Date my Family Tanzania: Vionjo, ukakasi na uelewa finyu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Fursa zipo kila mahali , kinachotakiwa ni jicho tu la kuziona na kuzifanyia kazi..baada ya hapo unatulia na kula hela...

Date my family Tanzania ipo nchi zingine pia kwa majina ya hizo nchi.. Ni mwanzo wa enzi mpya za kutafuta wenza...kwa njia ya kujitangaza wazi... Hapo mwanzo haya mambo ni mashkolo mageni kabisa.. Utandawazi umerahisisha mengi

Date my family Tanzania ni kitu chema kwa watufutao wenza lakini wengi hawajui ama hawana uzoefu ama hawako makini kwa kile wakitakacho...maswali wanayouliza ni ya kawaida sana
Mahusiano yako ya mwisho yalikuwaje?
Una mtoto?/ watoto?
Unapendelea nini
Hupendi nini?

Ukakasi
Vigezo navyo mmh kila mtu na ladha zake..lakini kubwa na baya lenye ukakasi ni urefu kwenda chini hili nimeliona kwa wadada karibia wote ...hawataki wanaume wafupi vijeba.. Hii ni kasoro kubwa sana..hao wafupi mnataka wawaoe kina nani?
Mabrazeni nao swali linalojirudia rudia sana ni mdada kuwa na mtoto...hapa kuna hasi na chanya
Mdada kutokuwa na mtoto kuna maana kuwa kajitunza sana(haya ndio mawazo ya vijana wengi) lakini je ndio uhalisia?
Kuna ambao hawana watoto lakini wameshatoa mimba sana...
Kuna ambao hawana watoto pengine hawana uzazi , ni tasa..!!
Kuna ambao hawana watoto ni warukwa ukuta maarufu
Hili la mtoto lina ukakasi sana...!!!!

Uelewa duni....
Zaidi ya vigezo vya kawaida lakini wengi hawaulizi
Magonjwa ya kurithi kwenye familia
Laana za kifamilia/ koo
Haiba ya familia, mitazamo na fikra chanya
Wengi wake kwa waume wanapenda wenza wenye hofu ya Mungu...je kuwa na hofu ya mungu kunatosha kupata mwenza bora.?
Kazi ..wengi wanaulizia kazi ya mhusikaa..pengine hili ni muhimu lakini si lazima..kuna kazi za mkataba..ukiisha umeisha..
Matumizi ya vilevi nk

Vionjo
Je date my family ni kutaniko la ma x? Maana wote hakuna ambaye hana background...wote walishawahi kuwa na wenza..na wengi hujionesha kuwa wao hawakuwa wakosa kwenye mahusiano yaliyovunjika...

Nitarejea...
 
Hapo kwenye kujionesha kuwa hawakuwa na makosa kwenye mahusiano yaliyopita nakubaliana na wewe kabisa! Wengi wanasema nilikuwaga na ex wangu ila tuliachana sababu alikuwa na tabia fulani abc ambazo ni mbaya sasa huwa najiuliza ina maana wote wale hawakuwa na matatizo kabisa au ndiyo kuogopa watakosa wenzi endapo watajisema makosa yao!

Cc Heaven Sent
 
Hongera kwa kununua Diesi tivii ila tambua zile ni reality show wanaweza wakawa wana igiza tu

Ukitazama date my family zambia ,Botswana , Nigeria huko si ndo utajua ni acting tu

Na kuna season 8 inakaribia kuamza
 
Hongera kwa kununua Diesi tivii ila tambua zile ni reality show wanaweza wakawa wana igiza tu

Ukitazama date my family zambia ,Botswana , Nigeria huko si ndo utajua ni acting tu

Na kuna season 8 inakaribia kuamza
Nipe hongera na kununua tiiviii
 
Umenena

Mahusiano yoyote lazima yawe two way street
Goods n Bads
Huwezi kuanza mahusiano mapya ukijieleza 'ulionewa sikumkosea Alinikosea mmmh'
Wanawake tuna hulka ya kunyooshea vidole wanaume Tunapenda kuuvaa unyonge pale unapojaribu kuficha madhaifu yako....
Back kwenye mada
Ukakasi
Ni vyema Mwanamke ukajua ni muhimu kujitambua kama wote lengo ni kukuza familia basi ni jukumu la pande zote mbili.....sawa mwanamke anaweza akawa alitoa mimba nyingi au ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu hawezi kuzaa lakini pia Wanaume wana mapungufu hayo hayo (mwanaume anaweza kuwa aliugua magonjwa ya zinaa kukampelekea kupoteza uwezo wa kuzaa au ukawa ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu)
Laana ni vigumu kutambua labda mpaka muishi pamoja (sijui lakini)
Ni hayo tu Mkuu
 
Nimetoka kukiangalia mda si mrefu hapa, ni kipindi kizuri kukutanisha watu maana watu bana mnaweza kukutana popote na mkaja kuoana. So mazingira ya kukutana hayajalishi kivile

Shida niliyoiona hapo ni umri maana kwa mwanaume wa 20 yrs kibongo bongo bado ni mdogo kuanzisha mahusiano yale ya serious kuelekea ndoa ndio maana maswali yao yanakua ya kitoto sana
 
Back
Top Bottom