza? ccm walipeleka majeshi ya mikoa miwili yaani iringa na mbeya mbona walishindwa kuhimili nguvu ya umma? Watanzania tufike hatua tukatae!!!!!!
 
Jamani leo asubuhi nimekutana na David Jairo, kilichonishangaza ni kumkuta anatumia gari la serikali Landcruiser V8 wakati nilijua ametolewa serikalini moja moja. nimeshindwa kuelewa sasa anatumia gari yetu, mafuta yetu, dereva wetu sisi watanzania walipa kodi ambao alitusaliti, anatumia kwa misingi gani hivi kapewa cheo gani cha siri huko serikalini ambako sisi watanzania ambao tunatakiwa kumiliki hiyo serikali hatuna SAUTI hata kiduchu mpaka wakati wa uchaguzi ndo tunaambiwa serikali ni yetu si kama inamilikiwa na watu wachache wenye jeuri na kiburi na wanatufanya tuzidi kuwa maskini siku baada ya siku.

Katika nchi inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora mambo kama haya tunayoshuhudia hayawezi kutendeka lakini serikali inayoendeshwa na wezi haya mambo wanayofanya hawa jamaa hayawanyimi usingizi!
 
Back
Top Bottom