DAS Asenga alitangaza ziwa 'Chala' Rombo

ray jay

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,084
485
Nimemsikia kijana akizungumza Radio Kill FM umuhimu wa Watanzania kutembekea ziwa Chala kwa Utalii wa Picha na kuogelea.

Amepost kwenye ukurasa wake haya:

Hapa palikuwa Mlima, Mzee Chala alikuwa akiishi na familia yake juu ya Mlima.
Ilipotokea Volcano akatitia yeye, nyumba yake na familia yake hadi Leo hawajaonekana, likajizalisha Ziwa unaloliona na linaitwa Ziwa Chala

Kina chake urefu wa viwanja vya mpira Mara 3 (Mita 300) robo tatu ya Ziwa ipo Tanzania na robo ipo Kenya. Ni Ziwa la maji baridi watu wanakunywa, halina samaki wengi wala wadudu zaidi ya kaa. Watalii na wanaojua kuogelea huogelea.

Halina Pwani, linafanya kuwa Ziwa hatari kabisa kwa wasiojua kuogelea.

NJOO ROMBO
UFANYE UTALII WA NDANI.
ROMBO KUNA KIYOYOZI CHA ASILI.

KAZI KAZINI

Jamani kweli Tanzania tumebarikiwa.
7ec9138060bfce5410cc0bc38ecf832d.jpg
 
Hilo ziwa ni hatari sana kwa kuogelea tena kuna vibao vya swim at your own risk,weka mbali na watoto,ila kwa muonekano linavutia
 
Ziwa Chala ni hatari sana kwa asie jua kuogelea, ukipiga hatua moja umezama,......

Lina historia ya kuuaua wanakijij,.....

Kuna mwaka mwanafunzi alienda na mchumba wake, msichana akaingia kuogelea awez, ikabid jamaa aende kumuokoa matokeo yake mschana akamng'ang'ania jamaa Wakafa wote.......!

Pia kuna Mzungu alishawai kuliwa namba japo walisema wamewaua wote.... .
 
Mwaka jana mabinti wawili wa sekondari kutoka familia moja walifia Chala
 
Back
Top Bottom